Friday, December 23, 2016

MKUU WA WILAYA YA ILALA SOPHIA MJEMA NA DSTV WANOGESHA KAPU LA SIKUKUU KWA VING’AMUZI VYA BURE


sewe
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa na mmoja ya mshindi wa kapu la sikukuu na kulia ni msanii wa vichekesho Tanzania Mboto
wafanyakazi wa kituo cha redio cha EFM na kampuni ya MULTICHOICE Tanzania muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi

mgeni rasmi bi Sophia Mjema (katikati) akizungumza jambo kabla ya kukabidhi zawadi kwa mmoja wa washindi

Mshindi wa kapu la sikukuu akikabidhiwa zawdi zake

washindi wakipokea zawadi za kapu la sikukuu kutoka kwa kampuni ya MULTICHOICE

mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi zawadi za kapu la sikukuu bi Sophia Mjema akitoa hotuba fupi kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi

Meneja masoko wa kampuni ya MULTICHOICE tanzania Alpha Mria akiwa na wafanyakazi wengine wa kapuni hiyo muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi za ving’amuzi kwa washindi wa shindano la kapu la sikukuu.PICHA ZOTE NA IMANI KELVIN MBAGA
Na.Alex Mathias,Dar es salaam

Kampuni ya Multichoice Tanzania leo imeendelea kurejesha  kile inachokipata kwa jamii baada ya kukabidhi zawadi za ving’amuzi vipatavyo 24 vikiwa na vifurushi vya mwezi mzima, kwa washindi wa shindano lijulikanalo kama kapu la sikukuu lililoendeshwa na kituo cha redio cha EFM kilichopo jijini Dar es salaam.
Katika hafla iliyofanyika leo jijini, jumla ya washindi 24 kutoka maeneo mbalimbali ambao walitakiwa kujibu maswali yaliyoulizwa katika vipindi tofauti vya redio hiyo walikabidhiwa zawadi zao vikiwemo ving’amuzi vya DStv kutoka kampuni ya Multichoice Tanzania mbele ya mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya Ilala Sofia Mjema
Akikabidhi zawadi hizo mkuu huyo wa wilaya alisema ni jambo la kufurahisha kuona namna ambavyo EFM na kampuni ya Mulitichoice kwa pamoja wameamua kuwaangalia wananchi na kuwapa fursa ya kufurahi hasa katika nyakati za msimu wa sikukuu mwishoni mwa mwaka.
“Ni jambo la kufurahisha sana kuona namna ambavyo wananchi wana pata zawadi hizi katika msimu huu wa sikukuu na hilki ni jambo zuri na la kutia moyo sana na nawaomba EFM na Multichoice waendelee kuwaangalia wananchi mara kwa mara” Alisema bi, Mjema
Awali akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Masoko wa kampuni ya Multichoice Tanzania, Alpha Mria alisema kuwa wamamua kuwazawadia washindi hao ving’amuzi vya DStv na vifurushi vya mwezi mzima ili kuwafanya washerehekee sikukuu ya Krisimasi na Mwaka mpya kwa furaha zaidi na familia zao
Hivi karibuni kampuni hiyo ilishusha bei za vifurushi vyao kwa asilimia 16 huku kifurushi maarufu cha DStv bomba chenye zaidi ya chaneli 70 kikipunguzwa bei pia ili kuwezesha watumiaji wengi zaidi kufurahia matangazo yanayorushwa kupitia king’amuzi hicho.
Katika kunogesha hafla hiyo waigizaji maarufu hapa nchini “MBOTO” na IRENE PAUL walikuwa miongoni mwa wageni waliokabidhi zawadi kwa washindi wa kapu la sikukuu

No comments :

Post a Comment