Saturday, December 3, 2016

WAHARIRI WATEMBELEA MIRADI YA UKARABATI MIUNDOMBINU YA UMEME DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (aliyenyoosha kidole), akifafanua jambo wakati wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya wahariri kutembelea miradi ya ukarabati wa miundombinu ya usambazaji umeme jijini Dar es Salaam, Desemba 3, 2016.
Mhandisi Mramba akiwa na wahariri na waandishi kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha City Centre

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAHARIRI wa vyombo vya habari nchini, wametembelea miradi ya ukarabati wa miundombinu ya usambazaji umeme jijini Dar es Salaam leo Desemba 3, 2016, ili kujionea hatua zinazochukuliwa na shirika hilo katika kuboresha hali ya upatikanaji umeme jijini.
Akiongea wakati wa ziara hiyo ambayo iliwawezesha wahariri hao kutembelea vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Muhimbili, kituo kipya cha City Centre, kituo cha Sokoine Drive, kituo cha Ilala Mchikichini na kituo cha kuratibu na kudhibiti mifumo ya umeme jijini kilichoko Mikocheni.
“Dhana ya kujenga uchumi wa viwanda ni dhana inayotekelezeka na ushahidi wa wazi ni kiasi cha uwekezaji uliowekwa na serikali kwenye sekta ya umeme,” alisema Mhandisi Mramba.
Alisema hivi miradi hiyo ya kuboresha miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imehusisha ufungaji wa vifaa vipya kabisa.
“Tumeona kituo hiki cha Ilala, upanuzi mkubwa unafanyika hapa kwa ushirikiano na serikali ya Japan, City centre kinatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya Japan na Finland, kituo cha Sokoine kwa ushirikiano na African Development Bank, kituo kipya cha Muhimbili kwa ajili ya kutoa huduma kwenye hospitali ya taifa Muhimbili, Taasisi ya Moi na Taasisi ya Jakaya Kikwete, pamoja na chuo kikuu cha Muhimbil Kituo cha kudhibiti mifumo ya umeme cha Mikocheni kinachosimamia mifumo yote ya umeme kwa jumla ukilinganisha  vituo vyote vya distribution, (usambazaji), ukaunganisha na vituo vya uzalishaji umeme kama vile Kinyerezi I na II, ukaunganisha na vituo vya transmission (kusafirisha) Backborne, Makambako-Songea na miradi mingine mingi, vitafanya nchi yetu iweze kupata umeme wa kutosha.” Alifafanua.
Mhandisi Mramba pia aliwaambia wahariri hao kuwa agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, wa kupeleka umeme kwenye kiwanda cha Bakhresa kilichoko Mwandege tayari umeme umeshafika.
Mhandisi Mramba amesema, kwa sasa TANESCO inatekeleza miradi mbalimbali ya umeme kote nchini ili kuhakikisha taifa linapata umeme wa uhakika na ulio bora.
Miradi hii ya Dar es Salaam, itakamilika ifikapo Aprili mwakani, alisema Mhandisi Mramba.
Akielezea lengo la ziara hiyo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji alisema, ni kuwawezesha wahariri kuona na kuwafahamisha wananchi jinsi serikali ilivyofanya uwekezaji mkubwa wa katika sekta ya umeme. “Mnaweza kuona kwamba umeme unaopatikana sasahivi ni bora zaidi ukilinganisha na ule uliokuwa ukipatikana miaka michache ya nyuma,” Alisema.
Aidha Mhandisi Mramba alisema miradi ya TANESCO inayotekelezwa hivi sasa nchi nzima ina thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni 5 za kitanzania.

 Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa  Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona, (kulia), akielezea hatua iliyofikiwa hadi sasa ya uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam
Meneja Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere


Kituo cha City Centre.
 Mhandisi Mramba akiwa na wahariri na waandishi wa habari kwenye gari wakati wa ziara hiyo
Mhandisi Mramba, akifafanua jambo wakati wahariri na waandishi walipotembelea kituo cha City Centre.


Tarehe 1 Desemba kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani,mwaka huu 2016 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya dhahabu ya Acacia kupitia mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeadhimisha siku hiyo kwa kuzindua Mashindano ya mpira wa miguu na pete “Mahusiano Cup” ili kuhamasisha jamii inayozunguka mgodi huo kupima virusi vya Ukimwi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara wa Arusha kwenye Kituo cha Mikutano cha Arusha (AICC) Desemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




 Baadhi ya wafanyabiashara wa Arusha wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Ukumbi wa Simba katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha, Desemba  2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments :

Post a Comment