Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wajumbe wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta
uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Wajumbe wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wataalamu wa masuala ya gesi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kufungua mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Wazalishaji Petroli Afrika, Mhandisi Mahaman Laouan Gaya mara baada ya kufungua mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
………………………………………………………………….

wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema
kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika
kuhakikisha rasilimali ya gesi na mafuta inakuwa ni chachu ya kukuza
uchumi wa taifa na wa wananchi kwa ujumla.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo 22-Nov-2016 Jijini Dar es
Salaam wakati akifungua mkutano wa mwaka wa kujadili masuala ya gesi na
mafuta barani Afrika ulioandaliwa na Kampuni ya Getenergy ya
Uingereza.
Uingereza.
Katika
hotuba yake, Makamu wa Rais amewahakikishia washiriki wa mkutano huo
kuwa Tanzania imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya
mafuta na gesi na itakuwa bega kwa bega na wadau wanaotaka kuwekeza
katika sekta hiyo ili kuhakikisha uwekezaji utakaofanyika unakuwa na
manufaa kwa pande zote mbili.
Amesisitiza
kuwa kwa sasa Serikali ya Tanzania inaendelea na mkakati kabambe wa
kusomesha wataalamu wa fani ya mafuta na gesi ndani na nje ya nchi ili
kuhakikisha taifa linajitosheleza kwa wataalamu hao ambao watakuwa na
uwezo na ujuzi wa kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa katika sekta za
gesi na mafuta.
Makamu
wa Rais amesema Tanzania imegundua kiasi kikubwa na gesi na ana imani
kubwa kuwa mafuta nayo yanapatikana hivyo ni muhimu kwa mataifa ya
Afrika kujipanga kuwa na wataalamu wake wazalendo wa kutosha
watakaoshikiri katika uchumi wa gesi na mafuta kwa kuajiriwa kwenye
makampuni yanajihusisha na utafiti na
uchimbaji wa gesi na mafuta.
uchimbaji wa gesi na mafuta.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema anaimani kubwa kuwa rasilimali ya gesi na mafuta zitakagundulika na
kuchimbwa barani Afrika zitasaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi
wa mataifa hayo, uchumi ambao utasaidia kuimarisha utoaji wa huduma
bora za kijamii kwa wananchi katika nchi husika.
Mkutano huo wa siku Mbili wa Kimataifa umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya gesi na mafuta kutoka ndani na nje ya nchi ambao wanajadili kwa kina na kubadilishana uzoefu kuhusu njia bora za uwekezaji katika sekta hiyo barani Afrika.
Kwa upande wake,Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kwa Serikali itaendelea kusomesha wataalamu wake ndani na nje ya nchi ili kujitosheleza kwa wataalamu wa sekta hiyo.
No comments :
Post a Comment