Friday, December 2, 2016

PROF. MUHONGO AKUTANA NA KAMPUNI ZA UTAFITI NA UCHIMBAJI GESI, MAFUTA

muho
Baadhi ya Watendaji wa Kampuni ya Pan- African Energy, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), wakati wa kikao chake na kampuni hiyo inayozalisha gesi ya Songosongo. Wengine ni watendaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Wizara ya Nishati na Madini.
muho-1
Mkurugenzi wa Mkondo wa Chini wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. Wellington Hudson akieleza jambo wakati wakati wa kikao baina ya Waziri wa Nishati na Madini, TPDC na Kampuni ya Pan- African Energy.
muho-2
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dodsal Hyrdocarbons  Pilavullathil Surendran akiwasilisha taarifa kuhusu maendeleo ya shughuli za Kampuni hiyo inayotafiti gesi katika Bonde la Mto Ruvu. Wanaofuatilia ni Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na baadhi ya wawasilishi ya kampuni hiyo.
muho-3
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiongea jambo katika kikao baina yake na kampuni ya Dodsal Hydrocarbons inayotafiti gesi katika Bonde la Mto Ruvu. Wengine ni Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, TPDC na wawakilishi wa kampuni hiyo.
muho-4
Wawakilishi wa Kampuni ya Pan- African Energy inayozalisha gesi ya Songosongo, wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa kikao baina yake na kampuni hiyo. Wengine wanafuatilia ni Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na TPDC.
………………………..
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa nyakati tofauti leo tarehe 2 Desemba, 2016, amekutana na kampuni zinazofanya Utafiti na Uchimbaji wa Gesi na Mafuta nchini za Pan-African Energy and Dodsal Hydrocarbons ikiwa ni utaratibu wa kukutana na kampuni zote zinazofanya shughuli hizo kila baada ya miezi mitatu, kwa lengo la kujadili maendeleo ya utekelezaji wa shughuli za kampuni hizo nchini.
Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons inafanya utafiti wa gesi katika Bonde la Mto Ruvu na kampuni ya Pan- Africa Energy inazalisha gesi ya SongoSongo.

No comments :

Post a Comment