Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akizungumza na wateja waliofika
kupata huduma katika ofisi za Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini
Dar es Salaam. Wapili kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria
Lembeli Mwigulu alifanya ziara katika idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya
utendaji katika ofisi hizo, alizungumza na maafisa na askari Uhamiaji na
baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji
Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo. (PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (aliyevaa tai) akiangalia fomu za
kuomba pasipoti za Idara ya Uhamiaji mara baada ya kuchapishwa katika kiwanda
hicho kilichopo Kijichi, jijini Dar es Salaam. Waziri Mwigulu alikitembelea
kiwanda hicho pamoja na Mradi wa nyumba za Makamishna zinazojengwa katika eneo
hilo. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali
wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (kulia) alipokuwa anatoa hotuba fupi na baadaye
kumkaribisha Waziri huyo kuzungumza na maafisa na askari wa Uhamiaji wa Makao
Makuu wa Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Waziri
Mwigulu aliwataka askari hao waongeze juhudi zaidi ya kuwakamata wahamiaji
haramu na kuwachukulia hatua kali bila kuwaonea watu katika ukamataji wao
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (aliyevaa tai) akikaribishwa na
Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (kulia) pamoja
na maafisa waandamizi wa Idara hiyo katika ofisi za Makao Makuu, Kurasini
jijini Dar es Salaam. Mwigulu alifanya ziara katika idara hiyo kwa kutembelea
maeneo ya utendaji katika ofisi hizo, alizungumza na maafisa na askari Uhamiaji
na baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji
Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (aliyevaa tai) na Kaimu Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli wakitoka moja ya nyumba zinazojengwa kwa
ajili ya Makamishna wa Uhamiaji, Kijichi, jijini Dar es Salaam. Waziri Mwigulu
alizikagua nyumba hizo ambazo zipo hatua za mwisho kukamilika. Waziri huyo
alifanya ziara katika idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi
hizo na baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha
Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Makamishna, Maafisa
na Askari wa Uhamiaji katika ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini
jijini Dar es Salaam. Mwigulu aliwapongeza watumishi hao kwa kazi
nzuri wanayoifanya na aliwataka waongeze juhudi zaidi ya kuwakamata wahamiaji
haramu na kuwachukulia hatua kali bila kuwaonea watu katika ukamataji wao. Waziri
huyo alifanya ziara katika idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika
ofisi hizo na baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha
Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo
No comments :
Post a Comment