Kutoka
kushoto ni Ibrahim Samuel- Meneja Uhusiano- Mikopo ya Nyumba, Wasia
Mushi- Naibu Mkurugenzi Benki ya Afrika Tanzania (BOA), na Muganyizi
Bisheko- Meneja Masoko Utafiti na Maendeleo wakiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani).
Kutoka
kushoto ni Beatrice Mirigo- Marketing executive, Ibrahim Samuel- Meneja
Uhusiano- Mikopo ya Nyumba, na Wasia Mushi- Naibu Mkurugenzi Benki ya
Afrika Tanzania (BOA) wakiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).
BANK OF AFRICA- TANZANIA
leo imezindua aina mpya ya mkopo wa ujenzi wa nyumba unaoitwa ‘WEZESHA’
ambapo mtu anaweza kukopa kiasi cha shilingi milioni 40 hadi 500 kwa
mrejesho wa miaka hadi 25 bila utaratibu wa kutoa malipo yoyote ya
awali.
Akizungumzia progamu
hiyo, Naibu Mkurugenzi wa BANK OF AFRICA- TANZANIA bwana Wasia Mushi
alisema, ‘programu hii ya mkopo wa ujenzi wa makazi mapya unawapa uwezo
wateja wetu kubuni nyumba zao kadiri wanavyopenda, kulingana na mahitaji
yao na ndani ya bajeti zao. Kwa kiwango kidogo kabisa cha riba na
katika viwango vya punguzo, Bank ya Afrika pia imetengeneza mazingira
rafiki na kuondoa usumbufu kwa mteja pindi anapohitaji mkopo huu’
Aidha, huduma ya mkopo
ya ‘Wezesha’ inapatikana kwa watu wote wenye mishahara katika sekta za
umma na binafsi, na kwa kutoa muda wa miaka 25 ya kulipa deni, mkopaji
atapata uhuru zaidi pindi atakapochukua mkopo.
Mpango wa huu wa
‘Wezesha’ kujenga makazi unalenga kutoa suluhu kwa changamoto za makazi
zinazowakabili watanzania wengi ambao kwa mazingira ya kawaida hutumia
zaidi ya miaka 10-15 kujenga nyumba ya kawaida ya kuishi.
Fursa hii ya kutatua
changamoto ya makazi kwa watanzania wengi, inaendana na ongezeko kubwa
la watu kupata ardhi iliyopimwa, hivyo kuwapa watu nafasi ya kujenga
nyumba wanazozitaka kwa masharti nafuu na rahisi ambapo kwa kuanzia
mteja atatakiwa kuwa na kiwanja ambacho nyumba hiyo itajengwa.
Kwa mujibu wa takwimu,
Tanzania ina uhaba wa nyumba kwa ajili ya makazi zaidi ya 3,000,000.
Huku kukiwa na ongezeko la uhitaji huo kwa zaidi ya asilimia 1 kila
mwezi.
Muganyizi Bisheko,
Meneja Masoko Utafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA-TANZANIA aliongeza
kuwa, ‘Benki inatoa asilimia 100 ya ufadhili wa ujenzi ili watu wengi
waweze kuumudu mkopo. Mara nyingi, hasa kwa mtu anayeanza maisha,
kujiwekea akiba na kupata kiwango cha kulipia gharama za ujenzi wa
makazi ni jambo gumu sana. Jambo hilo liliwezekana kwa wale wenye kipato
kikubwa na endelevu, lakini kwa sasa, na kwa uwepo wa WEZESHA, si jambo
gumu tena la kuchelewesha ndoto zako za kumiliki makazi ya kuishi, kwa
kuweka akiba kwa miaka 2-5’
Aliongeza kuwa, ‘Mara
mteja wetu anapopata mkopo wa makazi, yeye ndiye atachagua mkandarasi wa
kujenga nyumba yake miongoni mwa makandarasi waliochaguliwa na BANK OF
AFRICA- TANZANIA. Mkopo utatolewa kulingana na hatua za ujenzi, kama
vile msingi, boma, paa, na umaliziaji. Na fedha hizo zitapelekwa kwenye
akaunti ya Kandarasi anayejenga iliyofunguliwa kwenye Benki ya
Afrika.Baada ya kukamilisha ujenzi, ripoti ya mkaguzi wa ubora
itakabidhiwa kabla ya fedha za hatua nyingine ya mkopo kutolewa’
Kwa mara ya kwanza BANK
OF AFRICA- TANZANIA ilizindua mkopo wa nyumba mwaka 2011 ambao ulikuwa
unajumuisha mkopo wa ununuzi wa nyumba pamoja na uboreshaji wa nyumba.
Toka mkopo ulipoanza kutolewa zaidi ya shilingi bilioni 10
zimeshatolewa.
Pamoja na mikopo ya
nyumba, BANK OF AFRICA- TANZANIA pia imekuwa ikitoa mikopo kwa
wakandarasi wa ujenzi ili kuongeza upatikanaji wa nyumba bora za makazi
na wakati huo huo wakiwezesha watu wa kawaida kuzinunua nyumba hizo.
No comments :
Post a Comment