Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akizungumza na baadhi
ya viongozi wa Serikali wakati wa kumuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero, ambapo
alimshukuru kwa jitihada zake katika kusaidia upatokanaji wa mikopo kwa
ajili ya kutekeleza miradi ya Barabara, nishati, kilimo na elimu, Makao
Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) na aliyekuwa
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia
Kandiero wakifurahia uhusiano mzuri uliopo kati ya Benki ya AfDB na
Tanzania ambapo mpaka sasa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo inafikia
thamani ya Dola za Marekani Bilioni 2, wakati wa kuagwa kwa Dkt.
Kandiero, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia
Kandiero akitoa maneno ya shukrani mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), wakati akiagwa na Waziri
huyo, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akimkabidhi
zawadi ya shukrani aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia) wakati akiagwa rasmi baada ya
kupewa majukumu mengine ya Ukurugenzi Mkuu wa Benki ya AfDB kusini mwa
Afrika, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana
mkono na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia), baada ya kuagwa rasmi, katika Makao
Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Wakuu wa Idara na Taasisi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa
tayari kumuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero baada ya kufanya kazi nchini kwa
takribani miaka sita, Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini
Dar es salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia
Kandiero wakisaini mikataba miwili ya mikopo yenye masharti nafuu yenye
thamani ya shilingi Bilioni 360 kwa ajili ya kuongeza Ufanisi wa Tanesco
na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Wakulima nchini-TADB, Makao
Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia
Kandiero(kulia), wakibadilishana mikataba ya Mkopo wa Sh. Bilioni 360,
zitakazo kwenda katika Sekta ya Nishati ya Umeme na Benki ya Maendeleo
ya Kilimo nchini-TADB, tukio lililofanyika makao Makuu ya Wizara ya
Fedha na Mipango Jijini Dare salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia
Kandiero(kulia), wakibadilishana mikataba ya Mkopo wa Sh. Bilioni 360,
zitakazo kwenda katika Sekta ya Nishati ya Umeme na Benki ya Maendeleo
ya Kilimo nchini-TADB, tukio lililofanyika makao Makuu ya Wizara ya
Fedha na Mipango Jijini Dare salaam.
Mwakilishi
Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero
(kulia), akizungumza baada ya kusaini Mikataba miwili ya Mikopo yenye
masharti nafuu yenye thamani ya shilingi Bilioni 360, ambapo ameshauri
fedha hizo zitumike kikamilifu katika maeneo husika ambayo ni Bajeti na
kuendeleza kilimo. kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Bw. Doto James, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar
es salaam.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
…………………………………………………………………………….
Na Benny Mwaipaja-WFM, Dar es salaam
BENKI ya Maendeleo ya
Afrika-AfDB, imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola
Milioni 164, karibu Shilingi Bilioni 360, kwaajili ya kuchangia Bajeti
kuu ya Serikali katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na
kuongeza mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini-TADB.
Mikataba miwili imesainiwa leo
Jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Bw. Doto James kwa niaba ya Serikali na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika anayeondoka Dkt. Tonia Kandielo.
Mkataba wa kwanza uliosainiwa ni
kwa ajili ya kutunisha Mfuko Mkuu wa Serikali ambapo Benki hiyo imetoa
dola za kimarekani milioni 70 sawa na tsh 154 bilioni ambazo
zitaelekezwa kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Shirika la Ugavi wa
Umeme nchini-TANESCO.
Mkataba wa pili ni kwaajili ya
kuongezea mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini-TADB wenye
thamani ya dola Milioni 94 sawa na shilingi Bilioni 204 kwa ajili ya
kuiongezea uwezo Benki hiyo kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima
ili kuongeza mnyonyoro wa thamani kuanzia uzalishaji, uongezaji thamani
na upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao ya wakulima.
Uhai wa mikopo yote miwili
utakuwa ni miaka 40 ambapo serikali itaanza kuilipa baada ya miaka kumi
tangu kutolewa kwake, huku riba yake ikiwa chini ya asilimia 1.
Akizungumza baada ya kusainiwa
kwa mkopo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto
James, amesema mkopo huo umekuja wakati muafaka na utasaidia kukuza na
kuimarisha TANESCO na kuendeleza kilimo nchini.
“Tanzania ni nchi iliyonufaika
zaidi na mikopo yenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya
Afrika-AFDB ikilinganishwa na nchi nyingine yoyote iliyoko katika
Ukanda wa Kusini mwa Afrika” Alisema Bw. James.
Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi
wa AFDB anayeondoka Dkt. Tonia Kandielo amesema kuwa hadi sasa Benki
yake imeipatia Tanzania mkopo wenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani
bilioni 2, ambazo zimewekezwa kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi
wa miundombinu ya barabara, maji, nishati ya umeme, elimu na kilimo.
“Ninaamini kuwa hatua ya kuongeza
mtaji katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo-TADB itachochea maendeleo ya
kilimo nchini, na tunaahidi kuwa tutaendelea kuiwezesha zaidi siku
zijazo” Alisema Dkt. Kandielo.
Kuhusu Sekta ya Nishati, Dkt.
Kandielo amesema kuwa Benki yake imeona umuhimu wa kuliwezesha shirika
hilo ili liweze kutoa huduma kwa ufanisi zaidi ili kuchochea uchumi wa
Taifa.
“Mikopo hii inahusiana na
vipaumbele tulivyoviweka kama Benki ambavyo viko katika malengo matano
ambapo tunataka kuwekeza katika sekta ya nishati, uzalishaji wa chakula,
kuendeleza viwanda, kuiunganisha Afrika na kuboresha maisha ya waafrika
kwa ujumla” aliongeza Dkt. Kandielo
Wakati huo huo, Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amemuaga rasmi Dkt. Tonio Kandielo
ambaye amehamishiwa nchini Afrika Kusini kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki
hiyo atakaye simamia Kanda ya Kusini mwa Afrika.
Dkt. Mpango, amesifu jitihada
kubwa zilizofanywa na mwana mama huyo katika kipindi cha miaka 6
aliyokuwepo hapa nchini ambapo ameweza kusimamia vizuri maslahi ya
Tanzania katika Benki hiyo.
Amesema kuwa katika kipindi hicho
Tanzania imeshuhudia maendeleo makubwa katika sekta za ujenzi wa
miundombinu ya barabara, kilimo, maji na umeme, ambapo benki hiyo
ilihakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa.
Amemwomba Mkurugenzi Mkuu huyo
kuwezesha upatikanaji wa fedha kwaajili ya ujenzi wa Reli ya Kati kwa
kiwango cha kimataifa (Standard gauge) inayohitaji fedha nyingi,
kusimamia utekelezaji wa mradi wa umeme wa kikanda unaoanzia nchini
Zambia, uboreshaji wa Bandari ya Itungi na Mbambabay.
Akijibu hoja za Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Dkt. Tonia Kandielo amesema kuwa
anaamini mrithi wake ataendeleza mazuri aliyoyafanya na kwamba yeye
binafsi atahakikisha anafuatilia kwa karibu miradi ambayo mikataba yake
imesainiwa katika nyanja za maboresho ya sekta ya umeme na kilimo.
Mwisho
No comments :
Post a Comment