MBGUNGE wa Kibaha Vijijini Hamoud
Jumaa,akizungumza jambo na mke wa Selemani Mgoto,baada ya kwenda
kumjulia hali Mgoto,ambae anaomba msaada wa kupelekwa nchini India
kupatiwa matibabu ya macho baada ya kupofuka kutokana na kumeza dawa
zilizokwisha muda wake aina ya fansidar.(picha na Mwamvua Mwinyi)
MKAZI wa Mlandizi,Kibaha
Vijijini mkoani Pwani, Selemani Mgoto ,wa kwanza kulia kwenye
kochi,akizungumza baada ya kwenda kutembelewa na mbunge wa jimbo la
Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa (picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKAZI wa Mlandizi,Kibaha Vijijini
mkoani Pwani, Selemani Mgoto (42)ameiomba serikali kupitia wizara ya
afya ,kumsaidia kumpelekea nchini India kwenye matibabu ya macho ambayo
ameyapoteza baada ya kutumia vidonge ya malaria (fansidar).
Amesema kinachomuumiza ni
kuthibitishiwa na madaktari bingwa wa hospitali ya CCBRT na Muhimbili
kuwa endapo ataenda India atapona lakini kinachomkwamisha ni sh.mil.18
kwa ajili ya safari hiyo.
Aidha kufuatia tukio hilo,mbunge
wa jimbo la Kibaha Vijijini,Hamoud Jumaa amefanya jitihada za kuzungumza
na mh January Makamba ambae amechangia sh.500,000 na kampuni make one
ambayo imechangia mil.mbili.
Akizungumzia wakati alipokwenda
kutembelewa na mbunge huyo ,nyumbani kwake kitongoji cha Janga,alisema
tangu yamkute maswaibu hayo ni miaka minne sasa.
Mgoto alimuomba msaada rais John Magufuli kumtupia macho kwani nae ni kati ya wananchi wanyonge wasio na uwezo.
Hata hivyo alimwangukia pia waziri
wa afya Ummy Mwalimu na naibu wake kuangalia uwezekano wa kumpeleka
kwenye matibabu ya macho nchini India baada ya kuthibitishiwa kwamba
anaweza kupona kama atapata matibabu zaidi.
Mgoto alisema hadi sasa
ameshasaidiwa kiasi cha sh.mil.5 pekee hivyo bado kiasi kikubwa cha
fedha ambacho kinahitajika kuondoka kwenda kwenye matibabu.
“Kweli kabla hujafa
hujaumbika,namshukuru mungu kwa hili,nateseka,muda unazidi kwenda
nahofia kupoteza macho yangu kabisa,watanzania wenzangu,mawaziri,wabunge
na mh.rais wangu naomba mnisaidie nikaangalie nguvu za mungu”aliongea
kwa uchungu.
Alieleza kuwa mnamo agosti 2012
alikuwa anaumwa na kwenda kupimwa malaria katika kituo cha afya cha
Mlandizi ambapo aligundulika kuwa na wadudu 9 wa ugonjwa wa malaria.
Mgoto alisema aliandikiwa dawa
aina ya fansidar na kuamua kwenda kuzinunua katika moja ya duka la dawa
na baada ya siku mbili kuzimeza hali ilibadilika kutokana na sumu kali
iliyokuwepo mwilini mwake .
“Nilianza kuharibika kucha zangu
za miguu na mikono,nilianza kutoka nywele zangu za kichwani,na
kukimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Pwani,(Tumbi) kupata
matibabu,na kugundulika dawa nilizomeza zilikuwa zimeisha muda
wake”aliongeza.
Mgoto alisema mara ya mwisho alikwenda kuwaona madaktari bingwa
wa hospitari ya CCBRT ya jijini Dar es salaam na muhimbili ambao
walimwambia hawezi kupona Tanzania hadi aende nchini India .
Akizungumzia kuhusu maisha yake
,alieleza anashindwa kulipa kodi ya nyumba kwani amepanga anadaiwa kodi
sh.300,000 huku kipato kikididimia kutokana na kutokuwa na uwezo tena wa
kufanya kazi.
Nae mkewe mama Baraka,alisema maisha yao yamekuwa magumu ,kufuatia tangu mumewe apate matatizo hayo yeye alikuwa mjamzito.
Alisema kwasasa anajishughulisha na masuala ya salun ya kike na kumhudumia mumewe na watoto wao watatu .
Walimshukuru mbunge wao, kwenda
kuwafariji na kuonyesha jitihada za kutaka kuwasaidia ili kutekeleza
maombi ya wataalamu wa kiafya.
Kwa upande wake mbunge wa Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa alisema hali ya mgoto hasa kimaisha sio nzuri.
Kwa upande wake mbunge wa Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa alisema hali ya mgoto hasa kimaisha sio nzuri.
Alisema inasikitisha
kilichomuumiza ni dawa zinazoingizwa hapa nchini na wauzaji wengine
kutofuata masharti ya kitaalamu hatimae kuwaingiza kwenye athari wasio
na hatia.
Jumaa alisema ameshachukua hatua
mbalimbali za kuongea na wadau ambapo January Makamba amechangia laki
tano na mkurugenzi wa kampuni ya make one amechangia mil.mbili.
Alieleza anaendelea na jitihada
nyingine za kwenda wizara ya afya na kuzungumza na wabunge wenzake ili
kuangalia namna ya kumsaidia.
Jumaa aliwaomba wadau wa Kibaha
,mkoa wa Pwani na nje ya mkoa wajitokeze kumsaidia Mgoto aweze kwenda
kutibiwa kwani kutoa ni moyo na sio utajiri.
Mtu yoyote anaehitaji kumsaidia mchango wake kwa hali na mali Seleman Mgoto ,atumie namba ya tigo pesa –0655-413939 au M-PESA 0754-413939 na akaunti namba NMB -80110000915.
No comments :
Post a Comment