Kamishna wa Kanda Maalum ya
Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro amesema matukio ya Ubakaji
na Ulawiti yameongezeka kwa kiwango kikubwa katika mwaka wa 2016
ukilinganisha na mwaka 2015 kutokana na matukio yaliyolipotiwa kiwa
kipindi cha mwaka mzima.
Amesema hii inatokana na
kuanzishwa kwa Dawati la Jinsia na pia wananchi kupata uelewa na
kuripoti matukio hayo kila yanapotokea hii ndiyo sababu kubwa inayofanya
kuongezeka kwa matukio hayo katika mkoa wa Dar es salaam.
Kamishna Saimon Sirro akizungumza
katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati jijini Dar es salaam ametoa taarifa
hiyo wakati akielezea takwimu za matukio mbalimbali yaliyotokea kwa
mwaka 2016,
Kamishna wa Kanda Maalum ya
Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro amesema mwaka 2015 vitendo
vya ubakaji vilivyoripotiwa vilikuwa 972 wakati mwaka 2016 vitendo vya
kubaka vilivyoripotiwa vilikuwa 1030 ambapo ongezeko lilikuwa ni
asilimia 58 ukilinganisha na matukio hayo kwa mwaka 2015.
Akitoa takwimu za vitendo vya
kulawiti kwa mwaka 2015 amesema vitendo vya ulawiti vilivyoripotiwa ni
3010 ambapo mwaka 2016 vitendo hivyo viliripotiwa kwa matukio 383 sawa
na asilimia 73.
Amewataka wananchi kuacha matendo maovu kwani hayatawafikisha popote zaidi ya kuishia katika mikono ya sheria na kutupwa jela.
Kamishna wa Kanda Maalum ya
Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro aksisitiza jambo wakati
alipozungumza na waandishi wa habari katika kituo kikuu cha polisi Kati
jijini Dar es salaam.
Diana Masala Kaimu Mkurugenzi
Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA
akizungumzia msako uliofanywa kati ya Mamlaka hiyo na Polisi pamoja na
vyombo vingine vya usalama ambapo ulifanikisha kukamata bidhaa
mbalimbali za magendo.
Kamishna wa Kanda Maalum ya
Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akiangalia silaha
mbalimbali zilizokamatwa katika misako mbalimbali ya pilisi mwaka 2016.
Kamishna wa Kanda Maalum ya
Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akieleza jambo kwa
wanahabari wakati alipokuwa akionyesha silaha hizo.
Kamishna wa Kanda Maalum ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro mitungi ya Shisha iliyokamatwa katika misako hiyo.
Kamishna wa Kanda Maalum ya
Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akionyesha moja ya silaha
ya kivita zilizokamatwa katika misako hiyo.
Baadhi ya maofisa mbalimbali wa polisi wakiwa wametandaza silaha hizo zilizoonyeshwa mbele ya waandishi wa habari.
Kamishna wa Kanda Maalum ya
Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akionyesha moja ya bidhaa
zilizokamatwa kwa pamoja na jeshi la polisi likishirikiana na Mamlaka ya
Mapato TRA kulia ni Diana Masala Kaimu Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa
Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.
Kamishna wa Kanda Maalum ya
Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akionyesha moja akionyesha
moja ya mirija maalum inayotumika kutengenezea pombe haramu ya Gongo.
Kamishna wa Kanda Maalum ya
Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akionyesha viroba vya bangi
iliyokamatwa katika misako hiyo.
No comments :
Post a Comment