Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi
Ofisi ya Makamu wa Rais wakiimba kwa pamoja wimbo wa wafanyakazi kabla
ya kuanza kwa Mkutano wa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya
Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo.
Kulia katibu wa baraza la wafanyakazi
Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Isaya Kisiri akifungua mkutano wa baraza
hilo uliofanyika katika Ofisi ya Makamu wa wa Rais Mtaa wa Luthuli
jijini Dar es Salaam. (kushoto) ni Katibu Mkuu mstaafu Bw. Mubarak
Abdul Wakil.
Kushoto Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Professor Faustin Kamuzora akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba aliyekaa
katikati, katika Mkutano wa Baraza la wafanyakazi cha Ofisi Hiyo
uliyofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
Katikati Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa
Rias Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wajumbe
wa Baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Makamu wa Rais leo Jijini DSM
kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Professor Faustine Kamuzora na
kulia ni Katibu wa Baraza hilo Bw. Isaya Kisiri.
NA EVELYN MKOKOI – DSM
Tawi la baraza la wafanyakazi katika
Ofisi ya makamu wa Rais limetakiwa kuwa ndo sehemu sahihi ya kujadili na
kutatua migogoro ya wafanyaki na siyo majukwaa ya siasa.
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi
anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe January Mkamba,
Lipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya
Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini dar es Salaam.
Mhe.Makamba alisema kuwa vikao vya baraza
la wafanyakazi vimekuwepo kisheria na ni muhimu wajumbe kukaa pamoja
kujadili masuala ya msingi yanyowahusu watumishi kwani wao ndo
waliowachangua hivyo, majadiliano yanayokuwepo katika vikao hivyo ni
nyenzo muhimu ya kuondoa migogoro na migomo mahala pa kazi.
“Nyie ni miongoni mwa watumishi wa Ofisi
ya Makamu wa Rais ambao kwa namna moja au nyingine mmeaminiwa na
kukabidhiwa dhamana ya kuwawakilisha wenzenu katika chombo hiki muhimu,
katika kuamua na kushauri Baraza juu ya masuala mbalimbali yanayolenga
kuleta ufanisi na utulivu ndani ya Ofisi yetu.alisisita Makamba”.
Aidha, Waziri Makamba alisema kwamba,
Lengo la vikao vya Baraza ni kuleta ufanisi wa utendaji kazi mahala pa
kazi kwa ajili ya manufaa ya Taifa kuelekezana, kushauriana na
kukumbushana, kuhusu majukumu ya ofisi na ushiriki wa wafanyakazi
katika kuyatekeleza na kuyasimamia, na aliongeza kwa kusema kuwa ni
fursa ya kipekee ya kutafakari utendaji wa kazi na majukumu ya Ofisi kwa
ujumla.
Kikao hicho cha baraza la wafanyakazi cha
Ofisi ya makamu wa Rais kimudhuriwa na wawakilishi kutoka TUGHE Taifa na
Mkoa na Wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Zanzibar
No comments :
Post a Comment