Mmiliki wa kampuni ya hanspaul
group of companies Arusha ndugu Hans Paul akiwa anasoma maelezo
mafupi ya mradi walioujenga kwa ajili ya wananchi wa kata ya Engutoto
pamoja na kata ya Moshono
Ndugu Hans Paul katikati akimuonyesha mkuu wa mkoa daraja la zamani ambalo wananchi hao walikuwa wanalitumia
Pia viongozi wa vyama mbalimbali walijitokeza katika uzinduzi huo |
Sehemu ya wafanyakazi wa hanspaul waliouthuria uzinduzi huo
baadhi ya mameneja wa hans paul wakiwa wanafatilia uizinduzi
Mkuu
wa mkoa na mkurugenzi wa hanspaul group of companies Arusha wakikata
utepe kwa ajili ya uhashirikia kuwa daraja limezinduliwa
Mkuu wa mkoa wa Arusha akipita juu ya daraja mara baada ya kulizindua rasmi
huu ndio muonekano wa daraja lililo jengwa na kampuni ya Dharam Singh Hanspaul Group
Jumla
ya zaidi ya shilingi milioni 67.7 zimetolewa na kampuni ya Dharam Singh
Hanspaul inaojishulisha na utengenezaji wa bodi za magari ya utalii
jijini hapa kwa ajili ya ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya
Ongutoto pamoja na kata ya Moshono iliopo ndani ya jiji la Arusha .
Akiongea
wakati wa kukabidhi daraja hilo mara baada ya kukamilika kwa ujenzi
mmiliki wa kampuni hiyo Hans Paul alisema kuwa kampuni yake ipo tayari
kushirikiana na kuunga mkono serikali ya awamu ya tano pamoja na
serikali ya mkoa wa Arusha katika swala zima la kuleta maendeleo na
kusaidia wananchi wa hali ya chini hivyo ndio maana wameamua kuunga
mkono serikali kwa kusaidia shughuli mbalimbali za kijiamii ikiwa ni
pamoja na kujenga daraja
"
sisi kama kampuni ya Dharam singh Hanspaul tunahaidi kushirikiana na
serikali ya awamu ya tano katika kila jambo ili kuweza kuwasaidia
wananchi wanyonge pamoja na wale wa hali ya chini na tupo tayari
kushirikiana na viongozi wa serikali hii bega kwa bega"alisema Hans Paul
Alisema kuwa daraja hilo la
Mto kijenge lilianza kujengwa mwezi Juni na kukamilika Agost 2016 lina
upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani
tatu(3), urefu kwenda juu ni mita 2.2, uimara wa pekee na linaweza
kudumu kwa miaka 50; Ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni
67 .
Aliongeza
kuwa daraja hilo ni ukombozi na msaada kwa wananchi wengi ambao walikua
wakipata adha kubwa ya kuvuka haswa wakati wa mvua kutokana na kukosa
kivuko cha uhakika na kivuko kilichokuwepo awali kiliashiria hali ya
hatari kubwa kwa watoto, wazee, waendesha pikipiki, waenda kwa miguu
wote na zaidi hakuna Gari lililokuwa na uwezo wa kupita hapo.
Paul
aliongeza kuwa mbali na kujenga daraja hilo pia kampuni yake imejenga
madarasa matatu yaliko katika kata ya Engutoto yaliyogarimu kiasi cha
shilingi milioni 50 ikiwa ni njia moja wapo ya kusaidia watoto wa kata
hiyo kukaa darasani na kusoma kwa raha na amaani zaidi .
“pia
mbali na hivyo kampuni hii imeajiri wananchi vijana ambao ni wazawa
zaidi ya 500 ambao vijana hawa wanafanya kazi katika kampuni hizi zangu
tatu tofauti hii ikiwa ni njia moja wapo ya kuweza kusaidia serikali
kutatua tatizo la ajira ambalo linaikamili nchini yetu kwa kipindi hichi
na sitaishia apa kwani pia ninampango wa kuendelea kutoa ajira kwa
vijana wengine “alisema mmiliki wa kampuni hii ya Dharam Singh Hanspaul
Adha
kutokana na kuwa natatizo la kutokuwepo na zahanati katika kata hiyo
pia kampuni hiyo iliweza kuhaidi ofisi ya mkuu wa mkoa kuwa itatoa bati
1000 kwa ajili ya zahanati ambayo itajengwa katika kijiji hicho ili
wakina mama na watoto waweze kutibiwa kwa uharaka na uhakika zaidi .
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa
maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) ambaye amehaidi kujenga viwanja vya
michezo ndani ya kata ya Engutoto na Bw. Jagjit Aggarwal
Na Woinde Shizza,Arusha
WANANCHI kutoka kata ya Engutoto jijini hapa,wanatarajiwa kutimiza ndoto zao za muda mrefu juu ya ukosefu wa viwanja baada ya mfadhili kujitokeza kuwajengea.
Mfadhili huyo Hans Paul kupitia kampini ya Dharam Singh Hanspaul &son ltd alisema hayo mbele ya mkuu wa mkoa Arusha kuwa katika kutimiza adhma ya serikali kusaidia maendeleo ya michezo kwa vijana amejitolea kujenga viwanja viwili vya michezo.
“Viwanja tutakavyojenga ni kwa mpira wa miguu na mpira wa Netiboli na vinatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 30 fedha za kitanzania na tunatarajia kuanza ujenzi huo ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2017,”Alisema Paul.
Alisema kuwa lengo kuu la kujenga viwanja ni katika kuwawezesha vijana wapate muda wa kujihusiha na michezo ili kuepukana na tabia hatarishi ambazo zingeharibu ndoto za maisha yao.
Baahi ya wakazi wa kata hiyo wakizungumzia neema watakayoipata kutoka kwa mfadhili huyo walisema “Ni jambo
la kupongeza kwani vijana wengi wamekuwa hawana mahali pa kufanya
mazoezi na kwa hali hii itasidia sasa kuanza kuona vipaji vya michezo
katika kata hii.” Alisema mmoja wa wakazi hao.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo alisema juhudi
alizozifanya mfadhili huyo katika sekta ya michezo ni jambo la heri
ambalo linatakiwa liwe mfano kwa wadau wengine katika kusaidia kuinua
michezio katika jamii sambamba na kuwa michezo ni moja ya ajira kwa Vijana .
kawaida mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) ambaye amehaidi kujenga viwanja vya michezo ndani ya kata ya Engutoto na Bw. Jagjit Aggarwal
kawaida mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) ambaye amehaidi kujenga viwanja vya michezo ndani ya kata ya Engutoto na Bw. Jagjit Aggarwal
No comments :
Post a Comment