Mhandisi wa Kampuni ya Simu
Tanzania (TTCL), Paul Magembe akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, kuhusu mitambo ya kutolea
huduma za kifedha iliyopo katika ofisi za Kampuni hiyo mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya
watendaji wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), alipokuwa akikagua mitambo
ya kutolea huduma za kifedha iliyopo katika ofisi za Kampuni hiyo
mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa
Shirika la Posta Nchini, kanda ya Dodoma Bw. Laurent Thobias (kulia),
kuhusu utoaji wa matangazo ya huduma ya Posta mlangoni katika ofisi za
Shirika hilo mkoani humo.
Meneja wa Wakala wa Ufundi na
Umeme Nchini (TEMESA), Mkoa wa Dodoma, Eng. Bikulamchi Liberatus, akitoa
ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame
Mbarawa, kuhusu mikakati ya utengenezaji wa magari katika karakana
iliyopo Mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na watumishi wa taasisi
zilizo chini ya Wizara hiyo (hawapo pichani), alipokutana nao Mkoani
Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Taasisi za
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, wakimsikiliza Waziri wa
WIzara hiyo (hayupo pichani), alipokutana nao kuwapa mikakati ya
utendaji wa Wizara hiyo, Mkoani Dodoma,
………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL) kujipanga na kuanza mkakati wa kutangaza huduma za fedha ambazo
zitatolewa na kampuni hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao.
Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo
baada ya kukagua mitambo itakayotumika kwa huduma hiyo ambayo itaongeza
ushindani wa biashara kwenye huduma za simu nchini mkoani Dodoma.
“Lazima mjipange kwenye idara ya
masoko kwa kuanza kutangaza huduma hiyo kupitia njia zote zikiwemo
mitandao ya kijamii, ili wananchi warahisishiwe huduma za fedha kupitia
TTCL”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha, ameiagiza kampuni hiyo
kupitia idara ya masoko kujipanga kuona fursa zilizopo kwa kufahamu
mahitaji ya wateja wao na kuhakikisha inaongeza wateja katika mkoa huo
ili kuteka soko la ushindani ambapo Serikali inajipanga kuhamia huko.
Waziri Prof.Mbarawa ametaja baadhi
ya maeneo ambayo TTCL inahitaji kuboresha zaidi ni upande wa Simu
(Voice) na Data (video) ili kuweza kurahisisha mawasiliano kwa njia ya
video conference kwa kuwa kuna baadhi ya watendaji wengine watabaki Dar
es salaam.
“Mkiimarisha mawasiliano upande
wa data mtarahisisha hata maamuzi na pia kazi zitaenda vizuri Serikalini
hasa ukizingatia baadhi ya watumishi watakuwa hapa Dodoma na wengine
Dar es Salaam”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Sambamba na hilo, Waziri Mbarawa
ameliagiza Shirika la Posta nchini kuja na mkakati wa kuandaa matangazo
ya kutambulisha huduma ya Posta mlangoni kwa jamii ili kuiwezesha
huduma hiyo kutambulika kirahisi.
Amesisitiza kwa Taasisi hizo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ili kufikia malengo waliojiwekea na kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Amesisitiza kwa Taasisi hizo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ili kufikia malengo waliojiwekea na kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Akiwa mkoani humo Prof. Mbarawa
amemhakikishia Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana kuboresha miundombinu
nchini hususan katika mkoa huo ikiwemo kuboresha usafiri wa anga katika
uwanja wa ndege wa Dodoma ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kuruka na
kutua.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mbarawa ameongea na watendaji pamoja na wafanyakazi wa Taasisi zilizo
chini ya Wizara yake na kusisitiza kufanya kazi kwa kasi, uadilifu,
ubunifu na kushirikiana katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku.
Akizungumza kwa niaba ya
wafanyakazi hao Meneja wa Wakala wa Majengo(TBA) mkoani humo, Arch.
Masalu Bururu, amemuahidi Waziri huyo kutekeleza yale yote aliyowà agiza
ili kuleta ufanisi na tija kwa Taifa.
Waziri Prof. Mbarawa amemaliza
ziara yake ya siku kumi katika mikoa ya Mwanza, Mara, Arusha, Manyara na
Dodoma ambapo ametembelea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na
Wizara hiyo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments :
Post a Comment