SERIKALI
imeombwa kutengeneza bajeti ya kusaidia taasisi mbalimbali
zinazojishughulisha na kusaidia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
ikiwa ndio njia ya kuhakikisha huduma kwa waathirika hao zinaendelea
kuimarika.
Imeelezwa
kuwa ingawa serikali ndiyo inayotoa dawa za kufubaza makali ya UKIMWI
ARVs, haitengenezi bajeti kwa ajili ya wafanyakazi wanaohudumia
waathirika kisaikolojia na kitiba.
Hoja
hiyo imetolewa na Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for
People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA) Jovin Riziki wakati
akijibu maswali katika mkutano na ujumbe wa nchi za jumuiya ya NORDIC
waliotembelea makao makuu ya PASADA yaliyopo Chang’ombe, Temeke Dare s
salaam kuangalia miradi mbalimbali ya kijamii inayofadhiliwa na UNICEF.
Nchi za Jumuiya ya Nordic ni wafadhili wakubwa wa miradi inayoendeshwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Meneja
mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es
Salaam Archdiocese (PASADA) Jovin Riziki (kushoto) akitoa maelezo kwa
sehemu ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) katika chumba cha
kuhifadhia kumbukumbu za wagonjwa ulipotembelea kwenye kituo hicho cha
PASADA jijini Dar es Salaam. Kulia ni kiongozi wa ushirikiano wa
kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders
Rönquist.(Habari picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Akijibu
swali nini ambacho atataka kumweleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikutana naye, Riziki
alisema kwamba angelipenda kuona serikali inawajibika kusaidia huduma
katika taasisi mbalimbali zinazoigusa jamii zinaendelea kutolewa.
Alisema
asasi zinazosaidia waathirika wa UKIMWI kama hiyo ya PASADA hutegemea
asilimia 100 misaada ya nchi na wafadhili wa kigeni ambapo miradi
ikimalizika mara nyingi waliokuwa wanahudumiwa hukosa mahali pa kupata
misaada iliyokuwa inawawezesha kuendelea kuishi kiutu kwa kuwa na siha
njema na kufanya shughuli za kiuchumi.
Meneja
mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es
Salaam Archdiocese (PASADA), Jovin Riziki (kushoto) na ujumbe kutoka
nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa mtoa huduma katika kitengo
cha dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKIMWI ARV's ulipotembelea
kwenye kituo hicho cha PASADA jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuna changamoto kubwa kuhudumia wagonjwa zaidi ya elfu 21 wengine
wakiwa kufani majumbani bila kuwa na mtaji wa kutosha hasa malipo kwa
watoa huduma ambao ni wataalamu.
“Ipo
haja ya serikali kuchangia kazi hii ya kibinadamu hasa fedha kwa ajili
ya kulipa wataalamu na kuendeleza miradi ambayo inasaidia jamii moja kwa
moja” alisema huku akiongeza kwamba kwa sasa mathalani wanaendelea
kufanya mazungumzo na watu mbalimbali kuendeleza mradi uliokuwa
ukisaidiwa na USAID.
Alisema
Septemba mwaka huu USAID wamemaliza mchango wao wa mradi muhimu ambao
ndani yake ulikuwa unawasaidia waathirika katika elimu, tiba na pia
kiuchumi.
Ujumbe
huo ukiwa kwenye mazungumzo na vijana wanaoishi na VVU ambao wamepata
mafunzo ya ujasiriamali yaliyowawezesha kujiajiri kwa kufanya biashara
ndogo ndogo zinazowapatia kipato cha kusaidia familia zao na mahitaji
yao madogo madogo.
Alisema
mara nyingi kunapoendeshwa mradi ambao ndani yake watu wanawezeshwa
kiuchumi hujitokeza kwa wingi na hivyo kama serikali ikitenga bajeti
maana yake watu hao watafika kupata elimu na pia kufufua matumaini ya
maisha kwa kuwezeshwa kiuchumi.
PASADA
iliyoanza Agosti 1992 wakati kundi dogo la watu wanaoishi na virusi vya
UKIMWI kujikusanya ili kupata msaada wa pamoja sasa hivi ina wateja
36,000, ikitoa huduma za upimaji kwa watu 10,000 kila mwezi.
Aidha
PASADA ambayo imekuwa ikikua ikitegemea fedha za wahisani imekuwa
ikiwafikia watu walio majumbani ambao hawawezi na waliokufani kuwapatia
huduma za kibinadamu.
Ujumbe
kutoka nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) wakipata maelezo nje ya eneo
la vipimo katika kituo cha PASADA.
Ingawa
PASADA ipo chini ya kanisa katoliki huduma zake hupatikana kwa kila
mwananchi bila ubaguzi na huendesha pia huduma za elimu kuhusu afya ya
uzazi, ujana na maradhi ya UKIMWI.
Sehemu kubwa ya elimu ni kuondoa unyanyapaa na kuhimiza wananchi kupima afya zao. Aidha elimu imelenga watu kubadilika tabia.
Ikiwa
na watu wazima 3000 wanaotumia dawa na watoto 600, PASADA imesema
kwamba bado inakabiliwa na changamoto kubwa hasa pale ambapo wahisani
wanapojitoa kusaidia miradi iliyopo ya elimu na kiuchumi.
Aidha
PASADA imekuwa ikipambana kwa kusaidiana na wadau wengine kuhakikisha
kwamba haki za msingi za wenye virusi vya UKIMWI hazikiukwi.
Meneja
mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es
Salaam Archdiocese (PASADA), Jovin Riziki akiongoza ujumbe kutoka nchi
za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
pamoja na mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili
kulia) kutembelea vitengo mbalimbali vinavyotoa huduma kituo cha PASADA
jijini Dar es Salaam.
Ikiwa
imefanikiwa kupunguza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa
asilimia 97, huku ikiwa imefikia asilimia 4 ya waathirika nchini na kwa
mikoa ya Dar es salaam na Pwani asilimia 30, PASADA ikiwa na wafanyakazi
140 inahitaji sana uhakika wa bajeti na serikali ndiyo inayoweza kutoa
kwa kuwa kazi inayofanywa na serikali kupitia vituo vya umma ndiyo
inafanywa na PASADA.
Ujumbe
huo wa NORDIC ambao ulikujwa na wenyeji wao Mashirika ya Umoja wa
Mataifa ulielezea kuridhishwa kwake na kazi inayofanywa na PASADA na
kusema ipo haja kwa wadau kushirikiana kurejesha heshima ya binadamu na
kufanya serikali kuwajibika kwa watu wake.
Naye
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye ndiye mwenyeji wa
ujumbe huo unaopita katika miradi mbalimbali serikalini na hata katika
taasisi binafsi, Alvaro Rodriguez, alisema kuna changamoto nyingi katika
kusaidia wananchi katika maradhi yanawasibu kwa sababu ni kazi ya
kibinadamu zaidi na wala si ya kimaendeleo.
Ziara
ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika
ya Umoja wa Mataifa ikiendelea kutembelea vitengo mbalimbali vinavyotoa
huduma za afya kwa watu wanaoishi na VVU kituo cha PASADA jijini Dar es
Salaam.
Alisema
hata hivyo ili kuwa na haki sawa mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa
yakisaidia kupatikana kwa haki za maisha kwa kusaidia mambo kadhaa
ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moja na wagonjwa lakini yakiwa na
mchango mkubwa katika afya na shughuli za uzalishaji mali.
Alisema
amefurahishwa na ziara ya ujumbe huo wa Nordic ambao ni wafadhili
wakubwa wa miradi mbalimbali yenye lengo la kuwezesha uwajibikaji na
utawala bora nchini ikiwemo misaada ya kibinadamu.
Alisema
ni kazi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa kushawishi mabadiliko ya
kitamaduni ili kujiweka sawa katika shughuli za maendeleo.
Ujumbe
kutoka nchi za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika ya Umoja
wa Mataifa ukiwa katika eneo maalum lililotengwa na kituo cha PASADA kwa
ajili ya watoto kufanya michezo mbalimbali walipofanya ziara kituoni
hapo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akibadilishana mawazo na
kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden
(SIDA), Anders Rönquist wakati wa ziara ya kutembelea vitengo mbalimbali
katika kituo kinachohudumia watu wanaoishi na VVU, PASADA jijini Dar es
Salaam.
Meneja
mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es
Salaam Archdiocese (PASADA), Jovin Riziki akitoa historia fupi ya kituo
hicho pamoja na changamoto zinazowakabili katika kuhudumia watu
wanaoishi na VVU nchini kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana
watalaam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa ulipotembelea kituo hicho.
Sehemu ya ujumbe huo ukimsikiliza Bwana Jovin Riziki.
Kiongozi
wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA),
Anders Rönquist akifafanua jambo wakati wa kutoa mrejesho baada ya ziara
ya kutembelea vitengo mbalimbali katika kituo cha PASADA jijini Dar es
Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa neno la shukrani kwa uongozi
wa PASADA baada ya ziara ya kutembelea kituo hicho na kujionea
changamoto zinazowakabili.
No comments :
Post a Comment