Wataalamu wa kilimo wakiongea na wakulima wa zao la shahiri wanaoshilikiana na TBL -Karatu
Wananchi wakipatiwa mafunzo ya ujasiriamali kupitia mpango wa RDP wa TBL
Wakulima wanaoshirikiana na TBL katika mashamba yao wilayani Karatu
Moja ya panel ya kuvuna umeme wa jua katika kiwanda cha Mbeya
………………………………………………………………………
Kampuni
ya TBL Group imeeleza mkakati wake wa kuendelea kutekeleza malengo yake
yanayoshabihiana na Malengo ya Maendeleo Endelevu ((SDGs) yaliyobainishwa
na Umoja wa Mataifa ,lengo kubwa likiwa ni kuondoa changamoto
mbalimbali zilizopo kwenye jamii na kuifanya dunia iwe sehemu nzuri ya
Kuishi.
Meneja
wa Uendelezaji Mauzo wa TBL,Bw. Malaki Sitaki,aliyasema hayo alipokuwa
akitoa tathmini ya kampuni katika kutekeleza mpango wa kutoa elimu ya
ujasiriamali kwa wateja wanaouza bidhaa zake kupitia mpango wa Retail
Development Programme ulioanza mwaka jana unaoenda sambamba na elimu ya
Unywaji Kistaarabu.
Alisema
kuwa hivi sasa kampuni hiyo imejikita zaidi kufanya biashara sambamba
na kwendana na malengo hayo dhamira kubwa ikiwa ni kuyafanikisha na
kuondoa changamoto zilizopo kwenye jamii mojawapo ikiwa ni kuondoa
umaskini uliokithiri kwenye jamii mbalimbali.
“Tumeanza
kwa kasi kufanya kazi na wananchi katika maeneo tunayofanyia biashara
kwa kusaidia miradi mbalimbali yenye mwelekeo wa kufanikisha Malengo ya
Maendeleo Endelevu kama ulivyo mtizamo wa kampuni na mafanikio makubwa yameanza kupatikana hususani katika nyanja za uchumi, ustawi wa jamii na utunzaji wa mazingira”.Alisema.
Sitaki
alisema kampuni imejikita katika kutunza mazingira,kuboresha huduma za
maji na uhamasishaji wa matumizi mazuri ya maji,kusaidia wanawake kwenye
miradi ya kiuchumi endelevu,kutoa elimu ya ujasiriamali na unywaji
kistaarabu,kusaidia wakulima kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za
kilimo,kupanua wigo wa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja
na kusaidia miradi katika sekta ya afya na elimu.
Alisema
TBL itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kuleta ufanisi
kukabiliana na changamoto mbalimbali na kushirikiana na wananchi kuleta
mabadiliko chanya kwa kuwa inaamini wananchi ndio wadau wakubwa wa
kufanikisha malengo haya na hawapaswi kuachwa nyuma.
Kuhusiana
na maendeleo ya mpango wa kutoa elimu ya ujasiriamali unaoendeshwa na
kampuni alisema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika kipindi cha
miaka 2 tangia uanzishwe kwa kuwafikia wajasiriamali zaidi ya 2,500
kutoka mikoa yote ya Tanzania na matarajio ya kampuni ni kuwafikishia elimu zaidi ya wajasiriamali 20,000 hadi ifikapo mwaka 2019.
“Mwitikio wa wahitaji wa mafunzo haya ni mkubwa na kinachofurahisha idadi kubwa ya wajasiriamali wanaoshiriki mafunzo
haya ni Wanawake.Hii kwetu ni faraja kubwa kwa kuwa tunaamini
kuwaelimisha wanawake inakuwa umeelimisha jamii nzima na ni rahisi
kuleta maendeleo na mabadiko endelevu kama ilivyo lengo la mpango
huu”.Alisema Malaki
Alisema thatmini ya awali ya mpango imebainisha kuwa mafunzo yanaendelea kuwanufaisha wasambazaji wa bidhaa za TBL ngazi ya chini (Retailer level) na asilimia kubwa ya waliopata mafunzo haya wanaendelea kuendesha biashara zao na kujipatia faida inayowawezesha kuboresha maisha yao na familia zao kwa
kuzipatia lishe nzuri,watoto wao kupata huduma bora za kiafya na elimu
.” Huu ndio mwelekeo wa uwekezaji wetu unaokwenda sambamba na kuleta
mabadiliko kwenye jamii”.Alisema.
No comments :
Post a Comment