Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Kikanda wa Wadau wa Sekta ya Misitu wa nchi ya
Finland na Tanzania uliofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency,
Jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kuhamasisha
uwekezaji na kukuza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika
uendelezaji wa misitu nchini. Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa
Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland,
Taasisi ya Uongozi – UONGOZI Institute na Shirika la Maendeleo ya
Kifenda la Finland – FINFUND.
Waziri
wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Serikali ya Finland, Kai
Mykanen akizungumza katika Mkutano huo ambapo ameahidi kuendeleza
ushirikiano uliopo baina ya Finland na Tanzania katika kuendeleza
Misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho ikiwa ni pamoja na kukuza
teknolojia ya uhifadhi wa mazingira ya kupunguza hewa ukaa.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano huo, kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel
Mwakalukwa, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge, Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili, Eng. Angelina Madete na Kaimu Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.
Baadhi
ya wajumbe katika mkutano huo wakifualia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa
na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza
na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Finland ikiongozwa na Waziri
wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo, Kai Mykanen (wa pili kushoto)
muda mfupi kabla ya ufunguzi wa mkutano huo. Wengine kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mehenge, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili
na Utalii, Meja Generali, Gaudence Milanzi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi
wa habari muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano huo. Alieleza kuwa
Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa misitu
unaotokana na uvunaji wa mkaa na ukataji wa magogo, uvunaji wa miti usio
endelevu jambo lililoisukuma Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali
ikiwemo Serikali ya Finland na wananchi kwa ujumla kwa ajili kuendeleza
misitu kwa kupanda miti mingi zaidi iweze kukidhi mahitaji yaliyopo.
Aliongeza kuwa ni marufuku kusafirisha magogo na kwamba Serikali ya
awamu ya tano imelenga kukuza viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani
kwenye mazao ya misitu na kuyauza kama bidhaa. Kushoto kwake ni Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanzi na
kulia kwake ni Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph
Semboja.
(Picha na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili naUtalii)
No comments :
Post a Comment