Wataalam
kutoka Tume ya Mipango wakimsikiliza Meneja anayesimamia Ubora wa
Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi wakati wa ziara ya Tume ya Mipango katika
kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani
Pwani.
Meneja
anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi (aliyevaa koti
jeupe) akiwaonesha maofisa wa ukaguzi wa miradi kutoka Tume ya Mipango
hatua za mwisho za uzalishaji wa juisi katika kiwanda cha uzalishaji wa
vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
Meneja
anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi (mwenye koti
jeupe) akionesha mtambo unaotumika katika uzalishaji katika kiwanda
hicho.
Bidhaa
zikiwa zinapangwa baada ya kupitia hatua mbalimbalikatika katika
kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani
Pwani.
……………………………………………………………………………………………..
Na Adili Mhina, Pwani.
Tume ya Mipango imetembelea
kiwanda cha vinywaji cha Azam kilichoko eneo la Mwandege Mkoani Pwani na
kuonesha kuridhishwa na shughuli za uzalishaji za kiwanda hicho ikiwa
ni moja ya mikakati ya kutekeleza malengo ya Mpango wa Maendeleo wa
Miaka Mitano (2016/17-2020/21) wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya
viwanda.
Timu ya wataalamu wa Ukaguzi wa
Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ilifanya mazungumzo na Meneja
anayesimamia ubora wa bidhaa kiwandani hapo, Bibi Lilian Mwashigadi na
kuelezwa kuwa kiwanda hicho kipo katika hali nzuri na kinaendelea na
shughuli za kuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa katika kukidhi
mahitaji ya soko.
Bibi Mwashigadi alieleza kuwa
kiwanda hicho ambacho kina jumla ya wafanyakazi 800 ambapo kati hao 500
ni ajira za moja kwa moja (direct labor) na 300 ni ajira zisizo za moja
kwa moja (indirect labor) kina mikakati ya kuendelea kupanua soko la
bidhaa zake kimataifa ambapo kwa sasa kinauza bidhaa katika nchi za
Kenya na Rwanda.
Kuhusu upatikanaji wa matunda ya
kutosheleza kiwanda hicho, Meneja huyo alieleza kuwa hakuna changamoto
kwani hapa nchini kuna matunda yenye ubora unaokidhi mahitaji ya viwanda
na kiwanda chake kinategemea malighafi hiyo kutoka kwa wakulima wadogo
wadogo kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Pamoja na hayo, Bibi Mwashigadi
aliongeza kuwa kiwanda chake kimeendelea kununua matunda kwa bei nzuri
ambayo inaendana na bei ya kawaida ya soko lengo likiwa ni kuhakikisha
mkulima anaona faida ya kujishughulisha na kilimo cha matunda.
Hata hivyo alitoa wito kwa Tume
ya Mipango kuangalia namna ya kutengeneza sera itakayosaida kumnufaisha
zaidi mkulima mdogo kwani kwa sasa madalali ndio wanaochukua matunda
toka kwa wakulima na kupeleka kiwandani na mkulima anaishia kupata faida
kidogo huku madalali wakiendelea kunufaika.
No comments :
Post a Comment