Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Kushoto), akifafanua jambo kwa
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mhe. Suzani Kiwanga (Wa tatu kulia), wakati
alipokagua barabara ya Ifakara, Taweta hadi Madeke (KM 225) Mkoani
Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (aliyenyoosha kidole),
akizungumza na wananchi wa Mlimba wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro
wakati alipokagua barabara ya Ifakara, Taweta hadi Madeke (KM 225)
Wanakijiji wa kata ya Msagati
wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro wakicheza ngoma na Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani baada ya
kuhakikishiwa barabara ya Ifakara –Kihansi (KM 130) itajengwa kwa
kiwango cha lami.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa tatu kushoto) akipata maelezo
kutoka kwa Mbunge wa Mlimba Mhe. Suzani Kiwanga (Wa pili kushoto) kabla
ya mkutano na wanakijiji wa Msagati Mkoani Morogoro.
Wanakijiji wa kata ya Msagati
wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (hayupo pichani)
wakati wa mkutano na wanakijiji hao.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
…………………..
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ameutaka uongozi wa Wakala wa
Barabara nchini TANROADS Mkoa wa Morogoro kuhakikisha wanafanya
matengenezo katika barabara zao ili ziweze kupitika katika kipindi chote
cha
mwaka.
Mhandisi Ngonyani ameyasema hayo
mara baada ya kukagua barabara ya Ifakara, Taweta hadi Madeke (KM 225)
ambapo amesema barabara ya Ifakara –Kihansi (KM 130) imeshafanyiwa
upembuzi yakinifu na usanifu wa kina unaendelea ili kipindi cha miaka
mitano iweze kujengwa kwa lami.
“Katika miaka hii mitano
tutahakikisha maandalizi ya awali ya kuwezesha barbara hii kujengwa kwa
kiwango cha cha lami yanakamilika na hivyo kutuwezesha kutenga fedha kwa
ajili ya kuanza ujenzi rasmi”. amesema Mhandisi Ngonyani.
Amesema kuwa barabara hiyo ni
kiungo muhimu kwa wakazi wa Ifakara na Kilombero kwa kuunganisha na Mkoa
wa Njombe na hivyo kukamilika kwake zitafungua fursa za kiuchumi na
kibiashara kwa wananchi hao.
Mhandisi Ngonyani amesisitiza
kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kutekeleza ahadi zote
zilizotolewa kwa wananchi kwa kuunganisha mikoa mbalimbali kwa ujenzi wa
barabara bora kwa viwango vya lami ili kurahisisha usafiri na kuongeza
kasi ya maendeleo kwa wananchi.
“Serikali ya awamu ya tano ipo
madarakani kwa ajili ya wananchi bila kujali itikadi zao,tumewahaidi
kuwaletea maendeleo hivyo tutajenga barabara zote tulizozihaidi kwa
wakati ili wananchi waendelee kunufaika na matunda ya serikali
yao”.amesisitiza Mhandisi Ngonyani.
Ameongeza kuwa Serikali kupitia
Wizara yake itaboresha huduma za mawasiliano katika shemu mbalimbali za
nchi ili kuwawezesha wananchi kuwasiliana wakati wowote ili kukuza
mahusiano yao kiuchumi, kibiashara na hivyo kukuza pato lao na la taifa.
“Tumeuomba uongozi wa kila wilaya
utuletee maeneo ambayo huduma za mawasiliano hazijafika au zinasumbua
ili sisi tuweze kuzishghulikia na kuzipatia huduma bora za mawasiliano”.
Amesistiza Mhandisi Ngonyani.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mlimba
Mhe. Suzani Kiwanga ameishukuru Serikali kwa uamuzi wa kuiweka barabara
hiyo katika mpango wa kuijenga kwa kiwango cha lami kwa kuwa itafungua
fursa mbalimbali kwa wananchi ambo wataweza kusafirisha mazo yao kwenda
katika masokoni kwa urahisi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano yupo Mkoani Morogoro katika ziara ya kukagua Miundombinu
ya barabara, Madaraja na Reli.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments :
Post a Comment