Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli katika mkutano wa kimataifa wa Usafirishaji Duniani
utakaofanyika katika mji wa Ashgabat nchini Turkemistan kuanzia tarehe
26-27 Novemba, 2016.
Ajenda kuu ya mkutano huo
ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambao utashirikisha
viongozi mbalimbali utajadili kwa kina maeneo muhimu ya ushirikiano wa
kimataifa kwenye Sekta ya Usafirishaji kwa maendeleo endelevu Duniani.
Aidha katika mkutano huo Waziri
Prof. Mbarawa atapata fursa ya kukutana na wawekezaji mbalimbali Duniani
waliobobea katika sekta ya usafirishaji na kuwashawishi kuwekeza hapa
nchini
No comments :
Post a Comment