Tanga, WAJUMBE 14 wa Kamati ya
Mawasiliano na Ujenzi Baraza la Uwakilishi la Zanzibar wamesema ujio
wa Mradi wa Bomba la Mafuta Tanga litaongeza ajira kwa vijana wakiwemo
Wanzanzibar waishio Tanga.
Wajumbe hao wakiongozwa na
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamza Hassan Juma walitembelea bandari ya
Tanga eneo la upakuzi wa shehena ya mizigo na eneo itakapojengwa bandari
mpya ya Mwambani.
Akizungumza mara baada ya ziara
hiyo, Hassan alisema Serikali ya Zanzibar imejipanga kuimarisha bandari
zake ikiwemo ya Wete na Mkoani Kisiwani Pemba ikiwa ni maandalizi ya
ujio wa Bomba la Mafuta.
Akizungumzia kilio cha
wafanyabiashara na wasafiri wa Pemba na Tanga kwa kutumia usafiri wa
baharini, Hassan alisema kero hiyo Serikali inaitambua na jitihada za
kuwa na meli ya uhakika inafanywa.
Alisema kuna baadhi ya
wafanyabiashara wa Pemba ambao walikuwa wakichukua bidhaa Tanga
wamekatisha na baadhi yao mitaji kufa kutokana na kutokuwepo kwa usafiri
wa uhakika wa baharini.
Awali akizungumza na wajumbe hao
wa Baraza la Wawakilishi, Kaimu Meneja wa Badari Tanga, Henry Arika,
alisema mchakato wa mradi wa bomba la mafuta unaenda kwa kasi na
kuwataka wawekezaji kutoka Zanzibar kuja kuwekeza.
Alisema Tanga ziko fursa nyingi
za uwekezaji na yako maeneo mengi hivyo kupitia ujio wa mradi wa Bomba
la mafuta amewataka wawekezaji wa ndani kuchangamkia.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,
Henry Arika (katikati) akitoa maelezo kwa wajumbe 14 wa Baraza la
Wawakilishi kutoka Zanzibar walipotembelea bandari ya Tanga kujifunza
Afisa Mtekelezaji Mkuu Bandari
ya Tanga, Donald Kaire, akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi wa Zanzibar walipofanya ziara bandari hiyo juzi. Katikati ni
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika.
No comments :
Post a Comment