Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa
Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za
kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13,
2016
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Botswana
Luteni Jenerali Seretse Khama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa wa
Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa
Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Rais wa Kenya
Mhe william Rutto, Makamu wa Rais wa Namibia Mhe. Nickey Iyambo na Rais wa kwanza wa Zambia
Dkt. Kenneth Kaunda baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka
kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu
leo Septemba 13, 2016
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia
Suluhu Hassan akiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe william Ruttona wageni wengine
wakielekea jukwaani kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National
Heroes Stadium) jijini Lusaka ambako amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa
Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
Rais mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akiwasili kwenye uwanja
wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za
kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo
Septemba 13, 2016
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakiwa kwenye uwanja wa Taifa wa
Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka ambako kamwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za
kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13,
2016
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan akiwapongea Rais Edgar C' Lungu na Makamu wake wa Rais Mama Inonge
Mutukwa Wina baada ya viongozi hao kula viapo kwenye uwanja wa Taifa wa
Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka. Mama Samia amemwakilisha Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe hizo
Msanii Ben Pol
akiwa jukwaani kuwapagawisha wakazi wa Singida kwenye tamasha la Tigo Fiesta
lililofanyika uwanja wa Namfua usiku wa kuamkia jana.
|
FID Q akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta mkoani Singida katika viwanja vya Namfua usiku wa jana |
JUX akiwaburudisha wapenzi wa muziki waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Namfua mkoani Singida wakati wa tamasha la Tigo Fiesta usiku wa jana |
Niki wa pili akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa jana Mkoani Singida |
Malkia wa Uswazi Snura akiwa na madancer wake katika kuwapagawisha wakazi wa Singida katika usiku wa Tigo Fiesta usiku wa jana katika viwanja vya Namfua |
Maelfu ya wakazi wa SIngida waliojitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha kubwa la burudani Tigo Fiesta lilifanyika katika viwanja vya Namfua mkoani humo usiku wa jana. |
Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akielezea kampeni ya
USIKATE TAMAA na jinsi inavyoweza kubadili maisha ya watu waliokata
tamaa ya kufanikiwa kimaisha.kulia na Kaimu Meneja Masoko Msaidiz wa
Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige.
Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akizungumza kuhusu kampeni
ya USIKATE TAMAA, Kushoto ni mwanamuziki Shetta na kulia na Kaimu
Meneja Masoko Msaidizi wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL
Group), Zainul Mzige.
Mwanamuziki,
Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta akielezea safari yake ya muziki
hadi kufika hatua aliyopo sasa ambayo mwenyewe amesema kuwa kwake ni
mafanikio makubwa. Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group,
Fatema Dewji-Jaffer. kulia na Kaimu Meneja Masoko Msaidizi wa Mohammed
Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige.
Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akifafanua jambo katika
mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akiwa katika picha ya
pamoja na Mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta, kuashiria
kuwa kampeni ya USIKATE TAMAA imezinduliwa rasmi.
Na Modewjiblog
Kwa
kutambua hali ambayo inawakuta watu wengi katika jamii na kupoteza
matumaini ya kufanikiwa kimaisha, kampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited (MeTL Group) imefanya uzinduzi wa kampeni ambayo
imepewa jina la USIKATE TAMAA ikiwa na lengo la kuhamasisha watu
waliokata tamaa kuwa nao wana nafasi ya kufanikiwa.
Akizungumzia
kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer
alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kuleta matumaini mapya katika jamii
kwa watu ambao wamekuwa wakipoteza matumaini kutokana na hali ya ugumu
wa kimaisha ambayo imekuwa ikiwakabili.
Alisema
kampeni hiyo itakuwa ikitumia watu mbalimbali ambao wamefanikiwa na
watakuwa wakitoa historia zao katika maeneo mbalimbali ambayo
watatembelea, wakielezea jinsi walivyokuwa na maisha magumu hapo awali
na sasa wamefanikiwa kimaisha.
“Kuna
watu hawana uwezo na wanazungukwa na watu ambao wamekuwa wakiwaambia
kuwa hawawezi kufanikiwa lakini kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA
wataweza kupata matumaini kutoka kwa watu ambao walipita katika maisha
magumu na baadae wakafanya vyema,” alisema Fatema.
Mkurugenzi
wa masoko huyo aliongeza kuwa kampuni ya MeTL pamoja na kufanya
biashara lakini pia inaijali jamii na inapenda kuona watu wakifanikiwa
kimaisha hivyo kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA itaweza kusaidia watu wa
aina mbalimbali waliopo katika jamii ya kitanzania wakipata matumaini
mapya na kuongeza juhudi ili wafanikiwe.
“MeTL
kupitia chapa yake ya MO inataka kuona watu wakiendelea kupambana na
kufanikiwa, tunataka watu wafanikiwe na tuwape tuzo, tuwape sauti ya
kusikika na huu ni mwanzo tu, kampeni hii itafanyika kwa muda mrefu
zaidi,” alisema Fatema.
Kwa
upande wa mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali (Shetta) ambaye ametumika kama
mmoja wa watu ambao wamefanikiwa, alielezea safari yake ya kimuziki na
kusema kuwa awali alikuwa akiishi kwa moja ya wasanii wa muziki nchini
na alikuwa akifanya kazi za nyumbani kwa mtu huyo lakini akiwa na nia ya
kutafuta njia ya kutoka kimuziki na juhudi alizozionyesha zimemwezesha
kuwa moja ya wasanii waliofanikiwa nchini.
“Unaweza
kuwa unajiamini katika kipaji chako lakini bado watu wanakudharau, mimi
nimewahi kuishi na mwanamuziki mkubwa nchini lakini najijua nina kipaji
lakini kwakuwa nilikuwa natafuta njia ya kutoka kimuziki ilinibidi
nifanye hivyo,
“Ilikuwa
naosha gari lake, naosha vyombo na hata kumwogesha mdogo wake lakini
nilikuwa najua nini nafanya na nini nataka, msanii yule alikuwa
anafahamiana na watu wengi na mimi ikanisaidia kupata njia ya kutokea na
leo kwa hatua niliyofikia nimefanikiwa,” alisema Shetta
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Maghembe
Makoye akizungumza na waandishi wa habari wakati akifafanua mambo
mbalimbali kuhusu wafugaji walionyaganywa mifugo yao na uongozi wa
hifadhi ya Pori la akiba Katavi , Kushoto ni mfugaji anayelalamikia
kunyang'anywa mifugo yake Mayunga Gamasa na kulia ni mfugaji Charles
Mtokambali.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Maghembe
Makoyeakionyesha hukumu iliyotolewa na mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga
ili wafugaji hao warudishiwe mifugo yao kushoto ni Mayunga Gamasa
mfugaji na kulia ni mfugaji Charles Mtokambali.
..........................................................................................
NA MWANDISHI WETU
WAFUGAJI wa mkoa wa Katavi, wamemwomba Rais John Magufuli
kuwasaidia kurejeshewa mifugo yao 1,600 ambayo imeshikiliwa na watendaji
wa hifadhi ya Katavi.
Wamesema mifugo hiyo aina ya ng’ombe ilikamatwa Machi mwaka huu
na kufunguliwa kesi lakini baada ya kesi hiyo walishinda na kuamliwa
kurejeshewa ng’ombe zao lakini mpaka sasa amri hiyo haijatekelezwa.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
wamesema, kutokana na unyanyasaji wanaofanyiwa na watendaji hao wa
hifadhi, Rais Magufuli ambaye ni mtetezi wa wanyonge atupie jicho suala
lao na kulimaliza.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Maghembe
Makoye alisema wafugaji waliochukuliwa mifugo yao hivi sasa familia zao
zinaishi maisha ya shida kwani hawana njia mbadala wa kupata fedha na
ufugaji ndiyo tegemeo lao.
“Tunamwomba Rais Magufuli aingilie kati jambo hili ili
Watanzania hawa wanyomge wapate haki yao. Tunanyanyasika katika nchi
yetu, huku chini kuna watu wanaendesha serikali zao, hawajui juu kuna
Magufuli, tunamwomba sana Rais alione hili,” alisema Makoye
Alisema agizo la Rais la kuwataka wakuu wote wa mikoa kubaini na
kutenga maeneo kwa ajili wafugaji nchini limeshindwa kuchukuliwa kwa
uzito wake mpaka sasa hivyo umefika wakati wa kulifanyia kazi.
Katibu huyo alisema katika kufanikisha agizo hilo la Rais
Magufuli kwa ufanisi, wameomba kushirikishwa ili kumaliza migogoro
iliyopo kati ya wafugaji na wakulima.
Naye Mayunga Gamasa alisema kati ya ng’ombe hizo 1600 yeye zake
ni 552 ambazo kukamatwa kwake zimemfanya kuwa masikini huku familia
yake yenye watu zaidi ya 70 ikiishi kwa shida kwani chanzo cha mapato
ndiyo hicho kimeondoka.
“Mimi nina watoto 28, waijukuu 24, wake wane jumla na wasaidizi
kama watu 70, sasa ng’ombe hawa ndiyo msaada kwangu, lakini uongozi wa
hifadhi ya Katavi haitaki kutupatia licha ya kushinda kesi, tunaomba
Rais atusaidie” alisema Gamasa
Naye Charles Mtokambali mwenye ng;ombe zaidi ya 700, alisema
kunyimwa kwa ng’ombe hao kumebadili maisha yake kwani kwa sasa familia
yake haijui kesho yake, kutokana na watendaji hao wa hifadhi huku
akisema ana imani kubwa na Rais kwamba atalishughulikia suala hilo.
No comments :
Post a Comment