Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionyesha hati ya muswada wa sheria ya Utafutaji
na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya mwaka 2016, baada ya kusaini hati hiyo
katika hafla iliyofanyika leo Novemba 15, 2016 Ikulu Mjini Unguja, ambapo
Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria (PICHA NA
IKULU YA ZANZIBAR)
NA K-VIS BLOG
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein,
ametia saini muswada wa sheria ya
Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,
uliopitishwa hivi karibuni na Baraza la Wawakilishi na kusema, rasilimali hizo
ni mali ya Wazanzibari.
Akijibu
swali la mwandishi wa habari, Munir Zacharia aliyetaka kujua kama Rasilimali
hizo endapo zitapatikana visiwani humo, yawezekana zikachimbwa huko na
kupelekwa Bara (Tanzania bara)?, “Mafuta na gesi yakipatikana Zanzibar, ni mali
ya Wazanzibari, kama wenzetu wa Tanzania Bara, wakiyahitaji, tutawauzia kama
ilivyo kwa wengine, barrel, (pipa), moja dola 70, haya,” Alijibu Dkt. Shein
katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali yake, wakiwemo,
Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Profesa Sospeter Muhongo na Mwanasheria Mkuu, wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, George Masaju.
Hafla
hiyo iliyokuwa ikipeperushwa moja kwa moja na Televisheni ya Zanzibar, (ZBC),
ilifanyika Ikulu ya Zanzibar leo Novemba 15, ambapo baada ya Rais kusaini
muswada huo na kuwa sheria, alitoa nafasi ya kuulizwa maswali mawili tu.
Miongoni
mwa maswali yaliyoulizwa ni pamoja na lile la mtangazaji wa ITV-Zanzibar,
Farouk Karim ambaye aliuliza, kuwa wapo wanasheria waliotahadharisha kuwa, Rais
wa Zanzibara sisaini muswada huo kwa vile atakuwa amekiuka katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambayo kwa mujibu wa Karim, ni swala la Muungano.
Akijibu
swali hilo, Rais wa Zanzibar alisisitiza kuwa , hajafunja sheria wala katiba,
na kwamba alichofanya kimo ndani ya katiba ya Zanzibar na kwamba, na kuwashauri
wanasheria hao kusoma vifungu vyote na sio nusu nusu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini muswada wa sheria ya Utafutaji na
Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016, katika hafla iliyofanyika leo
ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama
vya Siasa walihudhuria hafla hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Profesa Sospiter Muhongo,(kushoto), akiwa na Spika wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar Mhe, Zubeir Ali Maulid (kulia) wakiwa katika hafla ya
Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na
Gesi asilia ya mwaka 2016, Ikulu ya Zanzibar Novemba 15, 2016
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi
na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya utiaji
saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia
ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi
na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya utiaji
saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia
ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Viongozi kutoka kushoto Kadhi Mkuu wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Sheihk Khamis Haji,Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na
Michezo Mhe,Radhid Ali Juma,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na
Naibu waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe,Juma Makungu Juma
wakiwa katika Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji
na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa leo
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein Ikulu Mjini Unguja
Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama
Zanzibar wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya
Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa leo
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
No comments :
Post a Comment