Mnara wa Mamlakaya Bandari Tanzania wa kuongozea meli ulioko Magogoni-Ferry jijini Dar es Salaam
NA K-VIS BLOG
WAKATI serikali ya awaamu ya tano imejikita katika
kujenga utamaduni wa kujitegemea kupitia kulipa kodi stahiki za serikali, bado
kuna vyanzo vingi vya kulipatia taifa letu mapato havijaangaziwa.
Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kujifunza kutoka kwa
wenzetu, ambayo yamekuwa ni sehemu ya kujiingizia mapato,
Nchini Ujerumani kwenye mji wa Berlin, mwaka 1965-1969
ulijengwa mnara wa TV (Berlin TV Tower- Fernsehturm television) wenye urefu wa
mita 368 eneo la shughuli nyingi za
kibiashara na stesheni kuu ya reli, Alexanderplatz. Mnara huu pamoja na
kufanya shughuli nyingine pia ni kivutio kikubwa cha utalii mjini Berlin,
ambapo watu hupanda kwa kutumia lift (elevator), na kufika kileleni ambako unakuwa kwenye
nafasi nzuri ya kuliona jiji la Berlin kwa uzuri kabisa. Na hapaunalipia ili
kufika huko.
Ukienda Dubai nakoni hivyo hivyo, kuna jingo refu
zaidi kwenye mji huo, ambalo pia watalii hupanda juu kabisa ya jingo hilo kwa
malipo, na kujionea mji wa Dubai kwa kutokea juu. Na watu hupishana kwa ajili
ya kupata fursa hiyoya “kutakasa macho”.
Hapa kwetu Dar es Salaam, upo mnara mrefu sana
pembezoni mwa bandari ya Dar es Salaam eneo la Feri-Magogoni, mnara huu ni
mrefu, lakini pia uko kwenye kona nzuri (angle), ambapo unaweza kufanya
shughuli zilizokusudiwa yaani kuongoza meli lakini pia ungweza kutumika kama
chanzo cha mapato cha Mamlaka yaBandari, kwa kuruhusu wananchi na watu wengine
kupanda kwenye kilele cha mnara huo ili kujionea mandhari ya jiji la Dar es
Salaam, ambalo kwa hakika linapendeza sana kutokana na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu.
Sio Watanzania wengi wanaojua jiji lao la Dar es
Salaam likoje, ni wachache sana ambao wanapata fursaya kupanda ndege, na kupita
kwenye maeneo jirani na ukanda wa pwani, wanaweza kujionea ni namna gani jiji
letu linapendeza.
Ni jukumu letu sisi watanzania kujiuza wenyewe badala
ya kusubiri ushauri kutoka nje.
Nakumbuka zamani wakati nikiwa Teenager, yaani kijana barubaru, wakati wa sikukuu, sehemu pekee
ambayo vijana wadogo na hata wakubwa wkati mwingine, tulifurika uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ili tu tuweze kujionea “midege” ikitua pale. Na
wakati huo watuwaliruhusiwa kutembelea eneo hilo kwa juu. Ingawa hapakuwa na
malipo yoyote ukiachilia mbali nauli yako ya daladala kukutoa utokako na
kukurudisha.
Najua yanaweza kusemwa kuwa sababu za kiusalama maeneo
hayo hayataruhusiwa, lakini mbona hao hao wanaotuonya tuwe makini na masuala ya
kiusalama wanaruhusuwananchi wao lakini pia na wasiowananchi kutembelea maeneo
muhimu ya nchi ili kujifunza na kuona maajabu, mfano ukienda pale Washington DC
nchini Marekani, watu huruhusiwa walau kukaribia Ikulu ya nchi hiyo yaani White House, ikiwa ni pamoja na kupiga picha
za kumbukumbu.
Sio hapo tu hata pale Capital Hill, kwenye bunge la
Marekani, nako watu rukhsa kutembelea na wanalipia ada (fee) kidogo, maana
utakuta kuna watu wenye kujua historia ya jingo hilo na hutoa elimu kwa
wanaotembelea hapo.
Kwa kufanya hivyo unakuwa sio tu serikali inajiongezea
kipato, lakini pia unawapa fursa wananchi kufaidi “kodi’ zao walau kwa
kusafisha macho kwa kuotembelea na kuona wenywe badala ya kusubiri picha
magazetini/TV na mitandaoni.
Kwa wale wanaojua jingo letu la bunge pale Dodoma,
watakubaliana na mimi kuwa, kila aliyepata fursa ya kutembelea jingo lile, basi
hupenda kupiga picha kwenye eneo hilo na huwa watu wanafurahia kwelikweli,
lakini sio wote wanaruhusiwa kwanza hadi upenye hapo ni mbinde kweli kweli.
Lakini ungewekwa utaratibu wa wazi na wa kawaida kwa
watu kutembelea eneo hilo na hata kwa kulipia ingweza kulipatia kipato cha
ziada Bunge letu.
Jambo la msingi kama ni hofu ya usalama, yanaweza
kuwekwa masharti na wana usalama wakachukuanafasi yaoya kuhakikisha usalama
unazingatiwa lakini tusiache mapato yakipita kwa hofu ambayo sidhani kama ipo
kwa mazingira ya sasa ambapo kuna kitu inaitwa “Google earth” inayompa uwezo mtu kuona kitu anachokitaka tena
akiwa nyumbani kwake au kiganjani kwake.
Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililoko Makao Makuu ya Nchi, mjini dodoma
Mnara wa TV ulioko Alexanderplatz mjini Berlin Ujerumani
Watalii na wananchi wakitembelea Ikulu ya Marekani, White House
Watalii na wananchi wakipita kwa nje kwenye jengola bunge la Marekani, (Capital Hill)
Watalii na wananchi wakipita kwa ndani kwenye jengola bunge la Marekani, (Capital Hill
No comments :
Post a Comment