Friday, December 23, 2016

UHURU MUSIC LIMITED TANZANIA YAWAPA MKONO WA SIKUKUU WATOTO YATIMA


 shangwe-1
Baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Amani Foundation For Orphanate kilichopo Mji Mwema,Kigamboni jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo ya kupokea msaada toka kampuni ya Uhuru Music Limited Tanzania.
mnc
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Music Limited Tanzania akitoa neno mbele ya waandishi wa habari kabla ya kukabidhi vifaa vya msaada kwenye kituo cha kulelea watoto Yatima cha Amani Foundation For Orphanate kilichopo Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es salaam.
shangwe-2
Bi.Zuena Abdallah Mlezi wa kituo cha kulelea watoto Yatima kilichopo Mji Mwema Kigamboni akitoa shukrani za dhati kwa kampuni ya Uhuru Music Limited Tanzania kwa kutoa msaada katika kituo chake.
sdf
Kijana Juma Nasoro anayelelewa katika kituo cha Amani Foundation For Orphanate ambaye anasoma kidato cha pili akiwa anasoma Risala mbele ya mgeni rasmi hayupo pichani.
ass
Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mhe.Faustine Ndunyalile akizungumza na waandishi wa habari akiwa ndiye mgeni rasmi katika kituo cha Watoto Yatima cha Amani Foundation For Orphanate kilichopo Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es salaam akishuhudia msaada uliotolewa na Kampuni ya Uhuru Music Limited Tanzania.
shangwe-3
Baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru Music Tanzania na watoto wakishusha mizingo iliyotolewa katika kituo cha Amani Foundation For Orphanate kilichopo Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es salaam.
shangwe-4
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Amani Foundation For Orphanate kilichopo Mji Mwema Kigamboni, wakishuhudia msaada uliotolewa na Uhuru Music Limited Tanzania.
asd
Watoto wakisoma dua ya kufunga kikao cha utoaji wa msaada katika kituo cha kulelea watoto Yatima kilichopo Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es salaam mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la kigamboni hayupo pichani.
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.

Kampuni ya Uhuru Music Limited Tananzaia imefanya ziara ya kijamii na kutoa msaada kwenye kituo cha kulelea watoto Yatima cha Amani Foundation For Orphanate kilichopo mji Mwema Kigamboni,katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka wa msimu wa Sikuku za Krismasi na Mwaka Mpya.
Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Music Limited Tanzania,Maneno Sanga,akiambatana na wafanyakazi na waandishi wa habari ambapo tukio hilo la kukabidhi zawadi hizo zenye thamani ya shilingi milioni tatu na kupokelewa na Mlezi wa kituo hicho Bi.Zuena Abdallah.
“Ni kweli kampuni yetu imeamua kutoa msaada katika kituo hiki kutokana na kukuguswa na tukio ambalo lilitokea kwa watu kuja kuvamia na kuiba vitu mbalimbali hivyo kama sisi ni watanzania tumeamua kuleta vifaa mbalimbali ambavyo vitawasaidia katika msimu wa sikuku pamoja na unifomu za shule”alisema Sanga
Kwa upande wa Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mhe.Faustine Ndunyalile,ametoa shukrani kwa kampuni hiyo kwa kuamua kujitolea na kuweza kuwasaidia watoto ambao wapo katika kituo hiki hivyo tunakarinisha makampuni mengine yaje kujitolea na kuiga mfano wa kampuni ya Uhuru Music Limited Tanzania
“Kiukweli binafsi nimeguswa na jambo hilo kwani nilikuwa na mialiko minne lakini nimeamua kuiacha na kuja kuungana na kwenye utoaji huu wa misaada katika kituo hiki na mpango wa Serikali ni kuzitaka taasisi zote zinaz0jihusisha na kulea watoto ni lazima vijisajili ili jimbo lijue lina vituo vingapi ili iwe rahisi kuweza kuwasaidia mahitaji yao”alisema Ndunyalile
Aidha Mhe.Ndunyalile amesikitishwa na tukio ambalo lilitokea katika kituo hicho cha baadhi ya watu kwenda kuvamia na kupora vitu mbalimbali vya watoto hao na anatoa tahadhari kwa wahusika kwani jeshi la polisi limeanza na kuwafatilia wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na ameahidi kutoa ushirikiano mpaka wahusika wakamatwe
Naye Mlezi wa kituo hicho,Zuena Abdallah ametoa shukrani zake kwa Kampuni ya Uhuru Music Limited Tanzania ambayo inajuhusisha na kusambaza kazi za music na kusema kuwa kupokea msaada huu ni faraja kwake na kwa kituo hicho kwani wataweza kukimu mahitaji yao na kuwaomba wadau wengine kuwa na moyo wa kujitolea.
“Tunashuku sana Uhuru Music Tanzania kwa kuguswa na tukio hilo lililotea kwa baadhi ya watu kuja kuiba vitu vya watoto ambao tunawalea hivyo tunatoa pongezi za dhati kwa kutuletea msaada huu na utatusaidia mno kwani kuna baadhi ya sare za shule ziliweza kuibia na watu hao”alisema Zuena
Katika ziara hiyo Kampuni ya Uhuru Music Limited Tanzania imeweza kutoa msaada wa vyakula,Mkaa,Vinywaji,Sare za shule kwa watoto wanaosoma katika shule mbalimbali kutoka katika kituo hicho chenye jumla ya watoto 35 wanaolelewa hapo,Sabuni,Madaftari pamoja na vitabu mbalimbali

No comments :

Post a Comment