Monday, October 31, 2016

Miji yote Tanzania kupata mtandao wa 4G wa kampuni ya Zantel

pet1
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Benoit Janin  (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mtandao wa  4G ambapo sasa miji yote nchini itafikiwa na huduma hiyo.  Kushoto ni Meneja Uendeshaji Mtandao, Ahmed Hassan Abdallah na Meneja Mauzo, Herbet Louis.
pet2
Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Hebert  Louis (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mtandao wa  4G ambapo sasa miji yote nchini itafikiwa na huduma hiyo.  Kushoto ni Meneja Uendeshaji Mtandao, Ahmed Hassan Abdallah na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin.
pet3
Meneja Uendeshaji Mtandao wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Ahmed Hassan Abdallah (wa pili kushoto),  akiwaonyesha waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, jinsi ya kurekebisha simu na kuwa katika mpangilio wa automatiki  wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mtandao wa  4G ambapo sasa miji yote nchini itafikiwa na huduma hiyo.  Kushoto kwake ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Meneja Mauzo, Herbet Louis.
pet4
Baadhi ya waandishi  kutoka vyombo mbalimbali vya habari walihudhuria uzinduzi huo. 
……………………………………………………..
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
 Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, imetangaza mabadiliko makubwa ya kiteknolojia kwa wateja wake ili kuendana na kasi ya ukuaji wa matumizi ya mtandao ya Intaneti.     Akiongea na waandishi  Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Benoit Janin, amesema kuwa Zantel imekuwa katika uboreshaji wa huduma zake kwa awamu na kwamba sasa wateja wa kampuni hiyo watafurahia huduma za kasi ya intaneti ya 4G ambayo itapatikana kwa zaidi ya 60% ya maeneo yote ambako huduma za kampuni hiyo zimefika.
  “Tangu tulipoanza huduma zetu,tumekua tukitoa huduma kwa kiwango bora na cha hali ya juu hususani katika huduma za intaneti kwa wateja wetu  tena kwa gharama nafuu kwa watumiaji hapa nchini Tanzania”alisema Janin.
  Zantel imetangaza kuwa hadi kufikia siku ya Jumapili tar 30 Octoba mwaka huu wateja wa kampuni hiyo wanatakiwa wawe wameziseti simu zao moja kwa moja “automatic” ili waweze kutumia huduma za 4G bila ya usumbufu wowote.
.Kwa upande wa Mkuu wa kitengo cha mauzo Herbert Luis,amesema kuwa wateja wa kampuni hiyo wanaweza kupata huduma hizo kwa nafuu na kwa urahisi baada ya kuboreshwa na kuwa Zantel wameamua kuwa wapya katika utumiaji wa huduma zake.
Aidha amezitaja  changamoto zinazolikabili soko la intanet nchini,amesema kuwa wamefanya utafiti wa kutosha na kujiridhisha kuwa mtandao wao utakuwa bora na huduma za uhakika kwa wateja wao.
  “Tumejitahidi kufanya marekebisho makubwa na sasa tuna uhakika kwamba wateja wetu wanaweza kufurahia huduma zetu bila ya wasiwasi na pale wengine wanapokwama basi sisi tumepafanyia kazi ili kuonyesha utofauti wetu na wengine kama ilivyo siku zote” Alifafanua Louis
  Zantel wamekuwa katika hatua za uboreshaji wa huduma zao na sasa wametangaza rasmi kuanza kutoa huduma ya 4G kwa wateja wao huku kampuni hiyo ikiwataka wateja kupiga namba 100 ili kupata maelezo sahihi ya namna ya kupata huduma ya 4G kwenye simu zao pale tu wanaposhindwa kufanya hivyo

No comments :

Post a Comment