Monday, October 31, 2016

MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHANDISI MATHEW MTIGUMWE AKUTANA NA WADAU WA ZAO LA PAMBA KUWEKA MIKAKATI MIPYA



Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe akifungua Mkutano wa wadau wa pamba wenye dhamira ya kujadili maendeleo ya kilimo cha zao la hilo katika mkoa wa Singida, Oktoba 31, 2016.
 Wadaau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini Mkutano wa kujadili namna bora ya kuimarisha kilimo cha zao hilo katika Mkoa wa Singida
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa pamba Mkoa wa Singida
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe Elias Choro Tarimo akisisitiza jambo wakati wa Mkutano huo
 Moja ya wakulima wa Kilimo cha pamba Wilayani Ikungi Timoth S. Nkulu akimuomba Mkuu wa Wilaya kuzisimamia Wilaya zote kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa uzalishaji wa kilimo hicho.
 Wadau wa kilimo cha pamba wakihakiki maazimio waliyoyapitisha


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa kwenye zungumza na Rais wa Taasisi ya Mashirikiano ya Kimataifaya Japan(JICA) Bw.Yasushi Kanzaki alipofika Ikulu Mjini Unguja leo Oktoba 31, 2016. (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)





NA MWANDISHI WETU
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90 kuanzia leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kukata rufaa kwa njia ya mtandao ikiwa hawajaridhsihwa na matokeo ya upangaji uliotangazwa hivi karibuni.
Serikali imetenga Tshs 483 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo kwa jumla wanafunzi 119,012 – kati yao, wanafunzi 93,295 ni wanaondelea na masomo na wanafunzi 25,717 ni wa mwaka wa kwanza. Hadi sasa, jumla ya wanafunzi 20,183 wa mwaka wa kwanza wameshapata mikopo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, Bodi imeanza kupokea rufaa hizo kwa njia ya mtandao (Online Loan Application and Management System) kuanzia leo (Oktoba 31, 2016) hadi Januari 31, 2017.
“Wanachotakiwa kufanya wanafunzi ni kulipa Tshs 10,000.00 kwa njia ya M-Pesa na kuingia katika mtandao wetu wa http://olas.heslb.go.tz na kujaza fomu, kuichapa na kuiwasilisha kwa Afisa Mikopo wa chuo chake ambaye atawasilisha kwetu fomu zote za chuo chake kwa barua kwa ajili ya sisi kuzifanyia kazi,” amesema Bw. Badru.
Bw. Badru, katika taarifa yake inayopatikana pia katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) ameongeza kuwa Bodi haitapokea wala kuzifanyia kazi fomu za rufaa ambazo zitawasilishwa Bodi na wanafunzi bila kupitia kwa maaifisa mikopo wa vyuo vyao.

No comments :

Post a Comment