Baada
ya mapumzko ya siku ya kwanza katika kituo cha Mandara,timu ya
Wanahabari na Asakari wa jeshi la Ulinzi asubuhi yake walipanga mstari
mmoja kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea kituo cha pili cha Horombo.
Safari ilianza kwa kila mshiriki kuoenkana mwenye afya na nguvu ya kufikia ndoto ya kufika kilele cha Uhuru.
Baada
ya kupita katika msitu mnene wakati wa kuanza safari uelekeo wa kituo
cha Mandara na baadae kutoka Mandara kuelekea Horombo,kidogo kidogo hali
ya uoto ilionekana kubadilika kadri washiriki walivyokuwa wakielekea
sehemu za juu.
Mwendo
wa takribani saa saba kuanzia majira ya saa 2:30 asubuhi kutokea
Mandara.Washiriki wakafika eneo la nusu njia kuelekea Horombo na kupata
chakula cha Mchana.
Safari ikaendelea.
Hatimaye majira ya saa 11 jioni ,timu ya Wanahabari na Askari wa jeshi la Ulinzi wakaingia katika kituo cha Horombo.
Kama
ilivy ada kuchukua kumbukumbu likawa jambo la muhimu kwao ,na hapa
wakapa picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu na
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi TANAPA,Jenerali George Waitara
aliyekuwa mkuu wa msafara.
Majira
ya usiku wa saa moja ,timu ilipata chakula cha usiku na maelekezo
kutoka kwa mkuu wa waongoza watalii ,Chombo kwa ajili ya siku
iliyofuata.
Siku
iliyofuata ilikua ni siku ya mazoezi ,siku hii ilitengwa kwa ajili ya
kuzoea hali ya hewa ya juu wenyewe wanaita “Climatization”,mazoezi
yalikuwa ni kufanya safari ya kueleke eneo lijulikanalo kama Zebra.
Safari ya kuelekea Zebra ikaanza.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara pamoja na
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii ,Mstaafu ,Balozi Charles Sanga pia walikuwa
katika safari hiyo ya mazoezi.
Hatimaye timu ikafika eneo la Zebra.
Baadahi
yao Washiriki wakapata nafasi ya kupata kumbukumbu na wageni kutoka
Japan walikuwa wakipanda mlima Kilimanjaro kama Watalii.
Timu
ikapata picha ya pamoja na Naibu Kamanda wa kikosi cha Ardhini,Brigedia
Jenerali ,Jairo Mwaseba baada ya kufika katika eneo la Zebra.
Eneo la Zebra umaarufu wake unatokana na michoro iliyopo katika Mawe makubwa ikiwa mithili ya pundamilia.
Majira
ya jioni baada ya kurudi kituo cha Mandari ,timu ilijiandaa na safari
ya kuekeea kituo cha Kibo,hali ya hewa eeo hili ilikuwa ni ya kubadilika
badilika kila mara zaidi baridi ikiambatana na ukungu ndio ilitawala.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa katika safari hiyo.
No comments :
Post a Comment