Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng.Edwin Ngonyani (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo
kwa kaimu Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Mtwara Eng.
Dotto Chacha alipokagua barabara ya Mangaka-Mtambaswala na Mangaka
–Tunduru.
Kaimu Meneja wa Wakala wa barabara
(TANROADS) Mkoa wa Mtwara Eng. Dotto Chacha akimuonesha Naibu Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.Edwin Ngonyani (katikati) eneo la
mzunguko wa Mangaka linalohitaji marekebisho katika barabara ya
Mangaka –Mtambaswala na Mangaka –Tunduru ambao ujenzi wake kwa kiwango
cha lami umekamilika.
Muonekano wa barabara ya
Mangaka-Mtambaswala inayounganisha Tanzania na Msumbiji ambayo ujenzi
wake kwa kiwango cha lami umekamilika barabara hii inatarajiwa
kuchochea uchumi wa mkoa wa Mtwara.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewahakikishia wananchi wa Wilaya za
Kibiti, Rufiji na Mafia kuwa ujenzi wa gati la kisasa katika eneo la
Nyamisati utaanza wakati wowote baadaye mwakani na kukamilika ifikapo
Machi 2018.
Akizungumza mara baada ya kukagua
eneo litakapojengwa gati hilo katika pwani ya Nyamisati wilayani Kibiti
Eng.Ngonyani amewataka viongozi na wananchi wa wilaya hizo kuwa na
uvumilivu katika kipindi hiki ambacho Serikali inatafuta ufumbuzi wa
kudumu.
“Endeleeni kutunza mazingira ya
eneo hili na kutunza mazingira ya bahari ili kudhibiti mabadiliko ya
tabia nchi katika eneo lenu, Serikali imejipanga kukabiliana na
changamoto inayowakabili sasa hivyo toeni ushirikiano unaohitajika ili
kuiwezesha Mamlaka ya Bandari nchini(TPA) kutekeleza ujenzi wa gati
hili”. Amesisitiza Eng. Ngonyani.
Naye Mbunge wa Mafia Mhe. Mbaraka
Dau amemhakikishia Naibu Waziri Ngonyani kuwa kukamilika kwa gati la
kisasa katika pwani ya Nyamisati kutahuisha shughuli za kiuchumi kwa
wakazi wa Mafia na Mkoa wa pwani kwa ujumla.
“Kukamilika kwa gati hili
kutavutia wasafirishaji wengine kuleta vyombo vya usafiri na hivyo
kushusha gharama za usafiri kati ya Kibiti na Mafia ambapo sasa ni zaidi
ya shilingi elfu kumi na tatu kwa safari”. Amesema Mhe. Dau.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri
Ngonyani amekagua barabara ya Ikwiriri-Lindi, Nanyumbu
–Masugulu-Mtambaswala na Mangaka -Tunduru na kumtaka Meneja wa Wakala wa
barabara Mkoa wa Mtwara Eng.Dotto Chacha kuhakikisha barabara inakuwa
salama wakati wote kwa kudhibiti madereva wanaoegesha magari barabarani
isivyostahili.
Naibu Waziri Ngonyani yupo katika
ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Bandari na Mawasiliano katika
mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments :
Post a Comment