Mkuu
wa kikosi cha Usalama barabarani SSP Nuru Suleiman akiwa katika kituo
cha kikuu cha mabasi yaendayo mkoania na nchi jirani ,mkoani Arusha
tayari kwa kutoa elimu kwa abiria na madereva leo 19Desemba 2016.Picha
pamoja na habari
na Vero Ignatus Blog.
na Vero Ignatus Blog.
Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Usalama barabarani mkoa wa Arusha bi.Stella Ruraguza akizungumza na mwenyekiti wa wakata tiketi stendi kuu ya mabasi yaendayo mkoani na nchi jirani Babuu Jumanne .Picha pamoja na habari na Vero Ignatus Blog |
|
||
Wa kwanza kushoto ni koplo Athilio Choga aliyepo katikati ni Vehicle Inspector Koplo Songoi na wa kwanza kulia ni PC Rajabu |
|
Na.Vero Ignatus- Arusha.
Mabalozi
wa usalama wa barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi
cha usalama barabarani wamefanya zowezi la kutoa elimu kwa abiria pamoja
na madereva huku jeshi la polisi wakiwapima madereva ulevi na kukagua
ubora wa magari hayo kabla ya kuanza safari kuelekea mikoani
Zowezi hilo limeongozwa na mkuu
wa kikosi cha usalama barabarani SSP Nuru Suleiman na katika stendi kuu
ya mabasi yaendendayo mikoani na nchini jirani Jijini Arusha huku
zowezi hilo likiwa na lengo la kuelimisha,kukemea na kuripoti mwenendo
mzima unaokiuka sheria za usalama barabarani.
Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani
Nuru Suleiman amesema kuwa kampeni hiyo inamafanikio makubwa tangia
ianze kwenye wiki ya nenda kwa usalama kwani tangia mwanzoni mwa mwaka
2016 hakuna ajali ya basi iliyotokea na kuleta madhara kwa jamii kwa
ujumla.
“Kwakweli tunamshukuru sana Mungu kwani tangia mwaka huu uanze hatujapata ajali
ya basi inaonyesha madereva wamepata elimu na wanaitendea kazi na tunawaomba waendelee kuwa makini ili ajali ikiwezekana zisitokee kabisa “alisisitiza kamanda Nuru.
ya basi inaonyesha madereva wamepata elimu na wanaitendea kazi na tunawaomba waendelee kuwa makini ili ajali ikiwezekana zisitokee kabisa “alisisitiza kamanda Nuru.
Aidha amesema kuwa wamekuwa wakiwapima madereva ulevi na madereva ambao
wanakiuka sheria za usalama barabarani na pale wanapogundulika na
makosa wapo wengine wanalipishwa faini na wengine wanapelekwa
mahakamanikufutiwa leseni na kuzuiliwa kuendesha chombo cha moto
kabisa.
wanakiuka sheria za usalama barabarani na pale wanapogundulika na
makosa wapo wengine wanalipishwa faini na wengine wanapelekwa
mahakamanikufutiwa leseni na kuzuiliwa kuendesha chombo cha moto
kabisa.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Bakari Msangi amesema kuwa lengo kubwa la oparesheni
abiria paza sauti ni abiria kutambua wajibu na haki yake awapo ndani ya
chombo cha usafiri ikiwemo kutokukaa kimya pale anapomuona dereva
anakwenda kinyume na sheria za usalama barabarani,ulevi,kuyapita magari mengine mahali
ambapo hapastahili,kutoa lugha zenye utata kwa abiria,dereva kuongea na simu wakati anaendesha,yote haya anatakiwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.
ambapo hapastahili,kutoa lugha zenye utata kwa abiria,dereva kuongea na simu wakati anaendesha,yote haya anatakiwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.
Aidha amesema kuwa
abiria anatakiwakutoa taarifa pale dereva anapokuwa kwenye mwendo kasi,
kufunga mkanda awapo ndani ya gari ili kwamba kama imetokea dharura
yeyote asiweze kuhamishwa kwenye kiti alichokaa,pia wawapatie jeshi la polishi ushirikiano kwaajili ya usalama zaidi.
“Unajua abiria wengine ni chanzo cha ajali kwani wanakuwa wanamchochea
dereva kuendesha kwa mwendo kasi,wanapoulizwa na askari hawasemi kama
kuna tatiuzo hilo ni kosa hebu wapeni ushirikiano jeshi la polisi kikosi
cha usalama barabarani ni kwaajili ya faida yenu jamani.“alisisitiza
Bakari

Naye mwenyekiti wa usalama barabarani Jijini Arusha bi.Stella Rutaguza amesema
kuwa kazi kubwa abiria kutokukaa kimya pale anapomuona dereva anakiuka sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepuka ajali ambazo zinaepukika.
kuwa kazi kubwa abiria kutokukaa kimya pale anapomuona dereva anakiuka sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepuka ajali ambazo zinaepukika.
Amesema zowezi hili la Operesheni Abiria Paza Sauti litaendelea hadi
April 2017.
April 2017.
No comments :
Post a Comment