Rais
wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, akiongozana na Naibu
Katibu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Milla
pamoja na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso, kwenye
ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu kwa Wanatasnia wa Filamu na michezo ya
kuigiza mkoani Mara, yaliyoanza jana kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari
Mara Mjini Musoma.
Mafunzo hayo yamelenga kukuza weledi kwa wazalishaji wa filamu na maigizo ikiwemo kuzingatia uandishi bora wa miswada ili kuendana na ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi.
#BMGHabari
Naibu Katibu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Milla (kulia) akiteta jambo na Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso, kwenye ufunguzi wa
Mafunzo ya siku tatu kwa Wanatasnia wa Filamu na michezo ya kuigiza
mkoani Mara.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso (kushoto), pamoja na
Kaimu Afisa Utamaduni mkoani Mara, Shekudadi Said (kulia), wakiwa kwenye
ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu kwa Wanatasnia wa Filamu na michezo ya
kuigiza mkoani Mara.
Naibu Katibu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Milla (kulia), Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso (kushoto) pamoja na
wanatasnia wa filamu na maigizo mkoan Mara wakifuatilia kwa makini
mafunzo hayo.
Mmoja
wa Wakufunzi wa mafunzo hayo, Richard Ndunguru kutoka Chuo Kikuu cha
Dar es salaam idara ya Sanaa, akitoa mafunzo kwa wanatasnia wa filamu na
maigizo mkoani Mara. Amewapa miongozo bora kuhusiana na uandishi wa
miswada ya filamu, upigaji wa picha mnato pamoja na nyongevu kwa ubora
zaidi ili kuongeza mvuto wa kazi zao.
Wanatasnia
wa filamu na maigiozo mkoani Mara, wakifuatilia kwa umakini mafunzo
kutoka kwa Richard Ndunguru ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
salaam idara ya Sanaa.
Wanatasnia wa filamu na maigiozo mkoani Mara, wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo.
Wanatasnia wa filamu na maigiozo mkoani Mara.
Wanatasnia
wa filamu na maigiozo mkoani Mara wakiwa kwenye mafunzo ya filamu na
maigizo mkoani humo, yanayotolewa na Bodi ya Filamu nchini.
Taswira ndani ya ukumbi wa mafunzo hayo.
Soma Zaidi HAPA
No comments :
Post a Comment