Katibu wa Shirikisho la Muziki
Tanzania Bw.John Kitime kulia akizungumza katika semina iliyoandaliwa
na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) juu ya Elimu ya Mlipa Kodi.Kulia
kwake ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) Bw.Simon Mwakifamba.
Viongozi mbalimbali kutoka
COSOTA,BASATA,Bodi ya Filamu,Shirikisho la Filamu Nchini(TAFF) na
Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF) wakipata Elimu ya Mlipa kodi kutoka
kwa maafisa wa Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Huduma na Elimu kwa
mlipa kodi za ndani wa TRA Bw.George Haule akizungumza na wasanii wa
filamu na Muziki nchini juu ya Umuhimu wa Kulipa kodi na kusajili mali
zao ili wachangie katika pato la Taifa.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
nchini Bi.Joyce Fissoo akiskiliza mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasiliswa na maafisa wa mamlaka ya mapato nchini(TRA) wakati wakitoa
elimu ya mlipa kodi kwa wasanii wa Filamu na Muziki iliyofanyika Jijini
Dar es Salaam.
Wasanii mbalimbali wa Filamu na
Muziki wa nchini wakiwa makini kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasiliswa na maafisa wa mamlaka ya mapato nchini(TRA) leo Jijini Dar
es Salaam.Wasanii hao wamepata elimu ya mlipa kodi.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma
na Elimu kwa mlipa kodi Bi.Diana Masalla akizungumza na baadhi ya
wasanii wa Filamu na Muziki nchini juu viwango mbalimbali vya Kodi
wanavyolipa wafanyabishara nchini.
Rais wa Shirikisho la Muziki
Tanzania (TMF) Bw.Addo Novemba akichangia jambo wakati wa semina kwa
wasanii wa filamu na Muziki iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) juu ya Elimu ya Mlipa Kodi.
………………………………………………………………………………
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)
imewaasa wasanii wa Filamu na Muziki kurasimisha kazi zao ili
zitambulike na hivyo kuwasaidia katika kujiongezea vipato vyao wenyewe.
Hayo yamesemwa na Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Bi.Diana
Masalla wakati wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo kwa wasanii wa
Filamu na Muziki leo Jijini Dar es Salaam.
“Tumeamua kuwaandalia warsha hii
ili muweze kupata uelewa juu ya suala zima la urasimishaji wa kazi zenu,
kwa kuziwekea Stamp na kulipa Kodi ya mapato’’, Alisema Bi. Masalla.
Aidha ametoa wito kwa wasanii hao
kujitokeza na kuwafichua wale wote ambao wanauza CD feki bila idhini
yao kwani itawasaidia kujipatia kipato kupitia jasho lao na zaidi
uwekaji wa stika utaisaidia kupata haki yao na Serikali kupata kodi kwa
ajili ya maendeleo ya nchi.
Aidha kwa upande wake Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini (KBF). Bi.Joyce Fissoo amesema kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kurasimisha Sekta ya Filamu nchini
kwa kuwa sekta hii imekuwa mkombozi mkuu wa Ajira nchini na hivyo
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Filamu wataweka kipaumbele
katika kuweka adhabu stahili ili zichukuliwe kwa wezi wa kazi za wasanii
hawa.
Mbali na hayo Mamlaka ya Mapato
nchini (TRA) imesema kuwa semina hizi zitakuwa endelevu na hivyo makundi
mbalimbali nchini na wadau watapata elimu hii muhimu kwa mlipa kodi na
hivyo kusaidia sekta hii kusonga mbele na pia kuchangia pato la Taifa.
No comments :
Post a Comment