Saturday, December 3, 2016

NMB YATOA MILIONI 10 KUFANIKISHA MAFUNZO KWA WAMILIKI WA MITANDAO YA KIJAMII


 Mwakilishi wa benki ya NMB, Doris Kilale, (Kushoto), akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10, kwa Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika Desemba 2, 2016 kwenye ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
NA MWANDISHI MAALUM


BENKI ya NMB imetoa shilingi Milioni 10, kwa Mtandao wa Wamiliki/Waendesha Mitandao ya Kijamii nchini Tanzania, (TBN), jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2016.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, mwakilishi wa benki hiyo, Doris Kilale alisema, NMB inatambua kuwa TBN ni wadau wakubwa na benki hiyo katika kuhabarisha umma, kwa hivyo benki imeona isaidie ili kufanikisha mkutano huo unaotarajiwa kuanza Jumatatu Desemba 5 jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi alisema, TBN ambayo  ilisajiliwa rasmi na Serikali Aprili mwaka jana, 2015 kwa kushirikiana na wataalam wa masuala ya habari na mitandao ya kijamii imeandaa semina kwa wanahabari hawa wa mitandao ya kijamii hasa 'Bloggers' wapatao 150 kutoka bara na visiwani.
Alisema mkutano huo ambao utaenda sambamba na mafunzo kwa wana TBN yatakayolenga kujenga uwezo juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato).


 Mhandisi wa umeme wa Shirika la Umeme nchuini Tanzania TANESCO, akiwa kazini jijini Dar es Salaam
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza,  Geita, Mara, Simiyu na na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya  Arusha, Manyara, Kilimanjaro  na Tanga na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam (Tazara, Mlimani City, Mandela Road, Ubungo na Kimara, Sinza, Mabibo) kuwa yatakosa Umeme siku ya Jumapili DESEMBA 04, 2016 kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.

SABABU: Kuruhusu Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo Mkubwa ya Kilovolti 400 maarufu kama (Backbone Transmission Line 400 kV) kutoka Iringa hadi Shinyanga.
SABABU: Kuzimwa kwa njia ya Umeme ya Msongo wa Kilovolti 33 Kituo cha Ubungo Dar es Salaam ilikumruhusu Mkandarasi kufanya matengenezo.
Matengenezo hayo yanalenga kuboresha na kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme Nchini.
  
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi alipowasili katika ofisi za ubalozi huo kushiriki sherehe ya madhimisho ya miaka 45 ya muungano.Tanzania na UAE zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan ya kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) hadi Juni, 2015 makampuni 67 ya uwekezaji kutoka UAE yamewekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali wenye thamani ya USD 497.12 Millioni na kuajiri Watanzania 9,044. Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu unaundwa na falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain
                                           
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 45 ya muungano wa falme hizo
Mhe.Waziri Balozi Dkt.Mahiga akivalishwa skafu maalum
Mhe.Waziri Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi
Wageni waalikwa wakifuatilia jambo
Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi akizungumza wakati wa maadhimisho 
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga akitoa hutuba fupi wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdalla Kilima akisalimiana na Mhe. Balozi wakati wa sherehe za maadhimisho
         ------------------------------------------------------------------------------------------------------                                                                  
Tanzania na Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan wa kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) hadi Juni, 2015 Makampuni 67 kutoka UAE yamewekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali kwa mtaji wa thamani ya Dola za Marekani  milioni  497.12  na kuajiri Watanzania zaidi ya 9,044. 
 
Hayo yalibainishwa jana katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya UAE zilizofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alikuwa Mgeni Rasmi. 
Tanzania na UAE  zinatarajiwa kufanya Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) ambao utakuwa chachu ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili hususan ya kiuchumi. 
Akiongea katika hafla hiyo, Mhe. Waziri alilipongeza taifa hilo kwa kuadhimisha siku yake ya Kitaifa ikiwa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo ya kichumi, kijamii na kisiasa. Mhe.  Waziri alisema kuwa siku hiyo ni inatoa fursa pia ya kutathmini mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na UAE.
Kwa upande wake, Balozi wa UAE hapa nchini, Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inayotoa kwa Ubalozi huo ambao unamwezesha kutekeleza majukumu yake kwa wepesi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili. Mhe. Balozi aliahidi kuendeleza ushirikiano huo hususan katika kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. 
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unajumusha falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain huadhimisha siku yake ya Kitaifa tarehe 02 Disemba ya kila mwaka tokea mwaka 1971.



Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allen Kijazi, (katikati), akiwa na   Meneja  Utalii na masoko wa Tanapa, Ibrahimu Musa kushoto na Mkurugenzi wa kampuni ya Zara,  Zainabu  Ansell wakati wa mkutano wao na waandisi wa habari juu ya   maandalizi ya miaka 55 ya uhuru ambayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 9, 2016

 katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi  (wakwanza kushoto), akizungumza na waandishi wa habari. kushoto ni Meneja  Utalii na masoko wa Tanapa, Ibrahimu Musa. Kulia ni Meneja uhusiano wa Tanapa, Paschal Shelutete

 Habari  Picha na Woinde Shizza,Arusha
Aliyekuwa mkuu wa majeshi na mwenyekiti wa bodi ya tanapa jenerali msataafu geogre waitara anatarajiwa kuongoza  msafara wa zoezi la kupanda mlima kilimanjaro desemba 5 hadi kumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 ya  uhuru wa tanzania,
Aidha katika msafara huo wa kupanda mlima kilimanjaro watakuwepo pia wanajeshi kutoka jeshi la wananchi tanzania pamoja na wanahabari ambao watakuwa wanahabarisha jamii kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza na vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa tanapa allan kijazi alisema kuwa mwaka huu tanzania itaadhimisha miaka 55 ya uhuru na hivyo shrikia hilo imeshirikiana na kampuni ya utalii ya zara pamoja na bodi ya utalii (ttb) kuandaa zoezi la kupanda mlima kilimnajro ili kuweza kuhamasisha  watanzania kuvifahamu vifutio vya utalii.
Alisema kuwa zoezi hilo la upandaji mlima litahusissha baadhi ya viongozi mashuhuri  wa jeshi awastaafu akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi ili kuhamasisha watanzania waweze kupanda mlima ambapo tukio hilo litajulikana kama Uhuru Epedition .
Kijazi alifafanua kuwa pamoja na kuadhimisha uhuru wa nchi ,lakini madhumuni mengine ya zoezi hilo ni kuhamasisha utalii na kuhimiza uhifadhi wa mazingira kwani bado watanzania wengi hawana muamko wa kutembelea vufutio vya utalii hivyo kujikuta asilimia kubwa ya watalii ni kutoka nje ya nchi.
"Katika maadhimisho haya tuna malengo ya kuhamasisha watanzania ili wajitokoze kupanda mlima kilimanajaro pamoja na kutembela hifadhi mbali mbaki kwani tunavyo vivutio 16 ambavyo vipo ndani ya tanzania na vinahitaji watanzania wote wanufaike navyo sio tu wageni kutoka nje ya nchi bali hata wa hapa wajue wanazo fursa "aliongeza kijazi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa zara Zainabu Ansell alisema kuwa watanzania wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kihistoria kwani  wengi wao wamekuwa na mawazo potofu ya kufikiria wanaopaswa kupanda mlima na kutembelea hifadhi ni wazungu tu na wageni kutoka nje ya nchi hali inayowafanya watanzania kupoteza haki yao.
Kauli mbiu ya zoezi la kupanda mlima kilimanjaro mwaka huu ni endelea kuweka mazingira safi na salama ya fahari ya afrika.
So fresh and so clean.


 Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafuri akizungumza na wananchi wa Mjini Njombe katika mkutano wake wa Hadhara
Baadhi ya wakazi mjini njombe wakisikiliza mkutano wa mkuu wa wilaya ambapo walipata nafasi ya kutoa maoni yao

WANANCHI halmashauri ya Mji wa Njombe wamemuomba mkuu wa wilaya hiyo Ruth Msafiri kuiamuru halmashauri hiyo kuwagawia wananchi viwanja vilivyopimwa ambapo katika halmashauri hiyo tangu mwaka 2012 hakujapimwa tena viwanja.

Wananchi wanatoa kero zao wakati wa mkutano wa kwanza wa mkuu wa wilaya na wananchi ambapo ni kitu cha kwanza kufanyika wilayani hapo.

Nestori Kigae akitoa kero yake kwa mkuu wa Wilaya ya Njombe alisema kuwa halmashauri hiyo haigawi viwanja kwa vijana na kuwa sasa ni muda mrefu viwanja havijagawiwa na kusasabisha wananchi kukosa maeneo ya kujenga.

Alisema kuwa vijana wapo tayari kujenga makazi yao lakini halmashauri hiyo haipimi viwanja na kuvigawa kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya alitoa nafasi kwa afisa wa Ardhi kujibu masuala yanayo husu ardhi yaliyo ulizwa na wananchi.

Afisa ardhi Taday Kabonge alisema kuwa halmashauri yake ilipima viwanja mwaka 2012 lakini mpaka sasa haijawahi kupima na kuwa kuna viwanja ambavyo mpaka leo bado vipo havijachukuliwa.

Alisema kuwa viwanja vinavyo gawiwa na halmashauri vinauzwa na havigawiwi bure kwa wananchi na kuwa vinatolewa kwa wananchi wote wa halmashauri hiyo.
Katika hotuba ya mkuu wa wilaya ya Njombe ya lisaa limoja kwa wananchi anasema kuwa serikali itahakikisha kero kwa wananchi zinaondoka na kuishi kwa amani bila bughuza.

Hata hivyo aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa inapima viwanja mara kwa mara ili wananchi wake kuendelea kupata maeneo ya kujenga na kuachana na kujenga maeneo ambayo hayahusiki.

Alisema kuwa haiwezekani halmashauri ikapima viwanja kila mara na sio baada ya miaka minne, na kuwa wananchi wanajenga kila wakati.

Hata hivyo diwani wa kata ya Njombe Mjini, Agrey Mtambo alilalamika viwanja vinavyo pimwa na halamshauri kuuzwa bei ghari na kusababisha wananchi kushindwa kuvimiliki.

(Na Furaha Eliabu wa Habari Online na Elimtaa)

NEW MUSIC FROM SPICY (GROUP MEMBER OF 2NITE ENTERTAINMENT)  
Spicy is Mr. Flavour's pianist 
Enjoy the good music


Badhi ya watumishi wa halmashauri ya Mji Makambako wakimsikiliza mkuu wa mkoa alipo fika katika Halmashauri yao kujia shina ma matatizo yao

Mkuu wa mkoa wa njombe Dr Rehema Nchimbi Akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri ya Makambako

SERIKALI mkoani Njombe imetoa ruhusa ya kujenga nyumba mama mjane ambaye amezuiriwa na Jeshi la polisi wilaya ya kipolisi Makambako kutokana na eneo hilo kuwa na mgogoro baina yake na jeshi hilo kwa kuwa majirani wa mama huyo wameruhusiwa kujenga.
Kauli hiyo inatolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa mkanganjiko wa kiwanja cha mjane huyo na kuwapo kwa mvutano mrefu baina ya yake na jeshi la polisi wakati akiwa na mkotano na watumishi wa halmashauri ya mji Makambako ambako yupo katika ziara ya kikazi mkoani humo.
Dr. Nchimbe anasema kuwa mama huyo ajenge kama majirani zake walivyo ruhusiwa kujenga maeneo hayo na wakati watakavyo bomoa kwa majirani wengine basi wabomoe kwa wao wote.
Alisema kuwa haiwezekani mama huyo akazuiliwa kujenga wakati wajirani zake wameruhusiwa kujenga na kuwa kwa kuwa watu hao walijenga kiholele basi hata mama huyo ajenge kiholela.
Hata hivyo mkuu wa mkoa aliingia katika majibizano ya maswali na majibu na afisa mipango walipo kuwa akimuhoji afisa mipango wa halmashauri hiyo Ephahim Mkambo.
Mkuu wa mkoa: kwanini mama huyo haruhusiwi kujenga.
Afisa mipango: mama huyo yupo katika eneo la polisi na haruhusiwi kujenga eneo hilo.
Mkuu wa mkoa: Kwanini majirani zake waliruhusiwa kujenga, eneo hilo.
Afisa mipango: Hawa wengine walijenga kiholela na wenye eneo walishindwa kudhibiti mikapa yao.
Mkuu wa Mkoa: sasa naamuru naye huyu mama ajenge eneo hilo kihilele na watakapo kuwa wakibomoa wabomolewe wote haiwezekani akazuiwa mmoja na wengine wakaruhusiwa.
Mkuu wa mkoa baada ya kutoa ruhusa ya ujenzi kwa mjane huyo alimuonya mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Makambako Paulo Malala kuto saini karatasi za watu wa ardhi kwa kuwa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao kwa usahihi na kufanya kwa ujanja ujanja.
“Nakuonya Mkurugenzi wewe usisaini karatasi za watu wa ardhi watakuingiza matatani hawa ni wajanja wajanja kuwa majini nao,” alisema Dr. Nchimbi.
Katika mkutano wake huo na maafisa na wakuu wa Idara walitoa maoni yao mbalimbali na changamoto zao ambazo zinawakabili kutekeleza majukumu yao na kufanya kazi za wananchi.
Afisa utumishi wa halmashauri hiyo Frederick Kazikuboma alisema kuwa halmashauri hiyo inaupungufu wa magari, na rasisimali watu ambapo kuna idara zinawafanyakazi wacheche.
Hata hivyo Dr. Kyunga Ernest, ni Afisa afya na ustawi wa jamii Halmashauri ya Makambako alisema kuwa pamoja na kuwa na kituo cha afya katika halmashauri hiyo changamoto kubw ani kuto kuwapo kwa chumba cha upasuaji licha ya kuanza ujenzi wake na baadhi ya vifaa kuwanavyo.
Alisema kuwa pamoja na changamoto hiyo halmashuri imekuwa ikipokea fedha za kituo cha afya huku huduma zinazotolewa zikiwa ni za hospitali kutokana na watu wanaofika Hospitalini hapo.
Alisema kuwa baada ya kufunga mfumo wa kielekroniki wa kukusanya mapato wamekuwa wakikusanya zaidi ya milioni 14 lakini watu wanaopata huduma za bure hupokea watu wanao hudumiwa kwa gharama ya Milioni 13 au zaidi ya milioni 14 kitu ambacho hushindwa kujiendesha kwa fedha za ndani.

No comments :

Post a Comment