Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akielezea siku ya
kisomo duniani na dhumuni la UNESCO kuanzisha siku hiyo.
Kaimu
Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw.
Nicholaus Bureta akizungumzia juhudi za serikali za kuhakikisha kila
mtanzania anajua kusoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, Basilina
Levira akitoa taarifa jinsi hali ilivyo kwa watu wazima ambao wanajua
kusoma na wasiojua kusoma.
Afisa
Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo akielezea mradi wa XPRIZE ambao
unasimamiwa na UNESCO ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa
kutumia uwezo walionao watoto katika maeneo mbalimbali nchi
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akitoa maelezo
kuhusu Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM).
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akimkabidhi mgeni
rasmi, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta, Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani
2016 (GEM)
Wageni
waalikwa katika maadhimisho ya siku ya kisomo duniani wakionyesha
Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM) wakiongozwa na Mkuu wa
Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez (wa kwanza kushoto).
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akimkabidhi mgeni
rasmi, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta, sanduku la Ripoti ya Ufuatiliaji wa
Elimu Duniani 2016 (GEM).
Mgeni
Rasmi katika maadhimisho ya siku ya kisomo, Kaimu Kamishna wa Elimu
kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta
akigawa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM) kwa baadhi ya
wafanyakazi wa wizara yake.
Na Mwandishi wetu
Katika
kutambua umuhimu wa kusoma na kuandika Tanzania na mataifa mengine
duniani zimeungana kwa pamoja kuadhimisha siku ya Kisomo Duniani ambayo
huadhimishwa kila Septemba, 8 ya kila mwaka ambapo pamoja na maadhimisho
hayo pia iliambatana na Uzinduzi wa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu
Duniani (GEM).
Akizungumza
katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi.
Zulmira Rodriguez alisema kuwa dhumuni la UNESCO kuweka siku hii ya
Septemba 8 kila mwaka kuwa siku ya kisomo kimataifa ili kuziunganisha
jamii zote za kimataifa duniani kuweka na kuendeleza nguvu na juhudi kwa
watu kujua kusoma na kuandika ili kuleta maendeleo katika jamii
mbalimbali.
“Kauli
mbiu hii inatufungulia milango ya uelewa juu ya malengo na mafanikio ya
miongo mitano iliyopita ambayo yaliwekwa ya kutaka kila mtu anajua
kusoma,” alisema Bi. Rodrieguez na kuongeza.
“Tunataka
kujua ni changamoto gani zinazoikabili sekta ya elimu katika kusoma na
kuandika na tunataka kufahamu namna ya kukabiliana na changamoto hizo
ili kufikia malengo ambayo UNESCO iliyakusudia kufikiwa ya kila mmoja
awe anajua kusoma.”
Kwa
upande wa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Kaimu Kamishna wa Elimu
kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta
ambaye alimuwakilisha Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo alisema
serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imejizatiti
kuondoa tabaka la wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa vijana na
watu wazima kwa kujenga uwiano sawa wa utoaji wa elimu kwa watu wote.
“Wizara
imejipanga vizuri, na lengo kubwa la wizara ni kuhakikisha tunakuwa na
mtanzania aliye elimika na aliye na stadi, maarifa na uwezo wa kutumia
elimu aliyoipata,” alifafanua Bureta.
Vile
vile Bw. Bureta amesema kwa sasa wizara ipo kwenye mpango wa kukuza
stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) ambao unaanzia chini kwa
wanafunzi wa awali mpaka shule za msingi.
Katika
mpango huo walimu wamekuwa wakipata mafunzo mbalimbali ya namna ya
kumuwezesha mwanafunzi kujua Kusoma Kuandika na Kuhesabu katika ngazi ya
elimu ya awali.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya
Mfumo Rasmi, Basilina Levira amesema kwamba kwa mujibu wa sensa ya mwaka
2012, asilimia 78 ya vijana na watu wazima ndio waliokuwa wakijua
kusoma na kuandika.
Akaongeza
kuwa mwaka 2015 idadi hiyo ya wanaojua kusoma na kuandika ilishuka na
kufikia asilimia 77 ambapo ilipelekea wizara hiyo kutoka na mikakati
inayokusudia kuondoa kabisa tabaka la watu wasiojua kusoma na kuandika
nchini.
Aidha,
Basilina amesema kuwa Serikali ilipitisha sheria ya vyumba vya madarasa
ya shule zote nchini kutumika kufundishia vijana na watu wazima ambao
hawajui kusoma na kuandika muda wa jioni baada ya wanafunzi wa kawaida
wanapomaliza masomo yao.
Amefafanua
kwa kusema kuwa, wizara imeandaa programu ambayo iko kwenye mfumo wa
Televisheni na picha za video (DVD) yenye masomo 65 ya kujifunza kusoma,
kuandika na kuhesabu, ambapo kwa kutumia programu hiyo mwanafunzi
anaweza kujua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa muda wa miezi 4 mpaka 6.
Mafunzo
hayo kwa njia ya Televisheni na Picha za Video tayari yameanza kutumika
kwa wilaya za Ilemela, Dodoma Manispaa, Songea Manispaa, Bagamoyo,
Mkuranga, Temeke, Ilala na Kinondoni, ambapo asilimia 65 ya vijana na
watu wazima wasiojua kusoma na kuandika wamejitokeza kujiunga na Elimu
hiyo huku idadi kubwa ikiwa ni ya wanawake.
Siku
ya Kisomo Duniani huadhimishwa Duniani kote kila ifikapo Septemba, 8 ya
kila ya mwaka, ambapo mwaka huu 2016 maadhimisho hayo yametimiza miaka
50 tangu yalipoanza kuadhimishwa mwaka 1966.
Kauli
mbiu ya siku ya kisomo duniani kwa mwaka huu ni ‘Tunasoma yaliyopita,
Tunaandika yajayo, Elimu endelevu’ ambayo kwa lugha ya kiingereza ni
‘Reading the future, Writing the past’.
Mgeni rasmi, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta akionyesha Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM) baada ya kuipokea kutoka kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez |
MKUU WA MKOA MARTINE SHIGELLA ATEMBELEA BANDARI YA TANGA
Kushoto ni Kaimu Meneja wa
Bandari ya Tanga,Henry Arika akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martine Shigella wa kwanza kulia aliyekaa kwenye boti wakati
alipofanya ziara ya kuitembelea bandari hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine
Shigella wa kwanza kulia akitazama maeneo ya bahari akiwa kwenye boti
wakati alipoitembelea kuona namna ya utendaji wao katikati ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na kushoto ni Kaimu Meneja
wa Bandari wa Tanga Henry Arika
Kaimu Meneja wa Bandari ya
Tanga,Henry Arika wa pili kutoka kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa
Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kulia wakati alipofanya
ziara ya kuitembelea Bandari hiyo kuona namna inayofanya kazi kwa
ufanisi,
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akipanda ngazi kuelekea kwenye meli ya mizigo iliyotia nanga bandari ya Tanga wakati wa ziara yake ya kuitembelea Bandari hiyo |
Katibu Tawala wa Mkoa wa
Tanga,Mhandisi Zena Saidi akipanda ngazi kuelekea kwenye meli hiyo
akifuatiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga,Faidha Salim wakati wa
ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
Kaimu Meneja wa Bandari wa Tanga
Henry Arika akipanda ngazi kuelekea kwenye meli ya mizigo iliyotia nanga
kwenye bandari ya Tanga wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martine Shigella kuitembelea Bandari hiyo kuona shughuli zake
anayefuatia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine
Shigella katikati akiteta jambo na PRO wa Mamlaka ya Bandari ya
Tanga,Moni Jarufu wakati wa ziara yake
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine
Shigella wa kwanza kushoto akionyeshwa kitu na Katibu Tawala wa Mkoa wa
Tanga,(Ras) Mhandisi Zena Saidi wakati wa ziara yake ya kuitembelea
Bandari hiyo jana
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine
Shigella kushoto katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi
Zena Saidi wakiteta jambo wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa kuitembelea
Bandari hiyo kuona namna inayofanya kazi zake kulia ni PRO wa Bandari ya
Tanga,Moni Jarufu
(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha Blog)
Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza,
Projestus Rubanzibwa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza,
kwenye kikao cha Utambulisho wa Mradi wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya
Wakunga katika maeneo ya Vijijini katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda
ya Magharibi, kilichofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Amesisitiza kwamba Wakuu wa Vyuo vya vya
Ukunga nchini wanao wajibu wa kuhakikisha kwamba wanatoa mafunzo bora
kwa wahitimu wa vyuo hivyo ili watakapohitimu masomo yao waweze kusaidia
kutoa huduma bora afya.
Mradi wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya
Wakunga katika maeneo ya Vijijini, unatekelezwa na Shirika la Jhpiego
kwa kushirikiana na Taasisi ya Wakunga nchini Canada, Shirika la Amref,
Serikari ya Canada, Taasisi ya Wakunga Tanzania na Wizara ya Afya
nchini, lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya kwa akina mama na mtoto
ili kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi maeneo ya Vijijini nchini.
Na BMG
Kaimu Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza,
Dr.Silas Wambura, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza,
ambapo amesema mkoa wa Mwanza unakabiriwa na upungufu mkubwa wa idadi wa
wakunga pamoja na vifaa tiba hali ambayo inasababisha kuwepo kwa vifo
vya akina mama na watoto.
Dr.Dustan Bishanga ambaye ni Mkurugenzi
wa huduma za Mama na Mtoto Shirika la Jhpiego, amesema lengo la mradi
huo ni kuhakikisha unaongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga maeneo ya
Vijijini hapa nchini ambapo wahitimu wa masomo ya Sayansi katika maeneo
hayo watakuwa wakipewa ufadhiri wa masomo kwa makubaliano ya kurudi
kwenye maeneo yao ili kutoa huduma za afya. Mradi huo unatarajiwa
kufikia tamati mwaka 2021.
Kikao cha Utambulisho wa Mradi wa
kuongeza ujuzi na idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini mikoa ya
Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi kilichofanyika hii leo Jijini
Mwanza.
Dr.Dustan Bishanga ambaye ni Mkurugenzi
wa huduma za Mama na Mtoto Shirika la Jhpiego, akizungumza na wanahabari
kwenye kikao hicho.
Martha Rimoy ambaye ni Mratibu wa Taifa
wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), amesema bado maeneo mengi nchini
yanakabiloiwa na upungufu wa Wakunga kutokana na idadi ya Wakunga
wanaohitimu vyuoni kutoendana na idadi ya ujenzi wa Zahanati na Vituo
vya Afya huku wengine pia wakishindwa kwenda kufanya kazi maeneo ya
Vijijini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mazingira duni.
Gustav Moyo ambaye ni Mkurugenzi wa
huduma za Uuguzi na Ukunga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, amesema hali ya upungufu wa Wakunga nchini hususani
maeneo ya Vijijini si nzuri hivyo Serikali inatumia jitihada mbalimbali
ikiwemo kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi ili kutatua
changamoto hiyo.
Amesema asilimia kubwa ya mikoa ya Kanda
ya Ziwa inakabiliwa na upungufu huo na kwamba Serikali itakuwa ikitolea
kipaumbele kwenye mikoa hiyo pindi inapotoa ajira kwa Wakunga.
Kikao hicho
kimewajumuisha wadau mbalimbali wa afya wakiwemo Wakunga, Waganga Wakuu
wa Wilaya na Maafisa Elimu ambao watakuwa na wajibu wa kuwahamasisha
wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi ili kuongeza idadi ya Wakunga.
Wadau wa afya kutoka Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Tabora, Kigoma na Mara wameshiriki kwenye kikao hicho.
BREAKING NEWS; MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN WAPATA AJALI, WASAIDIZI WAKE WAJERUHIWA
Hili ndilo gari lililoacha njia na
kupinduka kwenye msafarawa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan huko kijiji cha Nanguruwe mkoani
Mtwara leo Septemba 9, 2016.
MSAFARA wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassani ambao
ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Mtwara umepata ajali mapema leo
asubuhi Septemba 9, 2016, baada ya garilililobeba wasaidizi wake kuacha njia na
kupinduka.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
“Leo ikiwa ni siku yatatu ya ziara ya Mheshimiwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama yetu Samia Suluhu
Hassan, moja ya magari yaliyokuwa kwenye msafara namba ST 234 ilipata matatizo
ya kupinduka, na wasaidizi wanne wa Makamu wa Rais, wameumia lakini
wamekimbizwa hospital ya Ligula na wanaendelea na matibabu nahali zao
zinaendelea vizuri.” Amefafanua Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego
Taarifa za awali zinasema, watukadhaa waliokuwemo
ndani ya gari hilo akiwemo dereva wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Rufaa
Mkoani Mtwara, Ligula kwa matibabu.
Ajali imetokea
mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Mtwara
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa
rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa liliacha
njia na nusura lipinduke.
Picha
zilizotumwa kutoka eneo la tukio, zinaonyesha, Muhudumu wa afya
akiwahudumia majeruhi hao ambao walilazwa katikati ya barabara huku gari
linalodaiwa kuwabeba watu hao, likiwa nje ya barabara na limepondeka
Barabara ya kutoka mtwara kuelekea tandahimba si ya
kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha
magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
Wanaodaiwa kuwa wasaidizi wa Makamu wa Rais, wakipatiwa huduma ya kwanza baada la ajali hiyo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
akitembelea kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu
Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha kuchakata gesi
cha Madimba Mhandisi.Leonce namna gesi inavyopokelewa na kuchakatwa na
kusafirishwa kwa watumiaji
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu
Hassan akiangalia mfumo wa uendeshaji na usalama wa kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
.......................................................................
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyakazi wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo
Madimba mkoani Mtwara wawe wazalendo na wafanye kazi kwa bidii katika kulinda
na kuutunza uwekezaji huo mkubwa ambao serikali inautegemea katika uzalishaji
wa nishati ya umeme wakati taifa linaelekea kwenye nchi ya viwanda.
Makamu wa Rais ametoa kauli
hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi na watendaji wa kiwanda hicho baada ya
kutembelea kiwanda kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo kwa lengo la
kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo akiwa katika ziara
yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mtwara.
Amesema kiwanda cha
kuchakata gesi asilia ni hazina kubwa kwa
Taifa hivyo ni kikalindwa na kutunzwa ipasavyo kutokana na umuhimu wake katika
uzalishaji wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya nchi.
Makamu wa Rais pia amewashukuru
na kuwapongeza wafanyakazi wa kiwanda hicho cha kuchakata gesi asilia cha
Madimba na amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuwajali na kuwathamini
katika utendaji wao wa kazi na kwamba serikali itahakikisha wafanyakazi wa
kiwanda hicho wanapewa motisha ya kutosha ili waongeze maradufu utendaji wao wa
kazi ili malengo ya serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia viwanda
inatimia kwa sababu taifa litakuwa na nishati ya umeme ya uhakika.
Makamu wa Rais amewataka
watendaji wa Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC) ambalo linasimamia mradi
huo kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kusaidia huduma za jamii katika
vijiji vinavyozunguka mradi huo kila mwaka ili wananchi waweze kuwa walinzi wa
mitambo hiyo.
Akitoa maelezo mafupi ya
mradi huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe amesema
kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata gesi ya futi za ujazo milioni 210 kwa
siku.
Bw Donsun Lee ambaye ni
Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akikagua pump kwenye
moja ya kisima kwenye shule ya Msingi Makalala, anayetizama ni Mbunge wa
Mafinga Mjini Cosato Chumi
Bw Donsun Lee ambaye ni
Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akimsikiliza
kwa makini Mhandisi wa Maji wa Mji wa Mafinga Eng Eradius.
Baadhi ya wanafunzi
na waalimu wa shule ya Msingi Makalala wakiwa katika picha ya pamoja na Mrs Lee
na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi
Na Fredy Mgunda,Iringa
MBUNGE wa jimbo Mafinga
mjini Cosato Chumi ameendeleza juhudi zake za kuwatafutia maendeleo wananchi wa
jimbo lake kwa kufanya kazi kwa ukaribu na taasisi za kiserikali na zisizo za
kiserikali za nje ya nchi ya Tanzania pamoja na taasisi za ndani.
Hivi karibu balozi wa korea
nchini Tanzania Bw Song Geum Young akiwa na NGO ya Kutoka Korea ya World share alitembelea jimbo la mafinga mjini kwa lengo la kujionea
changamoto za jimbo hilo na kutafuta njia za kutoa msaada wa kutatua baadhi ya
changamoto hizo na walitoa msaada wa taa ndogo za solar kwa kaya masiki mia saba.
Baada ya balozi huyo kurudi
jijini Dar es Salaam alimuagiza Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving
Friends International Bw Donsun Lee kutembelea jimbo la mafinga mjini na
kuzifanyia tafiti kwa kina baadhi ya changamoto za jimbo hilo ambazo alikuwa
amezianisha hapo awali ili kuweza kusaidia kuzitatua.
Aidha mkurugenzi wa NGO ya
Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee
alifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za jimbo la mafinga mjini na kuzifanyia
tafiti changamoto zilizopo kama uhaba wa maji na kuahidi kuzitatua kwa kuwa
ameshazifanyia utafiti.
“Leo nimetembelea Shule za
Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo na Shule ya Sekondari Luganga na
nimejionea shida ya upatikanaji wa maji hivyo kwa kuwa NGO yetu inajihusisha
na uchimbaji wa visima hivyo tumewasilisha taarifa hizi makao makuu ya ofisi zetu na tunasubili majibu”alisema Bw Donsun Lee.
Bw Donsun Lee alimpongeza mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi kwa juhudi alizozifanya za
kuwashawishi kutembelea jimbo hilo na kujionea baadhi ya changamoto ambazo
wanaweza kuzitatua kwa kushiriana na mbunge huyo.
Katika ziara hiyo Bw Lee na
timu yake walitembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo
na Shule ya Sekondari Luganga.
Aidha baada ya tafiti hizo,
Bw Lee atawasilisha taarifa zake Makao Makuu ya NGO ya Serving Friends
International huko Seoul, Korea.
Nia ya kufanya tafiti hizo
ni kuiweka Katika Mipango Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa sababu ndo
utaratibu wa NGO hiyo ambayo kwa Sasa wanachimba visima mkoani Singida
Kwa upande wake mbunge wa
jimbo la mafinga Cosato Chumi amemshukuru Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya
Serving Friends International Bw Donsun Lee kwa kufanikisha kufanya tafiti
ambazo amejine mwenye na kuleta matumaini kwa wananchi wa jimbo hilo la kutatuliwa
tatizo la maji kwa kuchimbiwa visima na taasisi hiyo.
Chumi ameongeza kuwa haya ni
matokeo ya ziara ya Balozi wa Korea ambaye alitembelea jimbo la Mafinga Mwezi
mmoja uliopita na kujionea changamoto hizo.
Lakini mbunge Chumi
amewataka wananchi wa jimbo la mafinga kufanya kazi kwa kujituma na kuunganisha
na nguvu za mbunge wao ili kupata maendeleo kwa kasi inayotakiwa.
“Unakuta mbunge nahangaika
kuwaletea maendeleo wananchi wangu kama hivi mnavyoona lakini ukienda vijiweni
unakuta wananchi wanacheza bao,pooltable na wengi wanapiga soga zisizo na
malengo,wakati wangeutumia muda huo kufanya kazi jimbo la mafinga mjini
litakuwa na maendeleo ya kasi sio muda”.alisema Chumi
No comments :
Post a Comment