Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akitoa maelekezo kwa Mkuu wa
Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee (wa kwanza kulia) wakati wa ziara
yake katika shule ya Masasi yenye kuhudumia wenye ulemavu Mkoani Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) akiwa katika
ziara ya kuangalia maeneo ya shule ya Masasi inayohudumia wanafunzi wa
mahitaji maalum wakati wa ziara yake mkoani Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akikagua moja ya bweni la
wanafunzi wenye mahitaji maalum la Shule ya Masasi Mkoani Mtwara
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akionesha namna ya kutumia
Kurunzi ya mwanga wa jua kwa baadhi ya wazee wenye ukoma wanaoishi
katika Kambi ya Mkaseka Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara na kuwapatia
wazee hao kurunzi 20 kwa kila nyumba.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Halima Dendego
akimweleza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Dkt. Abdallah Possi historia fupi ya mkoa huo wakati wa ziara yake
mkoani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa sita kutoka kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Masasi mkoani Mtwara mara bada ya kumaliza ziara yake mkoani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya
waandishi wa habari katika ziara yake alipotembelea Shule na Makazi ya
wazee Wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
……………..
Na. Mwandishi Wetu
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi
ameitaka jamii kuzingatia haki na usawa kwa watu wenye
ulemavu nakuondokana na imani potofu za kuona watu wenye ulemavu hawana
uwezo wa kufanya shughuli za maendeleo.
Mhe. Possi ameyasema hayo kwa nyakati
tofauti alipotembelea Vituo na Shule zinazohudumia watu wenye mahitaji
maalum vya Nandanga, Rasi Bula, Shule ya msingi Nyangao mkoani Lindi
pamoja na makazi ya wenye ulemavu na Ukoma ya Mkaseka, Chuo cha wenye
Ulemavu cha Mtapika, shule ya Lulindi na Masasi mkoani Mtwara.
Katika ziara hiyo Mhe.Possi
alisisitiza jamii zibadili mitazamo hasi juu ya masuala ya haki na usawa
kwa watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha katika shughuli zote na
kuwapa vipaumbele vya fursa sawa.
“Ninasisitiza jamii ibadili mitazamo
dhaifu juu ya haki na usawa wa kuwashirikisha watu wenye ulemavu kwani
wana uwezo wa uzalishaji endapo tutawapa fursa sawa kama ilivyokuwa kwa
wakina mama walipoachwa nyuma muda mrefu ila jamii imeona fursa ndani
yao, iwe hivyo hivyo kwa watu wenye ulemavu” alisema.
Aidha Waziri Possi ameweka mkazo juu ya kuwahusisha na kutokuwaona kuwa ni kundi la kuachwa nyuma na kama tegemezi.
“sheria zipo wazi kabisa
zinazotuelekeza juu ya haki na usawa kwa watu wenye ulemavu kwa mujibu
wa matakwa ya Sheria ya watu wenye Ulemavu namba 9 ya mwaka 2010
inayoeleza haki za watu wenye Ulemavu kuwahudumia kwa haki na usawa na
kuboresha maeneo muhimu ikiwemo fursa za kielimu, ajira, kiuchumi na
kijamii,” alieleza.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya
Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti alikiri kuyapokea yote aliyoeleza
Mhe.Waziri katika ziara yake na kuipongeza Serikali kwa juhudi za
kuisaidia jamii bila kujali hali zao na tofauti zao.
“Ninaipongeza Serikali ya Awamu ya
Tano inayowajali wanyonge na kujali haki zao pamoja na mhe. Waziri kwa
kuona umuhimu wa kututembelea wana Ruangwa na tunaahidi kukuweka katika
kumbukumbu zetu maana umewagusa wakazi wa Mtwara hususani wazee na watu
wenye ulemavu.”Alisisitiza Mkuu wa Wilaya hiyo.
Nae Afisa Mfawidhi kituo cha Kulelea
wazee wenye ukoma cha Mkaseka Bw. Cleophace Nguli aliiomba Serikali
kuendelea kuwakumbuka watu wenye ulemavu ikiwa ni watu waliosahaurika na
kuendelea kupongeza hatua zilizopo kwa sasa.
No comments :
Post a Comment