Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na uongozi wa kiwanda cha Mt. Meru Millers mara baada ya kufanya ziara
kiwandani hapo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa taarifa kwa Makamu wa
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan juu ya
maendeleo ya kiwanda pamoja na changamoto wanazokutananazo wafanyabiashara
wazawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka kiwanda cha Mt. Meru Miller kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa ufafanuzi juu ya malighafi hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka kiwanda cha Mt. Meru Miller mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akingalia ndoo za plastiki zinazotengenezwa na kampuni ya Mt. Meru Millers kwa ajili ya kuhifadhia mafuta ya kula ,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal.
.....................................................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali
inajipanga kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye viwanda kama
hatua ya kuviwezesha viwanda vingi nchini kuongeza uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa
watanzania.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha baada ya
kutembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Mount Meru Millers ili
kujua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho ili Serikali iweze kuzifanyia
kazi katika kuleta unafuu kwenye uzalishaji wa mafuta ya kupikia nchini.
Makamu wa
Rais amesema mlolongo wa kodi zinazotozwa kwa wamiliki wa viwanda hazina
uratibu mzuri hivyo mkakati ya Serikali wa awamu ya Tano inataka kuweka
utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo ikiwemo kuondoa kodi ambazo ni kero
kwenye viwanda.
Amesisitiza
kuwa Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha viwanda vingi vinajengwa
nchini ambavyo vitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini hali ambayo
itasaidia uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kuuzwa kwenye masoko ya
nje ya nchi na kuliingizia taifa mapato na kuongeza ajira kwa makundi
mbalimbali ya wananchi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ziara ambazo anafanya kwenye viwanda mkoani
Arusha ni kujionea jinsi viwanda hivyo vinavyofanya kazi za uzalishaji na pale
kwenye changamoto zinazokwamisha viwanda hivyo kufanya kazi vizuri ziweze kufanyia
kazi na Serikali.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mount Meru Millers Atul Mittal amesema
kama Serikali itafuta au kuondoa utitiri wa kodi wanazotozwa kwenye Viwanda
hivyo watakuwa na uwezo wa kuongeza maradufu uzalishaji na kutoa ajira nyingi
kwa Watanzania.
Amesema kwa
sasa Kampuni hiyo inafanya kazi kwenye nchi 10 barani Afrika na kwa Tanzania
pekee imeajiri wafanyakazi zaidi ya 1000 ambao wanafanyakazi katika maeneo
mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme
nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Novemba
24, 2016. Alikuwa akitoa ufafanuazi kuhusu masuala muhimu ya TANESCO.
Wengine pichani, kulia ni Meneja wa Vyuo vya TANESCO, Mhandisi Said
Msemo na kushoto ni Kaimu Meneja Uhisano wa Shirika hilo, Leila Muhaji.
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
SERIKALI
kupitia Shirika lake la umeme nchini TANESCO limefanya uwekezaji mkubwa kwenye
miradi mbalimbali ya umeme yenye thamani ya Shilingi Trilioni 5.35, Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba amewaambia waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, leo Novemba 24, 2016.
Akitoa
ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali muhimu ya Shirika hilo, Mhandisi Mramba
alisema, “Katika historia ya sekta ya umeme, haijawahi kutokea uwekezaji mkubwa
kufanyika kwa wakati mmoja kama ilivyo sasa, Miradi yote ya umeme inayoendelea
na ambayo tayari iemtengewa fedha ina thamani ya Shilingi Trilioni 3.85, na
majadiliano kati ya Serikali na Exim Bank ya mradi wa Dar es Salaam-Arusha wa
Shilingi Trilioni 1.5 yakiwa katika hatua za mwisho.” Alifafanua Mhandisi
Mramba.
“
Uwekezaji huu unathibitisha kwamba nia ya Serikali ya awamau ya tano ya
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda sio ya maneno matupu bali inaambatana na
vitendo kwa uwekezaji madhubuti kwenye umeme.” Alisema.
Mhandisi
Mramba alitaja Miradi hiyo mikubwa ya umeme kuwa ni pamoja na ule wa upanuzi wa
Kinyerezi I, Kinyerezi II, mradi wa Backbone, Kenya-Tanzania, TEDAP,
Makambako-Songea, Uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam, City Centre-Dar es
Salaam, Electricity V, Bulyanhulu-Geita, Geita Nyakanazi na Rusumo Power Plant
(T), miradi yote hii ikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi Trilioni 3.85.
Akifafanua
zaidi kuhusu uwekezji huo, Mhandisi Mramba alisema, Miradi yote ambayo thamani
yake imetajwa haihusishi Miradi ya usambazaji umeme Vijijini chini ya mpango wa
REA.
Akizungumzia
utaratibu mpya wa manunuzi,(Procumbent), Mhandisi Mramba alisema, TANESCO
imechukua hatua kadhaa ili kuboresha manunuzi ambapo kuanzia sasa makampuni
yanayomilikiwa na mtu mmoja kuhodhi manunuzi ya Shirika hilo, na kwamba zabuni
zote zilizotangazwa kuanzia mwaka huu wa fedha, haitaruhusiwa kampuni moja kuwa
na mikataba miwili kwa wakati mmoja.
Akifafanua
zaidi alisema, Katika zabuni moja haitaruhusiwa kampuni moja kupewa zaidi ya
Lot 1, “Hii imeanza kusaidia kuondoa ukiritimba katika manunuzi na kuwapa
Watanzania wengi zaidi nafasi pana ya kushiriki katika zabuni za kusambaza
vifaa vya umeme.” Alifafanua Mhandisi Mramba.
Aidha
Mhandisi Mramba alisema, ili kuwezesha Watanzania wengi kushiriki katika uchumi
wa nchi, TANESCO itanunua vifaa vya umeme vinavyozalishwa hapa nchini na
kuachana na mtindo wa kuagiza kutoka nje.
“Mfano
kwa nguzo za umeme tumewapa Sao Hill, ambao watatuuzia nguzo 96,500, na new
Forest watatuuzia nguzo za umeme 9,668, na kwa upande wa Transfoma za umeme,
kandarasi hiyo imepewa kampuni ya TANELEC itakayotuuzia transfoma 1,500”
Alifafanua
Akieleza
zaidi kuhusu ununuzi wa vifaa, Mhandisi Mramba alisema, kampuni ya East Africa
Cables, intarajiwa kupewa kazi ya kusambaza waya na kuongeza kuwa utaratibu huo
pia utatumika kwenye huduma nyingine kama vile Bima, ambapo alisema Shirika
linatarajia kulitumia Shirika la Bima la Taifa, (NIC), kutoa huduma hiyo.
Akizungumzia
kuhusu hali ya umeme, Mhandisi Mramba aliwahakikishia Watanzania kuwa kutokana
na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Shirika hilo katika kuboresha miundombinu ya
umeme, hakutakuwa na mgao wa umeme nchini na ndio maana kwa muda mrefu sasa
hakuna mgao wa umeme.“Mwaka 2015 nchi ilikuwa na mgao wa umeme wa jumla ya
MW300, na maeneo mengine yalikuwa na hali mbaya hususan Mwanza, Arusha na Kilimanjarolakini
kwa sasa hali ya umeme katika mikoa yote na mingine ni nzuri hakuna mgao na
kama ikitokea umeme umekatika ni matatizo ya kiufundi katika eneo dogo na kwa
muda mfupi.” Alisema.
Hata
hivyo alisema Shirika lake linaongeza juhudi za kusambaza umeme kwa watanzania
wengi zaidi kote nchini, kutokana na uwekezaji wa miundombinu unaoendela kila
kona ya nchi.
Mhandisi
Mramba aliwaondoa wasiwasi wananchi kuhusu ombi la Shirika hilo la kuongeza
asilimia 18.9 ya bei ya umeme kuanzia Januari mwakani, kwa kusema ongezeko hilo
halitaathiri watumiji wa kawaida majumbani. “Tunachoomba kutoka kwa Msimamizi
(Regulator), ni kufanya mabadiliko ya kutenganisha watumiaji umeme wa majumbani
na wale wanaotumia kibiashara kama vile mabango ya matangazo, kwani hivi sasa
wote wanalipa gharama sawa na hili si sawa.” Alisema.
Aliwaasa
wananchi kuridhia ongezeko hilo kwani Shirika limo katika jitihada kubwa za kuhakikisha
Wananchi wengi zaidi wanapatiwa umeme kwa kufikisha miundombinu ya umeme kwenye
maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo gharama za kufanya hivyo zimeongezeka.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kushoto), akizunguzma jambo
Wajumbe
wa Kamati ya maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda
ya Kaskazini walipokutana na wanahabri mkoa Kilimanjaro kuzungumzia
tukio la uzinduzi litakalo fanyika kesho Ijumaa katika viwanja vya kituo
kikuu cha Mabasi mjini Moshi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda
ya Kaskazini ,Elizabeth Mushi akizungmza walipkkutana na wanahabari
mkoani Kilimanjaro.
Wajumbe
wa Kamati ya maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili kutoka Mtandao wa
Jinsia wa jeshi la Polisi (TPF Network) , Grace Lyimo (Kushoto) na
Theresia Nyangasa.(Kulia).
Meneja
Programu wa Shirika lisililo la Kiserikali linalojishughulisha na
kupinga ukeketaji (NAFGEM) Honorata Nasuwa akizungumza mbele ya
wanahabri juu ya uzinduzi rasmi wa siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia .
Afisa
Programu wa Shirika linalotoa msaada wa Kisheria
Kilimanjaro-KIWECO,Hilaly Tesha akizungumza wakati wa mkutano wa na
wanahabari kuzungumzia tukio hilo .
Baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa.
Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ,Elina Maro akizungumza katika mkutano huo na wanahabari.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Taasisi
ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) imeshirikiana na kampuni ya
Getenrgy kuandaa mkutano wa Afrika wa Mafuta na Gesi (GETENERGY VTEC
AFRICA 2016) ambao unafanyika nchini kwa siku tatu kuanzia Novemba,
21-23, 2016.
Katika
hotuba yake ya utangulizi, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida
alisema kuwa mkutano huo umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya
mafuta na gesi kutoka nchi mbalimbali Afrika ikiwepo serikali, viwanda,
mashirika ya maendeleo na vyuo ambavyo vinatoa elimu ya mafuta na gesi.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akitoa neno la utangulizi katika Mkutano wa Afrika wa Mafuta na Gesi.
"Malengo
ya mkutano huu ni kuangalia changamoto gani ambazo zinalikabili Bara la
Afrika katika sekta ya mafuta na gesi, kubadilisha ujuzi kwa wataalamu
wa mataifa ambayo yameshiriki na kujadili hatua ya kuchukua ili
kuboresha sekta hii lakini pia utasaidia kukuza ushirikiano baina ya
nchi washiriki,
"Katika
mkutano washiriki wataisaidia Serikali na wadau kuweka mikakati ya
kutekeleza na yenye ufanisi kuhusu sekta ya mafuta na gesi na kama
Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamiii tutaendelea kushirikiana na
wadau kutafuta changamoto zinazokabili sekta na mbinu za kutumia ili
kuyatatua," alisema Dkt. Kida.
Mgeni
rasmi katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania, Mama Samia Suluhu akizungumza umuhimu wa mkutano huo na jinsi
ambavyo unaweza kuwanufaisha Watanzania.
Kwa
upande wa mgeni rasmi katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu alisema, Serikali kwa sasa
inataka kuhakikisha kunakuwapo na wataalamu wengi ili kunapokuwepo na
sehemu ambazo kunapatikana mafuta au gesi waweze kushiriki wenyewe ili
kipato kinachopatikana kiwanufaishe wananchi na Taifa kwa ujumla.
"Nchi
ina akiba nyingi ya gesi na tunategemea kupata mafuta baadae lakini
tunangaalia upande wa wataalamu, tunahitaji kuwa na wataalamu katika
sekta ya mafuta na gesi ili tutakapoanza shughuli ya uchimbaji tayari
tuwe na wataalamu wanaohitajika hapa nchini,
"Huu
ndiyo mchango wa ndani, hatuwezi kufanya sisi pekee lazima tuwe na
wageni lakini pia tuwe na Watanzania wanaotumikia sekta hii na
wanaofaidika na uchimbaji wa hayo mafuta," alisema Mama Samia.
Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akieleza jinsi ambavyo
Serikali imejipanga kuinua sekta na mafuta na gesi ili Watanzania wengi
wanufaike na uwepo wa mafuta na gesi nchini.
Nae
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alisema Serikali
imejipanga kuboresha sekta ya mafuta na gesi kwa kutoa elimu kuhusu
sekta hiyo katika baadhi ya vyuo mbalimbali nchini ili wahitimu
wanapomaliza waweze kuingia moja kwa moja katika sekta hii.
"Tupo
katika orodha ya nchi 20 Afrika ambazo zinafanya vizuri, baada ya miaka
mitano tutakuwa tumepiga hatua na mtaona ni jinsi gani tumefanikiwa,
kwasasa tuna wanafunzi wamehitimu UDOM na tunashirikiana na China na
Uingereza kwahiyo niwahakikishie kuwa tumejipanga," alisema Prof.
Muhongo.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Getenergy, Virginia Baker akitoa taarifa kuhusu kampuni
hiyo, malengo na umuhimu wa kufanyika kwa mikutano hiyo.
Mikutano
ya GETENERGY VTEC kwa mwaka 2016 tayari imeshafanyika katika nchi ya
Mexico na Uingereza na imekuwa ikikutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya
mafuta na gesi ili kujadili jinsi sekta hiyo inaweza kuboreshwa na kuwa
bora zaidi kuliko ilivyo sasa.
Wadau
mbalimbali wa sekta ya mafuta na gesi kutoka mataifa mbalimbali
wakifuatilia mkutano wa mafuta na gesi ambao mgeni rasmi alikuwa ni
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu akipewa
maelekezo kutoka kwa msimamizi wa banda la Chuo cha AGR TRACS kuhusu
masomo yanayotolewa na chuo hicho. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF,
Dk. Tausi Kida.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa
Sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kwenye ukumbi wa Chuo
cha Mipango mjini Dodoma Novemba 23, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira
na Walemavu, Jenista Mhagama na kushoto kwake ni Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza
wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Wafanyakazi (TUKTA)
kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Novemba 23, 2016.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akiwasalimia wajumbe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi, Angela
Kairuki akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi (TUCTA) uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi
wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Novemba 23,2016
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
(TUCTA) , Gratian Mukoba akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Sita wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) uliofunguliwa na Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Novemba 23,2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza
wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Wafanyakazi (TUKTA)
kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Novemba 23, 2016.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Sita
wa Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA) wakiimba wimbo wa Mshikamano kabla
ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Chuo cha
Mipango mjini Dodoma Novemba 23, 2016.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Sita wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) wakimsikilza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipofungua mkutano huo kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini
Dodoma Novemba 23, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA)
na wananchama wa TUCTA baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Sita kwenye
ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Novemba 23, 2016. Kulia kwake ni Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira , Vijana
na Walemavu, Jenista Mhagama na kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Utumishi, Angela Kairuki
Waziri Mkuu akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana
Waziri Mkuu akisalimiana na Rais wa CWT, Gratian Mukoba
No comments :
Post a Comment