Tuesday, November 15, 2016

SERIKALI KUJENGA VITUO VITATU KWA KILA HALMASHAURI KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI NA MLANGO WA KIZAZI.


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza hii leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bure ya Uchunguzi na Matibabu ya Saratani ya Matiti na Shingo ya Kizazi mkoani Mwanza.
Na BMG
Amesema serikali itaendelea kuboresha huduma za saratani ikiwemo kupatikana katika hospitali za rufaa Bugando Jijini Mwanza na KCMC Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es salaam.
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu, amesema watanzania wengi wanakabiliwa na magonjwa ya saratani na kuwahimiza kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye ufunguzi huo
Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonald Subi, akizungumza kwenye uzinduzi huo, ambapo amesema uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi uliofanyika katika halmashauri za Buchosa, Ukerewe na Kwimba umewafikia wanawake 1294 na kati yao, 58 wana dalili za awali za saratani ya matiti, 13 saratani ya kizazi na kwamba 15 wamepewa rufaa ya uchunguzi zaidi hospitali ya rufaa Bugando.
Rais wa Chama cha Madaktari Wanawake nchini MEWATA, Dkt.Sarafina Mkuwa, amesema lengo la kampeni hiyo ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi ni kuhamasisha wananchi kupata huduma hizo mapema kwani magonjwa hayo hutibika ikiwa mgonjwa ataanza matibabu mapema.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto), akisalimiana na Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Angelina Mabula (kulia) ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngussa, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Furahisha
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akilakiwa kwenye uwanja wa Furahisha
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto), akisalimiana na Grace Shindika ambaye ni Katibu wa UWT Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akilakiwa kwenye uwanja wa Furahisha
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na mwakilishi kutoka Marie Stops Tanzania, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Furahisha
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akilakiwa kwenye uwanja wa Furahisha
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akilakiwa na wawakilishi kutoka Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania MEWATA, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Furahisha
Mwakilishi kutoka MEWATA akitoa maelekezo kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia), wakati akikagua mabanda ya huduma kwenye Uwanja wa Furahisha
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akiteta jambo na Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu 
Kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu pamoja na Rais wa MEWATA, Dkt.Sarafina Mkuwa.
Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ilemela (kulia), wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Meza kuu, aliyesimama ni mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, akisalimia
Mmoja wa akina mama akielezea kufurahishwa kwake na huduma za bure za uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza wamesema hawamudu gharama za uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi hivyo kampeni hiyo ya bure itawasaidia na wanaomba iwe inafanyika mara kwa mara
Wanafunzi nao wamenufaika na uchunguzi huo ambapo wamesema ni jambo jema kwani wanatambua afya zao mapema na wameshauri watanzania kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara
Wamesema bado upimaji na matibabu ya saratani nchini ni ghari hivyo wengi wao hawamudu gharama zake ambapo wameomba kampeni hiyo iwe endelevu.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza wakiwa kwenye foleni kupata huduma ya uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi bure
Mamia ya wanawake Jijini Mwanza waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi bure.
Na George Binagi-GB Pazzo
Serikali inatarajia kujenga vituo vitatu kwa kila halmashauri nchini ili kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu ya mapema ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi kwa akinamama kwa lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa hayo.

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, amebainisha hayo Jijini Mwanza wakati akizindua kampeni ya bure ya upimaji wa awali na matibabu wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto imetenga shilingi bilioni saba kwa ajili ya ununuzi wa dawa za magonjwa hayo huku benki ya dunia ikiwa imetoa shilingi bilioni tano kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma hizo katika ngazi za halmashauri nchini.

Ameongeza kwamba serikali itaendelea kuboresha huduma za saratani ikiwemo kupatikana katika hospitali za rufaa Bugando Jijini Mwanza na KCMC Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es salaam pamoja na vifo kwa akina mama ambavyo ni zaidi ya asilimia 60 nchini.

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu, amesema watanzania wengi wanakabiliwa na magonjwa ya saratani na kuwahimiza kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara.

Baadhi ya wananchi mkoani Mwanza wamesema bado upimaji na matibabu ya saratani nchini ni ghari hivyo wengi wao hawamudu gharama zake ambapo wameomba kampeni hiyo iwe endelevu.

Rais wa Chama cha Madaktari Wanawake nchini MEWATA, Dkt.Sarafina Mkuwa, amesema lengo la kampeni hiyo ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi ni kuhamasisha wananchi kupata huduma hizo mapema kwani magonjwa hayo hutibika ikiwa mgonjwa ataanza matibabu mapema.

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMI AZINDUA KAMPENI YA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATI NA YA MLANGO WA KIZAZI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa uzazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Novemba 15, 2016. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania Dk. Serafina Mkuwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim kwenye moja ya mabanda yaliokuwa yanatoa huduma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa uzazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Sehemu ya Wanawake waliojitokeza kwennye uzinduzi huo.
                                              

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa serikali imeweka mipango na mikakati thabiti ya kukabiliana na idadi kubwa ya vifo vinasababishwa na saratani  hasa saratani ya matiti na mlango wa kizazi kote nchini.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza wakati akizundua kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani humo.
Katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi wa mkoa wa Mwanza waliojitokeza katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo Kusini mwa Jangwa la Sahara ina kiwango cha juu cha vifo vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi ambapo asilimia 60 ya vifo vyote   vinavyotokea Kusini mwa jangwa la Sahara vinasababishwa na saratani hiyo.
Makamu wa Rais amesema kuwa vifo vingi vinatokana na uelewa mdogo, imani potofu,gharama kubwa za matibabu,unyanyapaa na kuwepo kwa vituo vichache wa kufanyia uchunguzi  hapa nchini ambapo kwa sasa tiba ya mionzi inapatikana katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Roas, Dar es Salaam.
Katika kukabiliana na tatizo hilo, Makamu wa Rais amesema kuwa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imepokea kiasi cha shilingi bilioni Tano kutoka Benki ya Dunia fedha ambazo zitawezesha vituo Vitatu kwa kila Halmashauri ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu ya mapema ili wanawake kote nchini hasa wale wale wa vijijini waweze kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa ukaribu kwenye maeneo wanayoishi.
“Wote ni mashuhuda kwa namna saratani ya mlango wa kizazi inavyosababisha vifo vingi hali ambayo hutokana  na magonjwa wanaogundulika na ugonjwa kuwa tayari wamefikia hatua isiyotibika na kwa pamoja saratani hizi mbili husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akinamama”

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa tayari kuna vituo takribani 300 vinavyotoa huduma za upimaji wa dalili za awali katika vituo vya afya kote nchini na hivyo vituo vipya vitaongeza huduma endelevu ili kupunguza vifo vitokanavyo na saratani.
Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanaume kote nchi kuunga mkono kampeni hiyo kwa kuwaruhusu wanawake na wasichana kwenda kupima saratani hiyo na amewapongeza na kuwashukuru wanaume wa mkoa wa Mwanza kwa kuwasindika wake zao na watoto wao wa kike kwenda kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kupima saratani hiyo na kupatiwa tiba.

Makamu wa Rais amepongeza Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania- MEWATA na wadau wote kwa kuanda zoezi la huduma za uchunguzi wa dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania  ni miongoni mwa nchi zenye wagonjwa wengi wa saratani ya mlango wa kizazi na pia ndiyo inaongoza katika nchi za Afrika mashariki.

Amesema kuwa idadi ya wanawake 6241 hugundulika kuwa na saratani kila mwaka  na kati y



Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la ElimuyaUfundi (NACTE) Dk. Adolf Rutayuga (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wahabari wakati akitangaza kufutiwa usajili vyuo 26 kwakosa  la kukiuka masharti ya usajili.

No comments :

Post a Comment