Sunday, December 18, 2016

LUKUVI ATUA MKOANI MARA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI lubi

lubi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi walio na migogoro ya ardhi wakati wa ziara zake mikoani.
lubi-1
Muonekano wa Halmashauri ya Musoma Mjini.
……………….
Na. Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano – Wizara ya Ardhi)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara
zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.
Mhe. Lukuvi kwa siku ya jumatatu tarehe 19 Desemba 2016 atatua migogoro ya ardhi ya wilaya ya Musoma mkoani Mara na siku ya jumanne tarehe 19 Desemba 2016 atatua migogoro ya ardhi ya wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi atakutana na wananchi wa Musoma mjini na wananchi wa Bunda walio na kero za migogoro ya ardhi na kuzitatua pamoja na kutembelea miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika wilaya ya Musoma.
Aidha, Mhe. Lukuvi baada ya ziara hiyo anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha ambapo pia atatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo.
Hadi sasa Mhe. Lukuvi ndani ya mwezi huu wa Desesmba ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Kigoma na wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na Shinyanga mjini na katika mkoa wa Geita amefanya ziara katika wilayani Chato.

No comments :

Post a Comment