Wastaafu mbalimbali wakiwa kwenye foleni kusubiri zamu yao ya kuhakikiwa jijini Dodoma.
Wastaafu wakipeana maelekezo wakisubiri kuitwa kuhakikiwa mkoani Dodoma
Mkaguzi
wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Stanslaus Mpembe akitoa ufafanuzi
kwa waandishi wa habari kuhusu zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa
pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango, mkoani Dodoma.
Katibu wa Chama cha Wastaafu wa Mkoa wa Dodoma John Kanyeto akielezea jinsi zoezi la uhakiki lilivyoeshendwa mkoani Dodoma.
Mstaafu
Christina Mashamba (kushoto), akifanyiwa uhakiki na Wakaguzi wa Ndani
wa Halmashauri ya Mmanispaa ya Dodoma, kushoto ni Jestina Naftaz na
kulia ni Devotha Masanja.
……………………………………………………………………
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Wizara ya Fedha na Mipango,
imezindua zoezi la uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara
hiyo. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma mkoani Dodoma.
Lengo la kufanyika kwa zoezi hili ni kuhuisha orodha ya malipo ya Wastaafu kwa mara ya mwisho zoezi hilo lilifanyika mwaka 2014.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
zoezi hilo, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa
Serikali Msaidizi, Stanslaus Mpembe, alisema kuwa zoezi hilo
litafanyika kwa muda wa siku tano katika Kanda ya Kati ambayo
imejumuisha mikoa mitatu ya Morogoro, Dodoma na Singida.
Mpembe alisema lengo la kufanyika
kwa zoezi hilo ni kubaini mabadiliko ya taarifa za Wastaafu kama vile
kufariki ili kuepuka kulipa Wasiostahili.
‘Zoezi hili linafanyika kutokana
na utaratibu uliojiwekea Wizara kufanya uhakiki wa Wastaafu baada ya
muda fulani, zoezi hili litafanyika nchi nzima. Mpembe alisema’
Aliongeza kuwa zoezi hilo litaisaidia Serikali kuhakikisha Wastaafu wote wanapata haki zao na kwa wakati.
Aidha alitoa wito kwa Wastaafu
kujitokeza kwa wingi kuhakikiwa ili waweze kupata haki zao za msingi,
bila kusahau viambatanisho wanavyotakiwa kuwa navyo ili kurahisisha
zoezi hilo.
Naye Katibu wa Chama Cha Wastaafu
wa Mkoa wa Dodoma John Kanyeto aliishukuru Serikali kwa kuwajali na
kukubali ombi lao kuhusani Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu
Kijaji kwa kufikisha ombi lao walipofanya nae kikao la kulipwa mafao
yao kila mwezi badala ya kila baada ya miezi mitatu.
‘Niwaombe Wastaafu wenzangu wajitokeze kwa wingi kwani zoezi hilo ni la kwa faida yao. Kanyeto aliongeza’.
Kwa upande wa mstaafu Bi. Halima
Matonya alisema kuwa zoezi hilo limeenda vizuri na ameipongeza Serikali
kwa kuwajali na kuwakumbuka, na amewapongeza pia Waratibu wa zoezi hilo
kwa kujipanga vema na kutoa maelekezo vizuri hivyo kufanya zoezi hilo
kuchukua muda mchache.
Tayari zoezi kama hilo la uhakiki
wa wastaafumwanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango limefanyika
katika Kanda za Pwani na Nyanda za Juu Kusini ambapo ilijumlisha mkoa wa
Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Katavi, Ruvuma, na Songwe.
Baada ya kukamilika kwa zoezi
hilo kanda ya kati, zoezi hilo litaendelea katika Kanda ya Kaskazini
ambapo litajumuisha Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga
No comments :
Post a Comment