Friday, December 23, 2016

Mkuu wa Wilaya Azomewa mbele ya Waziri. mnyeti

mnyeti
Na Mahmoud Ahmad Arusha
MKUU wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti Amepata aibu baada ya kuzomewa mbele ya Waziri wa Ardhi maendeleo ya makazi William Lukuvi katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Arusha .
Mnyeti alizomewa wakati akitoka katika kikao cha waziri kupewa taarifa za matatizo ya Ardhi mkoa wa Arusha.

Amezomewa Mnyeti kufuatia kitendo chake cha kuagiza kuwekwa rumande mwandishi wa ITV Halfani Liundi.
Agizo hilo ambalo mpaka sasa lina ukakasi wa u halali wake kwa kua Lihundi siyo makazi wa Arumeru anapotawala Mnyeti limelaaniwa na wadau wote wa habari.
Ziara ya Lukuvi.
Waziri Lukuvi amelazimika kufika Arusha kushughulikia  kukithiri kwa migogoro ya Ardhi hususani Wilaya ya Arumeru na viongozi wa Wilaya hiyo Kushindwa kuyapatia ufumbuzi.
Hivi karibuni Waziri mkuu akiwa katika ziara mkoani Arusha akiwa Wilaya ya Arumeru alipokelewa na mabango ya wananchi wakilalamikia migogoro ya Ardhi iliyokithiri Wilayani humo.
Katika majumuisho ya ziara yake hiyo Waziri mkuu kasimu Majaliwa akaeleza kuwa ukiona kiongozi wa juu anapokelewa na mabango katika Wilaya yenye viongozi ujue kiongozi aliyopo hapo hatoshi.
Mwandishi Lihundi hadi  Jana mchana alikuwa akihojiwa kituo cha polisi User River ili waweze kupata fursa ya kupata dhamana.
Aidha kulikuwa na utata juu ya tuhuma zinazomkabili ambapo Mara baada ya kufika mwanasheria anayemtetea katika kadhia hiyo Edwin Silayo kutaka kuongea na Mteja wake mkuu wa upelelezi Wilaya alimzuia akidai Lihundi hana kesi Bali amewekwa ndani kwa agizo la Dc.
Hali hiyo ilizidi kuonyesha mkanganyiko kwa waandishi wa habari waliokuwepo kituoni hapo na kulazimika kujiandaa vyema kushughulikia tatizo hilo.

No comments :

Post a Comment