Mwenyekiti wa Taasisi ya Kidini
ya Lohana Mahajan Bw.Navin Kanabal akitia saini katika moja ya nyaraka
wakati taasisi hiyo ilipokabidhiwa tiketi za Shirika la Ndege la ATCL
kwa ajili ya safari ya wachezaji wake kwenda Kisumu Nchini Kenya ambapo
tarehe 23 /12/ 2016 huu jumla ya wachezaji 49 watasafiri wa kwa ndege
ya shirika hilo kwa ajili kushiriki tamasha la michezo ambalo
litafanyika nchini humo na kurejea tarehe 27/12/2016.
Akizungumza katika makabidhiano
hayo ya tiketi Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Bw.
Edward Nkwabi ameishukuru taasisi hiyo kwa kutambua na kusafiri kwa
ndege za Shirika la Ndege la ATCL kwani itakuwa njia bora na nzuri ya
kuanza kujitangaza kimataifa kwa kuanzia katika nchi zetu wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa ATCL itatoa huduma
bora kabisa wakati wa safari yao ya Kwenda Kisumu Kenya na Kurudi
nchini ili wakati mwingine wasafiri na ndege za ATCL Ameongeza kwamba
kwa sasa Ndege za shirika hilo zinatoa huduma ya usafiri wa anga katika
viwanja vya Songwe, Bukoba, Mwanza, Kilimanjaro , Zanzibar na Comoro na
hapo baadaye wataongeza huduma katika viwanja vya Dodoma na Arusha,
Tabora Mtwara pamoja na Mpanda.
Hafla ya makabidhiano ya tiketi
hizo imefanyika kwenye Mgahawa wa AKEMI uliopo jengo la Golden Tower
jijini Dar es salaam, Katika pichwa wanaoshuhudia tukio hilo ni
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Bw. Edward Nkwabi wa
pili kutoka kulia, James Mbago Meneja Mauzo na Usambazaji, na
aliyesimama nyuma ni Katibu wa Taasisi ya Lohana Mahajan Bw.Sanjit
Ramji.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kidini
ya Lohana Mahajan Bw.Navin Kanabal akipokea tiketi kutoka kwa Mkurugenzi
wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Bw. Edward Nkwabi kwa ajili ya
wanakikundi wenzake 48 kwa ajili ya safari ya kwenda na kurudi Kisumu
nchini Kenya kwa ajili ya Tamasha la Michezo litakalofanyika nchini
humo.
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo
ya Biashara ATCL Bw. Edward Nkwabi akimkabidhi tiketi Meneja wa timu ya
Lohana Mahajan Bi. Sona Thakrar.
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo
ya Biashara ATCL Bw. Edward Nkwabi akiwa katika picha ya pamoja na
maofisa wenzake kutoka shirika la ndege la ATCL baada ya kumalizika kwa
hafla hiyo.
No comments :
Post a Comment