Wednesday, November 23, 2016

Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) na taasisi ya Open Heart International OHI waendelea na upasuaji wa moyo

jkn1
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari wenzao  wa Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo kwa njia ya kufungua kifua na kuziba  tundu la moyo. Kulia ni Dkt. Bingwa wa Upasuaji  Hussein  Hassan akifuatiwa na madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Dk. Godwin Godfrey (kushoto) na Dkt. Benjamin Bierbach.
jkn2
Madaktari bingwa wa moyo pamoja na wauguzi kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia wakiendelea na kazi ya kumfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo kwa njia ya kufungua kifua na kuziba tundu lililopo kwenye moyo. Taasisi hizo  hivi sasa ziko katika kambi maalum ya  siku sita ya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo, katika kambi hiyo wagonjwa 20 wanarajiwa kupata matibabu.
Picha na Anna Nkinda – JKCI

No comments :

Post a Comment