Gavin Van Wjik
Sehemu ya mitambo ya umeme ya kuzalisha umeme katika kiwanda cha TBL cha Mbeya
Sehemu ya mitambo ya umeme ya kuzalisha umeme katika kiwanda cha TBL cha Mbeya
……………………………………………………………..
Ni kwa kutumia nishati mbadala rafiki kwa mazingira
Mkurugenzi wa Ufundi wa kampuni ya TBL Group,Gavin Wijk,amesema njia kubwa ya kuondoa uchafuzi wa mazingira na hewa kutokana na uzalishaji wa viwandani ni kutumia teknolojia za kisasa ambazo haziathiri mazingira mojawapo ikiwa ni kufanya uzalishaji wa kutumia nishati ya umeme wa jua.
Akiongea
na waandishi jijini Dar es Salaam,Gavin Van Wjik alisema kuwa TBL Group
imejipanga kuhakikisha inaleta teknolojia rafiki kwa mazingira na
tayari imeanza kufanya uzalishaji wa kutumia nishati ya umeme wa jua katika kiwanda chake cha Mbeya.
Alisema umeme huo wa jua utaweza kupunguza tani zipatazo 130 za hewa chafu kwa mwaka na kampuni inao mkakati kuhakikisha teknolojia hii inasambazwa katika viwanda vyote vilivyopo
chini ya kampuni hiyo na alitoa ushauri kwa viwanda vingine vilivyopo
nchini kuangalia uwezekano wa kufanya uzalishaji kwa kutumia teknolojia
rafiki kwa mazingira.
“Moja ya maazimio ya Wakuu wa nchi mbalimbali walipokutana mjini Paris nchini Ufaransa Desemba mwaka jana katika mkutano kuhusiana
na hali ya hewa duniani moja ya ajenda ilikuwa kuangalia uwezekano wa
viwanda kufanya uzalishaji usioathiri mazingira.TBL Group tayari
tumeanza kutekeleza maazimio hayo kwa vitendo na siku zote tutakuwa
mstari wa mbele kulinda mazingira na vyanzo vya maji”.Alisema Gavin
Alisema
uzalishaji wa kutumia nishati mbadala pia kwa kiasi kikubwa
unaipunguzia kampuni gharama kubwa za kufanya uzalishaji wa kutumia
umeme wa gridi ya Taifa na kutolea mfano wa umeme wa jua wa kiwanda cha
Mbeya ambao unazalishwa Kilowati 268,000 kwa saa utaiwezesha kampuni kuokoa kiasi cha milioni 44 za malipo ya ankra za umeme kwa mwaka.
“Umeme
huu wa nishati ya jua tunautumia kwa asilimia 30 ya matumizi ya kiwanda
iwapo tutakuwa na teknolojia ya kuweza kutuwezesha kupata umeme wa
kutosheleza matumizi yote ya kiwanda gharama za uendeshaji zitazidi
kupungua zaidi wakati huo tatizo la uchafuzi wa mazingira kupungua kwa
kiasi kikubwa”.Alisema.
Gavin aliongeza kusema kuwa mbali na TBL kuanza kutumia teknolojia ya umeme wa jua ikiwa ni ya
kwanza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki vilevile katika kiwanda
chake cha Mwanza inafanya uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga na
mashudu ya pamba.”Uzalishaji wa kutumia umeme unaotokana na mashudu ya
pamba na pumba za mpunga unaendelea kupata mafanikio makubwa kwa kupunguza uchafuzi wa mazingira , kuongeza ajira kwenye jamii na kupunguza gharama za uzalishaji”.
Alisema
TBL Group inaunga mkono jitihada za serikali za kuigeuza Tanzania nchi
ya viwanda na itaendelea kushirikiana na wadau wote katika sekta ya
biashara na viwanda ili kuhakikisha ndoto hii inatimia
No comments :
Post a Comment