MBUNGE
wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amepongeza jitihada
kubwa zinazofanywa na wataaluma wa Halmashauri ya Chalinze katika
kuboresha mradi wa maji wa Wami kwa ajili ya wananchi wa Chalinze .
Akizungumza
baada ya kutembelea mradi huo jana mbunge Kikwete alisema kuwa
mradi huo ambao ulianzishwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo
Dkt Jakaya Kikwete ambae ni rais mstaafu wa awamu ya nne ni mmoja
kati ya miradi bora iliyoleta ukombozi mkubwa wa upatikanaji wa
maji safi na salama kwa wananchi wa mji wa Chalinze .
Hivyo
alisema kusudi la kufanya ziara katika eneo la mradi huo mto Wami
ni kuona shughuli mbali mbali zinazofanywa na wataalam kwa ajili
ya kuendelea kuboresha mradi huo ili kuwawezesha wananchi wake
kupata huduma ya uhakika ya maji safi na salama wakati wote .
”
Mradi huu ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa jimbo la Chalinze na
niwapongeze sana wataalam wa Halmaszhauri kwa kazi nzuri
wanayoifanya ya uboreshaji wa maradi huu” alisema mbunge Kikwete
Alisema
kuwa amefurahishwa na jitihada zinazoendelea kufanywa na wataalam
wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wananchi wanapata maji na kazi
kubwa yake mbunge akiwa ni mwakilishi wa wananchi ni kuendelea
kuisimamia serikali kwa kuwawakilisha wananchi wake vema bungeni.
Huku akiwataka wananchi kuendelea kutunza miundo mbinu ya maji ili kuwezesha mradi huo kuendelea kuwa msaada kwao .
No comments :
Post a Comment