Na Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali imesema kuwa haipo teyari
kuwavumilia watendaji wasiona uchungu na nchi yao na kutumia madaraka
yao vibaya na kupelekea serikali kuingia hasara kubwa na kushindwa
kuwahudumia wananchi.
Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya
ya Arusha Gabriel Daqarro wakati akifunga mkutano wa mwaka wa kongamano
la saba wa bodi ya manunuzi na ugavi uliofanyika kwa siku mbili jijini
Arusha.
Alisema kuwa kumekuwawepo na
baadhi ya maofisa wa serikali wanaofanya ubadhirifu katika sekta hiyo ya
manunuzi na kuwa wao wamekuwa na ubinafsi mkubwa unaopelekea serikali
kuingia hasara kubwa hivyo hawapo teyari kuwavumilia watu wa aina hiyo.
Daqarro aliekuwa akiongea kwa
niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha alisema kuwa watu wa manunuzi ni muhimu
kwani wamekuwa wakifanyakazi nzuri hivyo endapo wakisimamia maadili
vizuri na kuwaka mbele uzalendo na uchungu kwa taifa lao watafanikiwa
katika majukumu yao itasaidia kama taifa kupata maendeleo.
“Nawasihi Ndugu zangu kuwa na
uchungu na uzalendo kwa taifa lenu kwa kuhakikisha maendeleo
yanapatikana kupitia utaalamu wenu kwani nchi yetu imekuwa ikipata
hasara kwa asilimia 50% ya manunuzi kama ripoti ya mkaguzi mkuu wa
serikali inavyoainisha”alisisitiza Daqarro
Kwa Upande wake Kaimu mkurugenzi
mkuu wa bodi ya manunuzi na ugavi Godfrey Mbayi alisisitiza kuwepo
utawala bora katika mchakato wa manunuzi ya umma ilikuondoa hali ya
udanganyifu inayotokea mara kwa mara.
Alisema kuwa masuala mbali mbali
katika manunuzi ya umma yanahitaji wigo mpana na kuweka mbele uzalendo
utakaosaidia kuliondoa taifa eneo moja kwenda jingine na sisi wataalama
tunahitajika kulivalia njga suala hili.
Nae mwenyekiti wa bodi ya manunuzi
na ugavi sister Helen Bandiko alitoa Rai kwa wale wote wanaofanya
manunuzi ya serikali kuwa na sifa zinazostahili ili kulida upotevu wa
fedha za serikali katika manunuzi ya umma ikiwemo fedha za miradi ya
serikali.
No comments :
Post a Comment