Mkuu
wa Kitengo
cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa
Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA), Sarah Kibonde Msika, akikabidhi mifuko 100 ya saruji kwa Afisa
Mipango wa Wilaya ya Kibaha Vijijini, Bw. Wambura Yamo kwa ajili ya
ujenzi na ukarabati wa madarasa ya Shule za Msingi za wilaya hiyo, hivi
karibuni.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha Vijijini,
Bw.Wambura Yamo, akimshukuru Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ally Masaniga baada ya
kukabidhiwa mifuko 100 ya saruji na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na
Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia), kwa ajili ya ujenzi na
ukarabati wa madarasa ya Shule za Msingi za wilaya hiyo.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha Vijijini, Bw.
Wambura Yamo, akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa
SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia), mara baada ya kumkabidhi mifuko 100 ya
saruji kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya Shule za Msingi za
wilaya hiyo.
Sehemu
ya mifuko 100 ya saruji iliyotolewa msaada na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti
wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha
Vijijini kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya Shule za Msingi
za wilaya hiyo
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa
SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia), Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha
Vijijini, Bw. Wambura Yamo (katikati) na Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo,
Ally Masaniga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano hayo,
wilayani humo hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa
SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia), akiagana na Afisa Mipango wa Wilaya
ya Kibaha Vijijini, Bw. Wambura Yamo, mara baada ya makabidhiano hayo,
wilayani humo hivi karibuni.
No comments :
Post a Comment