Madereva wa bajaj na Pikipiki (bodaboda) wakimsikiliza kwa makini mrakibu Msaidizi wa Polisi Kitengo cha Elimu Makao Makuu ya Kikiosi cha Usalama Barabarani nchini,ASP Mossi Ndozero (Kulia) wakati wa mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva wa bajaji na pikipiki (bodaboda) yaliyofanyika eneo la Ubungo maji jijini
Dar es Salaam chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group ili kuwafanya
madereva hao waweze kuendesha kwa usalama katika msimu huu wa sikukuu za
mwisho wa mwaka
Madereva wa bajaj na Pikipiki (bodaboda) wakimsikiliza kwa makini mrakibu Msaidizi wa Polisi Kitengo cha Elimu Makao Makuu ya Kikiosi cha Usalama Barabarani nchini,ASP Mossi Ndozero (Kulia) wakati wa mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva wa bajaji na pikipiki (bodaboda) yaliyofanyika eneo la Ubungo maji jijini
Dar es Salaam chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group ili kuwafanya
madereva hao waweze kuendesha kwa usalama katika msimu huu wa sikukuu za
mwisho wa mwaka
Wafanyakazi wa TBL Group kitengo cha Uhusiano, Irene Mutiganzi (kushoto ) na Amanda Walter wakimsikiliza kwa makini Mrakibu Msaidizi wa Polisi Kitengo cha Elimu Makao Makuu ya Kikiosi cha Usalama Barabarani nchini,ASP Mossi Ndozero (Kulia) wakati wa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa bajaj na pikipiki (bodaboda) eneo la Ubungo maji jijini Dar es Salaam yaliyofanyika kwa udhamini wa TBL Group.
Madereva wa Bajaj na pikipiki maarufu kwa jina laBodaboda wanaofanya kazi katika sehemu ya Ubungo Maji jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Mwalimu wa mafunzo ya usalama barabarani Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani S/SGT Dina Mosi wakati alipokuwa akiendesha mafunzo ya Usalama barabarani .Mafunzo hayo yalifanyika kwa udhamini wa kampuni ya TBL Group.
Mwalimu
wa Mafunzo ya usalama wa barabarani wa jeshi la polisi kitengo cha
usalama barabarani ,S/SGT Dina Mosi,(kulia) akimfafanulia jambo mmoja wa
madereva wa bodaboda Juma Hamisi , wakati wa mafunzo hayo.
Abiria Khalfan Idd akisaidiwa kuvishwa kofia ngumu na Mwalimu
wa Mafunzo ya usalama wa barabarani wa jeshi la polisi kitengo cha
usalama barabarani ,S/SGT Dina Mosi wakati alipokuwa akitoa elimu ya
mafunzo kwa vitendo kwa madreva wa bodaboda eneo la Ubungo Maji jijini Dar es Salaam,mafunzo hayo yalidhaminiwa na kampuni ya TBL Group
……………………………………………………………
Katika
mkakati wake wa kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza ajali za
barabarani nchini,kampuni ya TBL Group imedhamini mafunzo ya Usalama
Barabarani kwa waendesha Bajaji na pikipiki wanaofanyia kazi zao katika
kituo cha Ubungo Maji .
Madereva
pia walipata fursa ya kupata mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu ambayo
yanaelekeza kutumia vinywaji vyenye kilevi kistaarabu na kuhakikisha
utumiaji wake hauleti athari yoyote ambapo pia madereva walikumbushwa
kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wametumia vinywaji vyenye kilevi.
Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL Group,Irene Mutiganzi ,alisema kampuni imedhamini mafunzo hayo yaliyotolewa na Maofisa kutoka Jeshi la Polisi,Kitengo cha Usalama Barabarani ni mwendelezo wa kampuni hiyo kuendesha kampeni za usalama barabarani.
“Tukiwa
kampuni inayotengeneza vinywaji vya aina mbalimbali vyenye kilevi
tunalo jukumu pia kuunga mkono jitihada za serikali kupunguza matukio ya
ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo vya watu wengi
na hasara kubwa.Hivyo tunatoa wito kwa madereva wote hususani wa vyombo
vya moto katika msimu huu wa sikukuu kuwa makini kuzingatia sheria za
usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazotokana na uzembe wa
kutozingatia sheria na kanuni za usalama barabarani”.Alisema Mutiganzi.
Mutiganzi alisema TBL Group itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na wadau wengine wa masuala ya usalama barabarani ili kutokomeza matukio ya ajali nchini.
Alisema
hivi sasa kampuni inaendesha mafunzo ya unywaji wa kistaarabu kwa
makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo madereva na elimu hiyo itaendelea
kutolewa kwa nguvu zote katika kipindi cha mwaka ujao ili iwafikie
watanzania wengi nakubadilisha jamii kuwa na utamaduni wa utumiaji wa
vinywaji vyenye kilevi bila kusababisha athari zozote kutokana na
utumiaji huo.
“kampuni
pia imekuja na mkakati wa kuhakikisha elimu ya usalama barabarani
inawafikia wanafunzi wa shule za msingi ili wakue wakiwa na uelewa wa
umuhimu wa kuzingatia kanuni za usalama barabarani ambapo kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani imeanza
kuendesha imekuwa mafunzo kwa wanafunzi wa shule za msingi katika mikoa mbalimbali nchini”alisema
No comments :
Post a Comment