Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa
yasioambukiza (NCD) Prof. Ayoub Magimba akisisitiza jambo mbele ya
madaktari na wadau wa afya ngazi ya mkoa na wilaya hawapo pichani wakati
wa kufunga mkutano Wa siku tatu Wa Madaktari na wadau Wa afya ngazi ya
mkoa na wilaya katika kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa
yasioambukiza uliofanyika mkoani Morogoro.
Baadhi ya Madaktari na wadau wa
afya ngazi ya mkoa na wilaya hawapo waklijadili sera na mipango wakati
wa kufunga mkutano Wa siku tatu Wa Madaktari na wadau Wa afya ngazi ya
mkoa na wilaya katika kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa
yasioambukiza uliofanyika mkoani Morogoro.
Na Ally Daud-MAELEZO-MOROGORO
WATUMISHI wa Umma wametakiwa
kufanya mazoezi ya viungo Mara moja kwa wiki ili kujiepusha na magonjwa
yasioambukiza ili kujenga watumishi wenye afya imara kwa maendeleo ya
taifa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
Msaidizi wa magonjwa yasioambukiza (NCD) Prof. Ayoub Magimba wakati Wa
kufunga mkutano Wa siku tatu Wa Madaktari na wadau Wa afya ngazi ya mkoa
na wilaya katika kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa
yasioambukiza uliofanyika mkoani Morogoro.
“Katika mkutano huu wa kupata
mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa yasioambukiza tumeazimia kua na
Sera inayoelekeza watumishi wote wa Umma wafanye mazoezi ya viungo
siku moja kwa wiki ikiwa ni sehemu ya majukumu yao” alisema Prof.
Magimba
Aidha Prof. Magimba amesema kuwa
mazoezi hayo ni sehemu ya majukumu ya watumishi wa Umma ili kuwasaidia
wale wanaokosa muda wa kufanya mazoezi majumbani kwao ili kujikinga na
magonjwa hayo.
Mbali na hayo Prof. Magimba
amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuepuka matumizi ya Mara kwa mara ya
Sigara na vileo kwa pamoja na badala yake wajikite kwenye mazoezi na
utumiaji wa vyakula asilia.
Kwa upande wake Daktari bingwa Wa
magonjwa ya ndani Dkt. Meshack Shimwela ambaye ni mshiriki wa mkutano
huo amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuzingatia na utekelezaji wa
Sheria za barabarani ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na ajali
mpaka kufikia mwaka 2030.
“Watanzania hasa madereva wa
vyombo vya moto wanatakiwa kuzingatia na kutii Sheria za barabarani
hususani kuacha kuendesha vyombo vyao wakati wamelewa ili kupunguza
asilimia 50 ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani hadi kufikia
2030” alisema Dkt. Shimwela
Aidha Dkt. Shimwela amesema kuwa
katika mkutano huo wameadhimia kuishauri serikali kutenga maeneo maalum
ya kuvutia Sigara pamoja na kuweka muda maalumu wa kunywa pombe ili
kujikinga na kuepuka magonjwa hayo.
Mkutano huo uliokutanisha
madaktari wa ngazi za mkoa na wilaya zote nchini umelenga kutengeneza
Sera na mikakati ya mwaka 2017 hadi 2020 katika kupambana na magonjwa
yasioambukiza kama kisukari, kansa,shinikizo la damu, ajali za
barabarani na uzito kuzidi kiasi ili kujenga taifa lenye afya na
Maendeleo.
No comments :
Post a Comment