Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa
Jamii Bi Beatrice Fungamo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto akikabidhi kwa niaba ya Rais zawadi ya Sikukuu
kwa Msimamizi wa Makao ya Taifa ya watoto yatima Kurasini leo jijini
Dare es Salaam.
:Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa
Jamii Bi Beatrice Fungamo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto akikabidhi kwa niaba ya Rais zawadi ya Sikukuu
kwa Msimamizi wa Kituo cha watoto Msimbazi arc diocese cha Dar es
Salaam leo jijini Dare es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa
Jamii Bi Beatrice Fungamo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto akikabidhi kwa niaba ya Rais zawadi ya Sikukuu
kwa ,Msimamizi wa Kituo cha Watoto cha Dar Al Arqum International
Islamic Relief Organisation leo jijini Dare es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa
Jamii Bi Beatrice Fungamo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto akikabidhi kwa niaba ya Rais zawadi ya Sikukuu
kwa Msimamizi wa Kituo cha Watoto Mburahati leo jijini Dare es Salaam.
…………………………………………………………………………
Na Anthony Ishengoma
Rais John Pombe Magufuli ametoa
zawadi yenye thamani ya shilingi 8,475,00 kwa watu walio katika makundi
maalum wakiwemo watoto walio katika mazingira hatarishi na wazee
wanaohudumiwa katika makazi ili waweze kusherehekea sikuu ya krismass ya
mwaka 2016 na mwaka mpya 2017.
Akikadidhi zawadi hizi kwa niaba
yake Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi Beatrice Fungamo kutoka
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto amesema ni
utaratibu wa kawaida kwa viongozi Wakuu wa Nchi yetu kuwapatia makundi
haya maalum zawadi ya Siku Kuu Krismass ya mwaka huu na mwaka mpya.
Zawadi zilizotolewa kwa thamani
hiyo ya fedha ni vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia
ili kuwawezesha kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu
wengine.
Zawadi hizi zimetolewa kwa vituo 7
katika Mkoa wa Dar es Salaam, vituo viwili kutoka Zanzibar na Makazi ya
Wazee katika mikoa ya Tabora, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Tanga,
Ruvuma, Shinyanga, Singida, Mwanza, Lindi, Mtwara, Kagera, Mara na
Morogoro.
Bi. Beatrice Fungamo amevitaja
vituo hivyo kutoka mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni Makao ya Taifa ya
Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto Msimbazi, Kituo cha
Watoto Dar Al Arqum, Makao ya Watoto Mburahati, Makao ya Watoto Kijiji
cha Furaha, Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam, Upanga na Makazi ya Wazee
Wasiojiweza na wenye Ulemavu Nunge, Kigamboni.
Zanzibar ni Kituo cha Watoto
Mabaoni – Chakechake, Pemba na Makazi ya wazee wasiojiweza Sebleni –
Unguja ikiwemo makambi ya wazee kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara yenye
makambi ya Wazee.
No comments :
Post a Comment