Friday, September 9, 2016

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MA- RAS





Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga (wa pili kulia) akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Karuta Manispaa ya Kigoma Ujiji baada ya kupokea madawati 185 kutoka kwa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo yaliyotolewa kwa shule tano za msingi mkoani Kigoma.
Meneja wa kanda ya ziwa wa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo Kamara Kalembo (kulia) akikabidhi kwa Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga (kushoto) sehemu ya madawati 185 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa shule tano za msingi mkoani Kigoma.
Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga akikabidhi madawati 50 kwa Mwalim Mkuu wa shule ya msingi Karuta Manispaa ya Kigoma Ujiji Therezia Edward ikiwa ni sehemu ya madawati 185 yaliyotolewa na kampuni simu ya mkononi ya tigo  kwa shule tano za msingi mkoani Kigoma
Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Karuta Athuman Juma (katikati) akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo ambayo ilitoa madawati 50 kwa shule hiyo ili kukabili upungufu wa madawati unaoikabili shule hiyo.




NA MWANDISHI WETU – DODOMA.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameliagiza Baraza la Famasia nchini kuanza kazi ya kuhakiki vyeti vya wauza dawa (wafamasia) katika maeneo mbalimbali nchini ili kudhibiti na kuwaondoa wauza dawa wasio na sifa ya kufanya kazi  hiyo kwenye maduka ya dawa.
 Pia ameligiza Baraza hilo kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kuwafutia usajili wafamasia wanaokiuka kanuni na taratibu za Baraza hilo ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya upotevu wa dawa na uuzaji wa dawa  na vifaa Tiba vya Serikali.
Mhe.Ummy alitoa maagizo hayo mjini Dodoma katika Kikao Chake cha kwanza na Bodi ya Baraza la Wafamasia nchini ambapo pamoja na mambo mengine alikemea utaratibu ulojitokeza wa kutaka kuifanya biashara ya dawa kuwa sawa na biashara nyingine za kawaida za maduka ya kuuza nguo jambo ambalo halikubaliki.
 “Biashara ya maduka ya dawa lazima iheshimiwe, lazima ianzishwe kwa kufuata taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na watu wanaoajiliwa kuhudumia maduka ya dawa kuwa na sifa zinazotakiwa, kazi ya kuuza dawa za binadamu sio sawa na biashara ya kuuza nguo au viatu”, alisema Mhe Ummy.
Ameliagiza  Baraza hilo kufanya operesheni nchi nzima  kukagua maduka yote ya dawa kubaini mapungufu yaliyopo kisha kuchukua hatua kali dhidi ya wale wataogundulika kufanya biashara hiyo bila kufuata taratibu na kuongeza kuwa baraza hilo ni lazima liendelee kupambana na watoa dawa wasio na sifa  na wale wasio waaminifu wanaotengeneza vyeti bandia vya Wataalam wa Famasi.
Pia ametoa maelekezo kwa baraza hilo  kuangalia suala la mgongano wa maslahi hasa pale ambapo Mfamasia wa Wilaya anatuhumiwa kumiliki maduka ya Dawa mawili hadi matatu ndani ya Halmashauri anayofanyia kazi.
“Ni lazima suala hili tulitafutue suluhish nimefanya ziara mikoani jambo hili nimelikuta, mimi sielewi na Wananchi wengi hawaelewi pale Mfamasia wa Wilaya anapokua na maduka ya dawa hadi matatu  na muda wote yana dawa wakati dawa hizo hizo hazipatikani katika vituo na Hospitali za Serikal, Kwa nini wananchi wasiwe na hisia kuwa dawa zile ni za Serikali? Baraza nileteeni mapendekezo ya kutatua hili. Alisisitiza Mhe Ummy.
Aidha,  ameliagiza Baraza hilo kuweka msukumo wa pekee kwenye masuala ya kuboresha mafunzo na elimu ili nchi iwe na wanataaluma wenye uwezo wa utendaji wa kiwango cha hali ya juu katika nchi yetu.
Akitoa taarifa ya Utendaji Msajili wa Baraza la Famasia Bi.Elizabeth Shekalaghe alieleza kuwa zipo changamoto wànazokumbana nazo katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo maduka mengi ya kuuza dawa kuendesha biashara hiyo bila ya kuwa na vibali vya biashaa pia kuwepo kwa wauza dawa wasio na sifa ya kufanya shuguli hiyo.
Pia alieleza mikakati iliyowekwa na barza hilo ili kuhakisha changamoto zilizopo zinapatiwa ufumbuzi ili kuhakikisha huduma za uuzaji dawa zinafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu ili kuhakikisha unora wa huduma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Bàraza là Famasia, Legu Ramadhani Mhangwa, amesema kuwa Baraza hilo limekuwa likifanya kazi zake  kwa kuzingatia sheria ili kufikia malengo liliyojiwekea na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo waliyopewa na Mhe Waziri pia kutatua changamoto ya  uwepo wa vyuo binafsi vinavyofundisha taaluma ya famasi kutokidhi viwango pamoja na nia ya serikali ya kuongeza idadi ya wataalamu wa kada za dawa nchini. 
Pia Baraza hilo limeahidi kushughulikia uhaba wa wakufunzi mahususi katika vyuo vinavyofundisha kada za famasi katika ngazi ya cheti na diploma.
Kuhusu mgongano wa maslahi kwa watumishi wakiwemo watendaji wa Halmashauri na wale wanaosimamia na kutekeleza kazi za baraza katika ngazi za mikoa na halmashauri, Mwenyekiti huyo ameahidi kuwa Baraza litahakikisha linasimamia kikamilifu Kanuni za Maadili na Miiko ya Kitaalamu za 2015 ili kutatua changamoto hizo iliwemo upotevu wa dawa za Serikali.



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha bunge kilichoingia siku ya 4, mkutano wa 4 bunge la 11 leo Septemba 9, 2016 Mjini Dodoma.


Waziri wa Habari, Utaamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akiwaeleza jambo Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa (Katikati)na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene wakati wa kikao cha bunge leo Mjini Dodoma.


Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiwaeleza wabunge mipango ya serikali kuendelea kushughulikia changamoto za nishati ya umeme nchini hasa katika maeneo ya Lindi na Mtwara


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu swali wakati wa kikao cha bunge na kuahidi kuwa serikali kuendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali nchini ikiwemo upatikanaji wa madawa na vifaa tiba.

Baadhi ya Wabunge wakiingia katika ukumbi wa bunge mapema leo.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali kwa wabunge ambapo alisema kuwa Serikali inafanya kila jitihada ya kuwaongezea uwezo katika watendaji wake ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia nchini.
 (PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)



Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles Tizeba akieleza bungeni leo kuhusu hali ya chakula nchini na kuwahakikishia watanzania kuwa nchi  ina  utoshelevu wa chakula kwa zaidi ya asilimia 123 kwa mazao ya nafaka na 140.
go02
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe Akipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa darasa la saba mara baada ya wanafunzi hao kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi katika shule ya Chanika wilayani Handeni.
go1
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe Akifurahia wanafunzi wa darasa la saba mara baada ya kuzungumza nao jambo alikutana nao waliokuwa walipomaliza kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi katika shule ya Chanika wilayani Handeni mkoani Tanga.
Wanafunzi hao wamemwambia Mkuu wa wilaya Mh. Godwin Gondwe kufikisha salamu zao kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli, wakimshukuru kwa kuwezesha elimu ya Msingi mpaka Sekondari kuwa bure , kwani itarahisha wanafunzi wengi ambao wazazi wao hawana uwezo kupata elimu. Wameongeza kuwa "Mtihani ulikuwa mzuri hivyo watafauru kwa kishindo".
go2
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chanika wilayani Handeni wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza elimu ya Msingi


Sheikh Mohammed Suleiman akisoma Quran kabla ya Uzinduzi wa Baraza la Vijana kwa Shehia Tatu za Unguja Ukuu Kaebona, Unguja Ukuu Kaepwani na Unguja Ukuu Tindini uliofanyika katika viwanja vya mpira Idumu Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said akisalimiana na Sheikh Mohammed Suleiman baada ya kusoma quran wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana Unguja Ukuu Zanzibar.
Vijana wa Shehia za Unguja Ukuu Kaepwani, Unguja Ukuu Kaebona na Unguja Ukuu Tindini wakifuatilia Uzinduzi huo wa Mabaraza yao.
Vijana wa Shehia za Unguja Ukuu wakisoma Utenzi wa Uzinduzi wa Mabaraza yao ya Vijana katika Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Mhe Simai Mohammed Said, Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Mhe Mashavu Sukwa wakisikiliza utenzi wakati wa uzinduzi huo. 
Msanii wa Gogoti Mussa akionesha umahiri wao wakati wa uzinduzi huo.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed SDaid akionesha dhana ya ushupavu na moyo wa ujasiri wa kucheza na chatu wakati wa Uzinduzi wa Mabaraza la Vijana wa Jimbo la Tunguu Shehia za Unguja Ukuu Kaepwani, Unguja Ukuu Kaebona na Unguja Ukuu Tindini uliofanyika katika viwanja vya Idumu Unguka Ukuu leo jioni..
Vijana wa Jimbo la Tunguu wakimpiga picha Mwakilishi wao wakati akicheza na Chatu katika hafla ya Uzinduzi wa Baraza la Vijana leo jioni katika viwanja vya Idumu Unguja Ukuu Zanzibar Wilaya ya Kati.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said akimsalimia Msanii Mussa Nyoka baada ya kutowa burudani wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Baraza la Vijana la Jimbo hilo. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akiwa na simu wakati Mhe Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Anayeshughulikia Muungano Mhe. Januhuri Makamba akiongea na Wananchi akiwa Mjini Dodoma alikuwa ahudhuria uzinduzi huo wa Mabaraza la Vijana wa Shehia za Unguja Ukuu Zanzibar na kutoa ahadi ya kuchangia shilingi milioni tatu kwa Shehia hizo Tatu za Unguja Ukuu Kaepwani. Unguja Ukuu Kaebona na Unguja Ukuu Tindini.
Vijana wa Shehia za Unguja Ukuu wakimsikiliza Mhe Januari Makamba akizungumza na Wananchi wa Shehia hizo kupitia simu ya mkononi akiwa Mjini Dodoma akihudhuria Kikao cha Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kiongozi wa Mabaraza ya Vijana wa Unguja Ukuu akisoma risala ya Vijana wa Mabaraza ya Unguja Ukuu wakati wa uzinduzi huo. uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Idumu Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akihutubia Vijana wa Shehia za Unguja Ukuu Zanzibar wakati wa Uzinduzi wa Mabaraza hayo uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Idumu Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja leo jioni.

Wazee wa Unguja Ukuu wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said akizindua Mabaraza ya Vijana wa Jimbo lake uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya mpira vya Idumu Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu akihutubia wakati wa Uzinduzi huo wa Baraza la Vijana Unguja Ukuu Zanzibar.
Vijana wa Shehia za Ungujav Ukuu Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Mwakilishi wao Mhe. Simai Mohammed Said akiwahutubia. 
Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Mhe Mashavu Sukwa akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Baraza la Vijana Shehia za Unguja Ukuu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja na Diwani wa Wadi ya Bungi Mhe Saidi Mtaji Askari, akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa Baraza la Vijana wa Unguja Kuu Wilaya ya Kati Unguja. 
Mwenyekiti wa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Kati Unguja Ndg Khamis Hamza Chilo, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo wa Baraza la Vijana Shehia ya Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja.
Vijana wa Shehia ya Unguja Kuu wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said akihutubia wakati uzinduzi huo.
Msanii wa Ngogoti akionesha umahiri wake wakati wa uzinduzi huo. akicheza na nyoka aina ya chatu
Wasanii wa Kikundi cha Sarakasi cha Bungi wakinesha umahiri wao.





Kikundi cha Wasanii wa Dance wa Bungi wakionesha umahiri wa kudance wakati wa hafla ya uzinduzi huo.

Sheikh Mohammed Suleiman akisoma dua baada ya kumalizika hafla ya Uzinduzi wa Baraza la Vijana Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akizungumza nma Viongozi wa Mabaraza ya Vijana ya Shehia za Unguja Ukuu wakati wa kumalizika kwa hafla hiyo ya Uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya mpira vya Idumu Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja.
 Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com
Zanzinews.com.



Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu fahirisi za bei za taifa kwa mwezi Agosti, 2016. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja. 
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo

Na Dotto Mwaibale

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipindi cha mwezi Agosti Umepungua kwa asilimia 4.9 kutoka asilimia 5.1 katika kipindi cha mwezi Julai 2016.

Hiyo inamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa  kwa mwaka ulioisha mwezi Agosti, 2016 imepunguwa ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwezi Julaai 2016.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa NBS, Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema Nchi zote za Afrika Mashariki kasi ya mfumuko wa bei imepuguwa katika kipindi cha mwezi Agost mwaka huu.

Alisema baadhi ya nchi hizio ni  Kenya Mfumuko wa bei umepunguwa kwa asilimia 6.26 kutoka asilimia 6.36 katika kipindi cha mwezi Julai na Uganda bei imepunguwa kwa asilimia 4.8 kutoka asilimia 5.1 kwa mei Julai Mwaka huu.

"Kupungua kwa mfumuko huo nhini kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali ya nchi," alisema Kwesigabo .

Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa z vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na bei za Samaki kwa asilimia 701, Mafuta ya kupikia kwa asilimia 7.02 na mbogamboga kwa ailimia 6.9.

Pia bidhaa zisizo za vyakula  zilionesha kupunga ni pamoja bei za Gesi kwa asilimia 22.8, Mafuta ya taa kwa asiimia 8.8, dezeli asilimia 9.8 na Petroli asilimia 15.8.

Aidha Fahilisi za bei ambacho hutumika kupima mabadiliko ya bei za huduma mbalimbali  zimepungua kwa asilimia 103.28 kwa mwezi Agosti mwaka huu kutoka 103.50 katika kipindi cha mwez Agosti mwaka 2015.

Alisema kupungua kwa fahilisi za bei umechangiwa hasa na kupungua kwa baadhi ya bidhaa za vyakula ambazo ni nafaka kwa asilimia 0.6, Unga wa muhogo asilimia 2.1, dagaa kwa asilimia 3 na mbogamboga asilimia 2.6.

Hata hivyo alisema thamani ya shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma imefikia sh.96 na senti 83 katika mwezi Agosti mwaka huu kutoka desemba 2015 ilivyokuwa sh.96 na sent 62 kwa mwezi Julai mwaka huu.

Kwesigabo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi umepunguwa kutoka asilimia 7.6 kwa mwezi Julai hadi kufikia asilimia 7 kwa Agosti mwaka huu.



TANGA UWASA YAPATA TUZO

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella kushoto akipokea tuzo ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) ya ubora wa kimataifa,kupitia hati ya ISO 9001:2015 ulitokana na ushindi wa kuwa mamlaka bora ya hduuma za Maji Safi na Usafi wa Mazingira nchini kwa Mwaka 2014/2015 wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte kulia akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella walioipata mamlaka hiyo ushindi wa kuwa mamlaka bora ya huduma za maji na usafi wa mazingira nchini mwaka 2014/2015
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte kulia akimkabidhi tuzo hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katikati akiwa na kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi ambapo kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Mpya wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Salum Shamte,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Joshua Mgeyekwa wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdulla Lutavi na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Mkuu wa Tanga,Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) uliyoteuliwa na Waziri wa Maji
 Mkuu wa Tanga,Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) uliyoteuliwa na Waziri wa Maji ikiwemo wafanyakazi wa Mamlaka hiyo
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga ( Tanga Uwasa) na wafanyakazi wa mamlaka hiyo
MKUU wa Kitengo cha Uzalishaji Maji katika kituo cha Kusafishia Maji Mabayani Jijini Tanga,Faraji Nyoni akimueleza mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella namna uzalishaji wa maji uzalishaji unavyofanyika na usafishaji wake kabla ya kuwafikia wananchi.
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imeweza kuwa mamlaka ya kwanza nchini kufikia vigezo vya kupewa leseni ya EWURA ya Daraja la kwanza (Class 1Lesence).

Leseni hiyo ilitolewa Juni 17 mwaka huu na Waziri wa Maji na Umwagiliaji katika mkutano wa kuzindua ripoti ya mwaka 2014/2015 ya mamlaka za maji uliofanyika Mjini Dodoma.
Akizungumza mwishoni mwa wiki,Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ,Felix Ngamlagosi  alisema kuwa leseni hiyo ilitolewa kwa Tanga Uwasa na kwa sasa ndio mamlaka ya maji pekee nchini iliyo na leseni ya EWURA ya daraja la kwanza nchini.

Alisema kuwa leseni hiyo ya daraja la kwanza imetolewa baada ya EWURA kupitia utendaji kazi wa Tanga Uwasa na kutadhimini viwango vilivyowekwa ili mamlaka ya maji kuweza kupata daraja la kwanza na kujiridhisha kuwa vimefikiwa.

Aidha alisema vigezo ambavyo vimeangaliwa kuwa mamkala bora ni kugharamia uendeshaji wa mamlaka,kugharamia uchakavu wa miundombinu na kuweza kulipia riba za mikopo ya uwekezaji.

  "Lakini pia uwezo wa Mamlaka hiyo kujitegemea kiufundi na kiuendeshaji"

Mkurugenzi huyo alisema kuwa mamlaka hiyo imeweza kuwa ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo miongoni mwa mamlaka kubwa 25 za maji zinazotoa huduma katika makao makuu ya mikoa Tanzania bara.

  Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema wao kama mamlaka wataendelea kuhakikisha wanatoa huduma bora zinazoendena na viwango vikubwa ili kuendelea kuwa mamlaka bora nchini.

Alisema pamoja na changamoto walizokuwa nazo lakini wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha wanakabiliana nazo kwa kuwawezesha wananchi waweze kunufaika ana huduma ya Maji kwa kiwango kikubwa .

"Lakini pia sisi kama mamlaka tumejiwekea mipango kabambe ya kuhakikisha huduma za maji zinaimarika sambamba na kujiandaa na fursa ya ujio wa bomba la mafuta utakaoanzia nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga ili changamoto ya maji isiwepo wakati wa ujio wa fursa hiyo.
habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
nh4
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kimbembe Auction Mart wakitoa Samani za kampuni ya Centre Point Limited Mpangaji wa Shirika la Nyumba NHC  nyumba kitalu Namba 2008/93 iliyopo Mtaa wa Indira Ghandhi katikati ya jiji la Dar es salaam Septemba 8, 2016
nh2
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kimbembe Auction Mart wakitoa Samani za kampuni ya Centre Point Limited Mpangaji wa Shirika la Numba NHC Katika nyumba Plot Namba 2008/93 iliyopo Mtaa wa Indira Ghandhi jijini Dar es salaam kwa kushindwa kulipa kodi ya pango kiasi cha shilingi Milioni 96, tukio hilo limefanyika leo asubuhi.
nh3
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kimbembe Auction Mart wakitoa Samani za kampuni ya Centre Point Limited Mpangaji wa Shirika la Numba NHC Katika nyumba Plot Namba 2008/93 iliyopo Mtaa wa Indira Ghandhi jijini Dar es salaam
nh4
Vitu mbalimbali vikitolewa ndani vikiwemo viti.
nh5
Baadhi ya vifaa mbalimbali vya kampuni hiyo vikiwa tayari vimetolewa nje.
nh7
Mmoja wa wanafamilia ambaye hakutaka jina lake litajwe akishuhudia tukio hilo wakati wafanyakazi hao wakiendelea kutoa vitu mbalimbali katika nyumba hiyo

GERMAN BUSINESS DELEGATION EXPLORING BUSINESS OPPORTUNITIES IN TANZANIA

SERIKALI YA UJERUMANI YATOA MSAADA WA FEDHA YURO LAKI NNE KWA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

04
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava pamoja na Mkuu wa program ya Maji toka Ubalozi wa Ujerumani Bw. Ernst Doring wakisaini hati za makubaliano ya Serikali ya Ujerumani kuisaidia Ofisi ya Makamu wa Rais kiasi cha fedha yuro laki nne kwa jaili ya kuendesha program za mabadiliko ya tabia Nchi.
01
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava akikaribisha ujumbe toka Serikali ya Ujerumani uliofika Ofisi kwake Mtaa wa Luthuli jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kuisaidia Ofisi ya Makamu wa Rais kiasi cha fedha yuro laki nne kwa ajili ya shughuli za mabadiliko ya tabia Nchi.

COMMUNIQUÉ: 17TH EXTRA- ORDINARY SUMMIT OF HEADS OF STATE OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY

(L-R) H.E Paul Kagame of the Republic of Rwanda, H. E. Hon. Aggrey Tisa Sabuni, Presidential Envoy of the Republic of South Sudan and H.E William Ruto, Deputy President The Republic of Kenya.
EAC Heads of State and Ministers in charge of Foreign Affairs and EAC matters during the closed session
H.E Ali Mohamed Shein, President of Zanzibar; H. E. Hon. Aggrey Tisa Sabuni, Presidential Envoy of the Republic of South Sudan; H.E Paul Kagame of the Republic of Rwanda; Dr Antony Kafumbe, Counsel to the Community(EAC) and H.E Dr John Pombe Magufuli, President of the United Republic of Tanzania and Chair of the EAC Summit during the closed session.

TORAJAN KABILA LINALOWAFUKUA WALIOKUFA KILA MWAKA NA KUWAVALISHA NGUO MPYA

MANCHESTER UNITED VS MANCHESTER CITY MCHEZO WENYE USAJILI GHALI KATIKA HISTORIA

Mchezo wa kesho wa timu za Jiji Manchester za Manchester United na Manchester City unatarajiwa kuwa mchezo ghali kuliko yote duniani katika historia ya soka kutokana na timu hizo mbili kwa pamoja kutumia paundi milioni 600 kwa usajili kuimarisha vikosi vyao.

Zikiwa na makocha mpya timu hizo mbili za Manchester, United wakiwa na Jose Mourinho na City wakinolewa na Pep Guardiola wenye upinzani wa jadi wote walimwaga fedha kuhakikisha wanajijenga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
                        Paul Pogba amesajiliwa kwa kitita kinachofikia paundi milioni 100
                               Beki John Stones alisajiliwa kwa kiasi cha paundi milioni 47.5

WATALII WAKWAMA KWENYE MAGARI YA JUU YA MLIMA NA KULALA USIKU MMOJA

SERENA WILLIAMS APOTEZA NAFASI YA KUENDELEA KUWA NAMBA MOJA

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUJIKITA KATIKA UFUGAJI KUKU

                                                                                             Na Woinde Shizza,Arusha.
 

Wajasiriamali nchini wametakiwa kujikita katika Ufugaji wa kuku wa Kienyeji na kisasa ili waweze kunufaika kiuchumi kufuatia ongezeko la uhitaji mkubwa wa mayai na nyama katika maeneo ya mengi hususan kwa wafanyabiashara wa vyakula.

Hayo yameelezwa na Mjasiriamali Boniventura Shiyo anayejihusisha na ufugaji huo amesema kuwa kwa sasa biashara hiyo imemuongezea kipato ambacho anakitumia kujiletea maendeleo pamoja na kuendesha familia pasipo kuyumba.

Mjasiriamali huyo amewataka Watanzania kujenga tabia ya uthubutu kwani soko la biashara ya kuku ni kubwa na linazidi kukua kila kukicha.

Hata hivyo Boniventura amesema kuwa kwa sasa anatumuia mashine maalumu ya inayototoa mayai na kuwa vifaranga maarufu kama incubator ambayo imemuongezea fursa ya kuwa muuzaji wa vifaranga pia.

Biashara ya ufugaji wa kuku ni moja kati ya biashara zinazoshamiri kwa kasi katika maeneo mingi nchini hususan maeneo ya mijini ambapo ndipo masoko makubwa yanapatikana kutokana na idadi kubwa ya watumiaji wa bidhaa za mayai na nyama ya kuku.

No comments :

Post a Comment