Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva akifungua kikao cha Tume ya Taifa
ya Uchaguzi na vyama vya Siasa vitakavyoshiriki katika uchaguzi mdogo
katika jimbo la Dimani Zanzibar leo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akitoa ufafanuzi kwa viongozi
wa vyama vya Siasa kuhusu maadili ya kuzingatia kwa vyama vya Siasa
wakati wa uchaguzi huo na maandalizi ya Uchaguzi wa jimbo la Dimani leo
mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva (kushoto) akiwa na wajumbe wa NEC
wakakifuatilia mkutano huo leo mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akitoa ufafanuzi kwa viongozi wa
vyama vya Siasa kuhusu maadili ya kuzingatia kwa vyama vya Siasa wakati
wa uchaguzi huo na maandalizi ya Uchaguzi wa jimbo la Dimani leo mjini
Zanzibar.
Viongozi wa vyama vya Siasa
vitakavyoshiriki uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani wakifuatilia mada
wakati wa mkutano wao na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mjini Zanzibar
leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva (kushoto) akizungumza na baadhi ya
viongozi wa vyama vya Siasa mjini Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa
mkutano wa Tume na Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi mdogo jimbo
la Dimani mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa
NEC Bw. Emmanuel Kawishe akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kisheria leo
wakati wa Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na viongozi
wa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani.
PICHA/Aron Msigwa – NEC.
……………
Na. Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imevitaka Vyama vya Siasa na wagombea watakaoshiriki Uchaguzi mdogo
katika jimbo la Dimani visiwani Zanzibar kuzingatia Sheria , Kanuni,
Taratibu na Maadili ili Uchaguzi huo uwe huru na wa haki na kuwawezesha
wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani
Lubuva wakati akizungumza na Viongozi 19 wa vyama vya Siasa
waliohudhuria mkutano wa maandalizi ya kufanikisha Uchaguzi mdogo wa
jimbo la Dimani utakaofanyika Januari 22, 2017.
Amewataka viongozi wa Vyama vya
Siasa waliohudhuria mkutano huo waendelee kudumisha hali ya amani na
Utulivu wakati wa kampeni za vyama vyao zinazotarajiwa kuanza hivi
karibuni pia kutoa ushirikiano kwa Waratibu na Wasimamizi wa Uchaguzi
huo.
“Ni matarajio ya Tume kuwa, Vyama
vya Siasa vitatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha uchaguzi
wetu katika jimbo la Dimani unakuwa Huru na wa Haki, lengo hili
litafanikiwa tu iwapo vyama na wagombea wote watazingatia na kufuata
sharia na maelekezo na maadili ya Tume” Amesisitiza Jaji Lubuva.
Amevitaka vyama vyote
vitakavyoshiriki katika uchaguzi huo wakati wa kampeni vijikite katika
kuelezea Sera zao na si vinginevyo pia kuepuka matumizi ya lugha ambazo
zinaweza kusababisha machafuko.
Ameeleza kuwa katika kufanikisha
uchaguzi huo kila Chama cha Siasa kina haki ya kuteua Wakala mmoja kwa
kila kituo cha kupigia kura ili kuongeza uwazi katika uchaguzi huo na
kuongeza kuwa mawakala hao watapangwa kwenye vituo vilivyo ndani ya
Shehia wanakoishi ili waweze kuwatambua wapiga kura katika eneo husika.
“Vyama vyote lazima muhakikishe
kuwa mawakala mnaowateua wanaelewa hatua zote muhimu za uchaguzi vituoni
kuanzia hatua ya kwanza ya kufungua kituo hadi kutangaza matokeo”
Amesisitiza.
Aidha, Mhe. Lubuva amewasisitiza
viongozi wa vyama hivyo watambue kuwa watu watakaopiga kura Januari
22,2017 ni wale walioandikishwa kwenye daftari la kudumu Wapiga Kura
ambao watakuwa na Kadi za kupigia kura na si vinginevyo.
“ Naomba ninyi viongozi wa vyama
vya Siasa muwakumbushe wanachama wenu walio na sifa na kadi za kupigia
kura wajitokeza siku ya kupiga kura, pia muendelee kuwahamasisha
wajitokeze kwa wingi kupiga kura siku hiyo” Amesema Mhe. Lubuva.
Katika hatua nyingine Mhe. Lubuva
amewakumbusha viongozi hao kuwa wananchi wakishapiga kura hawapaswi
kubaki katika eneo la vituo vya kwa kuwa vyama hivyo vitakuwa na
Mawakala ndani ya vituo hivyo na kuongeza kuwa ni marufuku kwa mgombea ,
Chama cha Siasa au Wakala kufanya kampeni Siku ya Uchaguzi kwani mwisho
wa kupiga kampeni ni siku moja kabla ya siku ya uchaguzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhan
akizungumza na viongozi wa vyama hivyo amesema kuwa maandalizi ya
uchaguzi huo yanaendelea vizuri huku akisisitiza kuwa ni matarajio ya
Tume kuwa Vyama vyote vitazingatia Katiba, Sheria, Kanuni, Maelekezo na
taratibu zote halalali zitakazotolewa na NEC.
Amewataka viongozi wa vyama hivyo
kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wapiga kura wao kuepuka kufanya
vitendo vya vurugu au viashiria vyovyote vya vurugu au uvunjifu wa amani
ili wananchi wote waweze kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuwachagua
viongozi wanaowataka.
Ametoa wito kwa wananchi wa jimbo
la Dimani walioandikishwa kupiga kura wajitokeze kwa wingi Januari 22,
2017 kwenda kupiga kura ili kufanikisha uchaguzi huo.
Kuhusu kampeni za vyama hivyo
amesema kuwa zitaanza Desemba 23, 2016 hadi Januari 21, 2017 na kuvitaka
vyama hivyo viwasilishe ratiba zao za kampeni kwa Msimamizi wa Uchaguzi
wa jimbo hilo ili viweze kukubaliana ambapo kampeni zitakua zinaanza
saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:30 jioni.
Kwa upande wao viongozi wa vyama
vya Siasa waliohudhuria mkutano huo kutoka vyama 19 wakizungumza kwa
nyakati tofauti wameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kutekeleza
majukumu yake kwa mujibu na kuahidi kutoa ushirikiano kwa waratibu na
wasimamizi wa uchaguzi huo.
Viongozi waliohudhuria mkutano huo
mjini Zanzibar wanatoka katika vyama vya ACT WAZALENDO,ADA, ADC,AFP,
CCK, CCM, CHADEMA, CUF, Demokrasia Makini, DP, NCCR –MAGEUZI, NLD, NRA,
SAU, TLP, UDP, UMD, UPDP na CHAUMA.
No comments :
Post a Comment