Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiongoza Wachezaji wa timu ya Taifa ya
mchezo wa kabadi walipowasili jijini Dar es salaam wakitokea nchini
India kwenye mashindano ya mchezo huo uliofanyika hivi karibu nchini
humo .
Wachezaji wa timu ya Taifa ya
mchezo wa kabadi wakiwasili jijini Dar es salaam wakitokea India kwenye
mashindano ya mchezo huo uliofanyika hivi karibu nchini humo ambapo
Tanzania imetolewa kwenye mashindano hayo .
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiongea na waandishi wa habari mara
baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es
salaam wakitokea nchini India kwenye mashindano ya mchezo wa kabadi
uliofanyika hivi karibu nchini humo .
…………………………………………………………….
Na Ally Daud-Maelezo.
SERIKALI imekusudia kuboresha
mazingira rafiki ya biashara nchini ili kuwezesha utashi wa Serikali ya
Awamu ya Tano katika kuifanya Tanzania kuwa nc hi ya uchumi unaoongozwa
na viwanda kama inavyoelekeza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025.
Akizungumza hayo wakati wa
uzinduzi wa kamati ya kuboresha mazingira ya biashara Tanzania jijini
Dar es salaam Waziri wa Viwanda ,Biashara na uwekezaji Charles Mwijge
amesema kuwa Serikali imejidhatiti kuweka mazingira rafiki kwa maendeleo
ya biashara nchini.
“Ili kuweza kufikia malengo ya
Serikali ya Awamu ya Tano katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi
unaoongozwa na viwanda kama inavyoelekeza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya
Mwaka 2025 ni lazima kuboresha mazingira ya biashara ambayo ni rafiki
kwa wawekezaji” alisema Mwijage.
Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa
maboresho ni kusaidia kupata mikopo kwenye mabenki na taasisi za
kifedha zitakazosaidia uwekezaji na uzalishaji wenye tija kwa maendeleo
ya uchumi wa taifa letu.
Waziri Mwijage amesema kuwa
Serikali itahakikisha inaboresha mazingira rafiki ya biashara ili
kufikia lengo kwa kurahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi wa viwanda kwa
wawekezaji wa nje na wa ndani ili kufanya sekta ya viwanda kua endelevu
Zaidi.
Mbali na hayo Waziri Mwijage
amesema kwamba kwa kuwa Serikali imeamua kujenga uchumi wa viwanda basi
itahakikisha inarahisisha suala la uboreshaji wa mazingira rafiki ya
biashara nchini .
Kamati hiyo iliyozinduliwa rasmi
na Waziri Mwijage ina kazi ya kufanya uchambuzi wa kina katika mazingira
ya kufanya biashara nchini na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya
kuboresha mazingira rafiki ya biashara nchini.
No comments :
Post a Comment